Watu wanne wafariki nchini Ghana kwajili ya maji ya upako!

mafutaJumla ya watu wanne wamefariki Jumapili nchini Ghana, walipokuwa wakikanyagana kwenye huduma ya “Maji ya Upako” katika kanisa la Synagogue Church of All Nations lililoanzishwa na Mtume TB Joshua wa Nigeria.

Msemaji wa polisi wa Mkoa wa Greater Accra kamanda Freeman Tetteh alisema wengine 15 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Mr Tetteh alisema waliokufa walikuwa wanawake watatu na mtu mmoja lakini umri haukujulikana.

Kufuatia vifo vya watu hao “polisi wameshauri viongozi wa kanisa kuacha usambazaji wa mafuta ya upako,” alisema.

Baadhi ya viongozi wa makanisa wamelaani jinsi anavyoendesha ibada zake, wakati wengine wamehoji historia yake kama mkristo.

Hata hivyo Mtume Joshua, amekanusha madai hayo kwamba hayana msingi na ni wivu kwa watu wanaotishiwa na mafanikio yake.

 

Imetoka Strictly Gospel (SG)

Posted in HOME | Leave a comment

Mambo ya Ambilikile Mwasapila wa Loliondo yameishia wapi?

Haleluya!
Jamani mimi niliongea mapema sana wakati huduma ya Loliondo inaanza! nlliposema haikutokana na Mungu, baadhi walisema nilaaniwe, wengine walisema nimekosa sadaka! wengine walisema namwonea wivu mch.ambilikile. Lakini kumbukeni niliwaambia neno moja! “Kama imetokana na Mungu itadumu”
siku hizi hii huduma sijuwi imeishia wapi! jamani hebu musikilize wachungaji wenu! maana Mungu husema nanyi kupitia kwao! msikimbilie miujiza tu, mingine ni mitego ya shetani. Ila Yesu anatupenda sote!

Posted in HOME | Leave a comment

Wakriso 2015 tuhakikishe CCM inatoka madarakani!

Mauaji na mateso makali yanayolikumba kanisa kwa sasa, halafu serikali ya ccm imekimya kama haina habari, ni bayana kabisa kwamba haitufai na wala haifai kuongoza nchi! imekuwa ni serikali inayoongoza kwa ubaguzi na upendeleo mkubwa! hasa kiongozi wake mkuu (rais kikwete) wakristo wanauawa, makanisa yanachomwa moto halafu yeye anachekacheka tu! hafai kuwa kiongozi, mimi nadhani anampango wa kuuangamiza ukristo nchini mwake! Bwana ampige kwa jina la Yesu! 2015 kura yako wape wagombea wakristo!

Posted in HOME | Leave a comment

Sherehe za Ishara na Miujiza, mwanza tar.19-23/06/2013

SHEREHE ZA ISHARA NA MIUJIZA

Poster A2

Pamoja na Mtumishi wa Mungu Mwinjilisti toka Sweden – Rev Johannes Amirtzer Pamoja na Band yake ya SOS PRAISE TEAM Toka Sweden Wakati wako ni SASA!!

Walete Wagonjwa na wenye shida mbalimbali nao wataombewa na kupokea MUUJIZA kutoka kwa MUNGU Kupitia kwa Mtumishi na Mpakwa mafuta wake Johannes Amirtzer – TOKA SWEDEN Ni VIWANJA VYA FURAHISHA – MWANZA JUNI 19 HADI 23, 2013 SAA 9:30 ALASIRI HADI 12:30JIONI KILA SIKU

HIIII SI YA KUKOSA MWALIKE NA JIRANI YAKO

Posted in HOME | 1 Comment

NENO LA YESU KRISTO, UJUMBE MAALUMU KWA WAENDAO MBINGUNI.

Watu ambao hawajaokoka ni dhahiri kwamba mioyoni mwao hawakuweka imani katika kristo Yesu hata kama walisikia neno la ushuhuda wetu mara elfu (EBRANIA 4:2), na hii ni uthibitisho kwamba kusikia tu haitoshi bali kuamini moyoni ili kupata haki. Hivyo basi kwa kuwa mioyo ya wanadanu imekuwa migumu kuamini hata baada ya kusikia, Mungu lazima ataiangamiza (YEREMIA 9:13-16). Sina maana ya kufunga mlango wa neema ya wokovu hapana, nafasi ya watu kuokoka bado ni kubwa sana hasa katika nyakati hizi ambazo ni za hatari, maana yangu ni kuwakumbusha  na kuwajulisha watakatifu  juu ya umuhimu wa kuomba kwa bidii juu ya watu ambao ibilisi ameweka mioyo ya jiwe ndani yao hata kushindwa kuamini na kujali wokovu mkuu namna hii ambao hakuna kupona pasipo huo. Tuombe kwamba wapelekao injili wapate kibali mioyoni mwao na kupanda mbegu ya Kristo katika udongo mzuri. Bila shaka mnajua maombi ya mwenye haki yafaa sana akiomba kwa bidii.DONT STOP PRAYING FOR THE SINNERS, THEY WILL CHANGE FOR SURE.

 

–ROM Kisoma Mussa–

Posted in HOME | Leave a comment

Kanisa acheni kumlaumu kikwete na serikali yake!

Kutokana na mateso makali yanayolipata kanisa la tanzania, kama wakristo kuuawa, makanisa kuchomwa moto n.k. Kumekuwepo minong’ono mikubwa na kelele nyingi kutoka kanisani kwenda serikalini, huku kanisa likimsonga rais kikwete kwamba ameshindwa kulilinda!
lakini ngoja nikuambie neno hili! Yesu alisema kanisa litaingia katika mateso makali! watu watakuwa wakiwaua watu wa Mungu wakidhani wanamfanyia Mungu Ibada! Haya mambo ndugu zangu Bwana wetu Yesu kristo alishayasema tangu zamani. Ni unabii ambao hauna budi kutimizwa, japokuwa kanisa linaonekana kana kwamba limesahau unabii huu, badala yake limekuwa likiilaumu serikali na hasa kiongozi wake mkuu rais kikwete. kwa hiyo suala la makanisa kuchomwa na wakristo kuuawa ni ishara ya kurudi kwake Bwana wetu. Lakini pia kumbukeni Biblia inasema heri watakapowaudhi, furahini maana thawabu yenu ni kubwa mbinguni.

Hii ndiyo hali halisi iliyopo kwa sasa! Kikwete hawezi kuzuia unabii kutimizwa! kilichopo hapa ni kumwomba Mungu sana ili atutie nguvu.

Bwana awabariki!

Ev.Moses mayila

Posted in HOME | Leave a comment

New hope ministry wako sengerema na mkutano!

Photo-0027Baadhi ya wahubiri kutoka New hope Ministry kwa sasa 30/05/2013  wako Sengerema mwanza na mkutano, waliopo sengerema ni Mwinjilisti Danford Kidosi na Mlima wa Makimbilio Band. wakati huo huo Moses naye ameongea kwa simu jana kwamba atakuwepo siku ya jumapili! nyote mnakaribishwa! Moto umewashwa! Yesu anainuliwa! utukufu unashuka! |Leteni wagonjwa na wenye matatizo mbalimbali wataombewa na kuponywa kwa jina la Yesu.

Sengerema 2013 Kwa Yesu!

Posted in HOME | 1 Comment