KITABU CHA KWANZA CHA MOSES MAYILA KIITWACHO “THE POWER OF GOD”

UTANGULIZI

Kitabu hiki kimeandaliwa na Mwinjilisti Moses Mayila wa Sengerema Mwanza Tanzania, kwa msaada wa Mungu kupitia maandiko matakatifu (Biblia) na kuhaririwa nay eye mwenyewe. Kitabu hiki kimeandaliwa na kusambazwa bure kabisa bila kodi yoyote, na hii ni kutaka kulieneza neno la Mungu na kutoa Msaada zaidi hasa kwa watu wanaohitaji msaada wa maandiko, “Binafsi nimeona kuwa ni vizuri sana kama nikisambaza vitabu hivi bila kumtoza mtu yeyote yule ushuru au gharama yoyote ya uchapaji, pia ninaamini kuwa Mungu atanibariki zaidi na zaidi katika jambo hili, ni wahubiri wengi sana Duniani wanafanya jambo hili lakini wanalifanya kibiashara zaidi kwa kuwatoza watu gharama ya juu zaidi ya ile iliyotumika kuandaa kitabu kile, Mimi Moses watu hao ninawaita ni watu wafanyao kazi kwa hila wakijali mapato yao na si kazi yake aliye juu. Kupitia kitabu hiki ninaamini kuwa utapata msaada zaidi katika maisha yako ya kiroho na hata katika maisha yako ya kimwili pia. Naomba usome kwa makini sana aidha katika kitabu hiki nimejaribu kuyafafanua baadhi kya maandiko ya Biblia na kuyaeleza kwa mapana zaidi.

SURA YA KWANZA

MSAADA WA MUNGU KATIKA MAISHA YA MWANADAMU

Biblia inasema katika kitabu cha Mathayo sura ya 11 mstari wa 28 hadi 31. Inasema kuwa “NJOONI KWANGU NINYI NYOTE MSUMBUKAO NA WENYE KUELEMEWA NA MIZIGO NAMI NITAWAPUMZISHA, JITIENI NIRA YANGU MKAJIFUNZE KWANGU MAANA MIMI NI MPOLE NA MNYENYEKEVU PIA WA MOYO NANYI MTAPATA RAHA NAFSINI MWENU. MAANA NIRA NIWAPAYO MIMI NI LAINI NA MZIGO WANGU NI MWEPESI”.

Haya ni maneno ambayo Yesu aliyasema wakati akihutubia katika baadhi ya mikutano aliyowahi kuifanya. Lakini katika haya, swali lililopo mbele ni kwamba kwa nini Yesu aliyasema haya? Yesu aliyasema haya akimaanisha kuwa kila laiyendani yake yaani aliyemkubali Yesu kuwa Mwokozi wa maisha yake hataona tabu tena, ni kama vile Biblia inavyosema katika kitabu cha Nabii Isaya sura 65 kifungu cha 19 hadi 25 inasema hivi “nitaufurahia mji wangu Yerusalemu wala kilio na maombolezo havitasikika tena ndani yake, wala hapatakuwa na mzee asiye timiza siku zake tena, maana mtoto ataishi miaka mia bali mtenda dhambi akiishi miaka mia amelaaniwa, watajenga nyumba na kuishi ndani yake watapanda mizabibu na kuvuna mtunda yake, wala hawatajenga akaishi mtu mwingine tena kwenye nyumba hiyo wala hawatapanda akavuna mtu mwingine tena. Ni kama zilivyo nyingi siku za mti na watu wangu wataishi kama hivyo. Wateule wangu watafurahia kazi za mikono yao. Wala hawatazaa kwa uchungu watakuwa ni watu waliobarikiwa na Bwana.

Hii inaonyesha vigezo vingi sana ambavyo Mungu huwapa wale wanaozishika amri zake. Hapo juu amesema kilio na maombolezo havitasikika mjini Yerusalemu. Hapa hana maana ya Yerusalemu pekee tu, bali ana maana ya watu wote wanaomcha yeye. Na aliposema kilio hakitasikika ndani yake ina maana kwamb atakomesha kila aina ya tabu, shida magonjwa, mateso na matatizo ya aina zote. Vile vile amesema hawatapanda akavuna mtu mwingine ana maana ya kwamba hawatajitaabisha bure maana shetani huharibu kile ambacho mwanadamu anakifanya ikiwa ni pamoja na mwanadamu mwenyewe. Biblia inasema mwivi kazi yake ni kuiba, kuchinja na kuharibu, ndipo Mungu akanena na Malaki akisema ‘NAMI NITAMKEMEA YEYE ALAYE MAZAO YAKO NA MIZABIBU YAKO HAITAPUKUTISHA MAJANI YAKE” hapa alikuwa na maana ya kwamba atamkemea shetani asiharibu kazi ya mikono yako, lakini hatamkemea kula matunda ya watenda dhambi bali ya wamchao yeye. Hii inamaanisha wazi kwamba Mungu humlinda amchaye, yeye na mali zake.

Kwa sababu hii na ndiyo maana Yesu alisema njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha. Kuna sehemu kubwa sana katika jamii hasa katika nchi za Kiislamu hususan Iraq, Tajikistani, Iran na nyinginezo wanaamini kabisa kwamba Yesu alikuwa ni Nabii tu na wao wnamwita Nabii Issa. Lakini mimi Moses ninakataa hadharani usemi huo ni uongo na upotoshaji wa hali ya juu sana. Hizi mbinu tu za shetani kutaka kuutenda ulimwengu kwa maneno yanayoonekana kuwa na maana hali ni ya uongo, kila siku shetani katika kazi zake hutumia kitu inachoitwa hila, Hila ni nini? Hila ni mipango mibaya. Shetani antumia hizi hila kuuteka ulimwengu kwa maneno yasiyokuwa na ukweli wowote ndani yake ambayo kwa mtu asikye na upeo wa kutosha katika Biblia ni lazima atayaamini. Jamii hii inaamini kuwa Yesu alikuwa ni binadamu tu wa kawaida kabisa kama wewe na alizaliwa na mwanamke kama ilivyo kawaida kwa wanadamu wote. Lakini ukweli kamili ni kwamba, Yesu ni Mwana wa Mungu, na kwa habari ya kuzaliwa na mwanamke ni kwamba, Yesu alichukuliwa mimba kwa miujiza kwa uwezo wa Mungu aliye juu. Biblia inasema katika kitabu cha Mathayo sura ya 1 kifungu cha 18 inasema hivi “HIVI NDIVYO KUZALIWA KWA YESU KRISTO KULIVYOKUWA, MARIAMU ALIKUWA AMEPOSWA NA YUSUFU LAKINI KABLA (HAWAJAKARIBIANA) MARIAMU ALIONEKANA KUWA NA MIMBA AMBAYO ILIKUWA NI KWA UWEZO WA ROHO MTAKATIFU”. Biblia hiyo hiyo imeendelea kusema katika Yohana 3 kifungu cha 16 KWA MAANA MUNGU ALIUPENDA ULIMWENGU NA HATA AKAMTUMA MWANAYE WA PEKEE ILI KILA AMWAMINIYE ASIPOTEE BALI AWE NA UZIMA WA MILELE. Hii inaonyesha wazi kuwa Yesu ni Mwokozi wa Wanadamu. Pia kuna siku Yesu aliwachukua baadhi ya wanafunzi wake akaenda nao mlimani kusali, walipokuwa huko wingu zito likawafunika na sauti ilisikika kutoka kwa wingu hilo ikisema “HUYU NDIYE MWANANGU MPENDWA NILIYEPENDEZWA NAYE MSIKILIZENI ATAKAYOWAAMBIA” hii ilikuwa ni sauti ya Mungu MARKO 9 kifungu cha 7. Vile vile kuzaliwa kwake alitabiriwa na Nabii Isaya kwamba Bikra atachukua mimba na atamzaa mtoto wa kiume atakey wachunga mataifa kwa fimbo ya chuma ISAYA 7 kifungu cha 16-16. Katika historia nzima ya dunia hakuna record ya mwanamke bikra ambaye alishawahi kuzaa mbali na Mriamu kumzaa Yesu, (Bikra yaani Mwanamke ambaye hajawahi kufanya tendo la ndoa tangu kuzaliwa kwake) pia Isaya alizidi kumtabiri huyu Yesu akisema “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa tumepewa mtoto tena wa kiume na uweza wa kifalme uko mabegani mwake (The Governmen of heaven) naye ataitwa mshauri wa ajabu Baba wa milele Mfalme wa amani jina lake. Maongeo ya enzi yake na amani haya mwisho kamwe. ISAYA 9 kifungu cha 6 – 7 inasemakana kwamba Isaya alimtabiri Yesu kabla ya miaka elfu moja (1,000) ya kuzaliwa kwake. Hivi vyote ni vielelezo vya kutosha kabisa vya kumtambulisha Yesu kuwa ni mwana wa Mungu na anauwezo wa kuratibu katika sector yoyote ile ya maisha yako. Nimeona kuwa kumbe kila wakati upatapo shida tatizo na mateso ya aina yoyote ile Yesu peke yake ndiye jibu. Na yeye ana mpango wa kukusaidia maadamu tu utakubali kufuata yale ambayo anataka uyafuate, wala hakuna kitu kisichowezekana kwake kila kitu kinawezekana LUKA 1kifungu cha 37. kwa maana moja, kila tatizo lako kwa Yesu lazima litatukuka tena kwa muda mfupi sana. Japo matatizo yamekukalia kwa muda mrefu sana siku ya leo naomba uamini kuwa yamefika mwisho, pamoja na kwamba umeombewa sana na watumishi wa Mungu mbali mbali leo utapokea muujiza wako.Hapatakuwa tena na kushindwa kufaulu kwako mwanafunzi, hapatakuwepo tena na utasa tumboni mwako mwanamke, hapatakuwa na ugomvi tena katika ndoa yako, maumivu yote ya ugonjwa wako yamefika mwisho leo, hautafukuzwa kazi tena na waliokufunza kwa muda mfupi kuanzia leo watakuletea barua ya kukutaka urejee kazini. Kila aina ya matatizo uliyo nay oleo yamefika mwisho.

Nimefanya maombi mara nyingi sana na watu wenye matatizo mbali mbali lakini meomuona Yesu akiwapumzisha papo kwa papo, nimeombea wagonjwa wengi sana ambao hata siwezi kukumbuka idadi yao, nimetoa huduma kwa wenye mapepo waliosumbuliwa na majini ya ukoo kwa muda mrefu sana, pamoja na wenye matatizo mbali mbali, papo kwa papo Yesu aliwaponya. Na wewe naomba uamini kupitia hiki kitabu matatizo yako yote yamekwisha.

MWISHO:

Weka kitabu hiki kifuani kwako kwa muda wa dakika tano ukiwa umefumba macho na kasha fumbua macho yako, kasha kagua ugonjwa uliokuwa nao, na kuhakikishia kuwa hautauona tena.

Baada ya hapo nenda zako ukiwa mzima ukasimulie ndugu, jamaa na rafiki zako mambo yote ambayo Mungu amekutendea.

BWANA WANGU YESU KRISTO NAOMBA UYATIMIZE MAMBO HAYA KWA MTU HUYU SAWA SANA NA UWEZO WAKO. AMINA

SURA YA PILI

NYAKATI ZA MWISHO

Inasemekana kuwa zamani Iraq ilikuwa ikiitwa Babeli,nchi hiyo ni miongoni mwa nchi maarufu sana duniani na ilishawahi kuitawala dunia nzima kisiasa na kiuchumi, nchi hiyo iliwahi kuongozwa na mtu mmoja jina lake Nebkadreza, ambaye alikuwa mfalme enzi hizo. Katika utawala wake yeye na jeshi lake waliondoka kwenda kuvamia huko Israel kipindi hicho Israel ilikuwa ikiongozwa na Mfalme Yeehoyakimu, katika vita hivyo mfalme Yehoyakimu alishindwa na watu wake wakachukuliwa mateka na mfalme Nebkadreza, miongoni mwa watu waliochukuliwa mateka alikuwemo kijana mmoja jina lake Daniel.

Siku moja Mfalme Nebkadreza aliota ndoto ambayo ilimsononesha sana katika moyo wake, lakini ndoto hiyo aliisahau, mfalme akawaita wachawi, waganga, wanajimu na wafuga majini ili wamwambie na wamfasirie ndoto hiyo, wote walishindwa wakamjibu hakuna mtu ambaye anaweza kulijua jambo hili ambalo mfalme analiomba isipokuwa ni miungu isiyoishi na wanadamu. Kwa kauli hiyo mfalme alikasirika sana akaagiza waganga, wafuga majini, wanajimu na wachawi wote wauawe.

Ndipo Daniel akamwomba mfalme asiwauwe hao watu, akamwambia yuko Mungu wa mbinguni ambaye atamwambia na kufasiria ndoto yake. Ndipo mfalme akamuuliza Daniel “Je unaweza kuniambia ndoto hiyo na ukaifasiri? Daniel akamjibu “Hakuna mwenye hekima, mchawi, wala mnajimu ambaye anaweza kuieleza siri ambayo mfalme anaiomba. Lakini yupo Mungu wa Mbinguni afunuaye siri, aliyemuonyesha mfalme Nebkadreza yale ambayo yatatokea siku zijazo.

Ndoto yako ee mfalme ilikuwa hivi: uliona ee mfalme mbele yako sanamu kubwa imesimama, sanamu hiyo ilikuwa ni ya kutisha sana. Kichwa cha sanamu hiyo kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu safi, kifua chake kilikuwa ni silver, kiuno chake na mapaja ni shaba, miguu yake ni chuma mchanganyiko na udongo. Wakati ulipokuwa unaendelea kuona haya likatokea jiwe kubwa ambalo halijatengenezwa kwa mikono ya wanadamu likaiponda miguu ya ile sanamu na kuisagasaga, ndipo chuma, udongo, dhahabu, na silver likazivunja vipande vipande kwa wakati ule ule na zikawa kama mapepe, upepo ukazipeperusha kwenda mbali. Lakini lile jiwe lililoiponda ile sanamu likakua na kuwa mlima mkubwa mpaka likaijaza dunia nzima”.

Daniel akasema Hii ndiyo ndoto yako ee mfalme ngoja nikufasirie, Mungu wa mbinguni amekupa uwezo, nguvu na mamlaka, na amewaweka watu, wanyama wa porini na ndege wa angani mikononi mwako wewe mfalme, popote wanapishi Mungu amekupa kuwa mtawala juu yao wote. Wewe ni kile kichwa cha dhahabu baada yako ufalme mwingine tena utainuka, baada ya huo, ufalme mwingine tena utainuka (shaba) utatawala juu ya Dunia yote, mwisho kutakuwa na tawala nne, ufalme wa chuma utakuwa na nguvu kuliko zingine hivyo utazipiga na kuziangusha zile zingine, kama ulivyoona miguu yake ilikuwa chuma mchanganyiko na udongo, huu utakuwa ni ufalme uliogawanyika upande mwingien utakuwa wenye nguvu na mwingine dhaifu. Kama ulivyoona chuma mchanganyiko na udongo watu watakuwa wamechanganyikana lakini hawana umoja kama chuma kisivyo shikamana na udogo. Katika wakati wa wafalme hao Mungu wa Mbinguni atapandisha ufalme ambao hautaharibiwa wala hautamwachia mtumwingine tena. Utaziharibu zile falme zote na kuziondosha lakini ufalme huo utadumu milele, hii ndio maana ya lile jiwe kuiponda ile sanamu. Hii ndiyo ndoto yako ee Mfalme. Daniel 2 kifungu cha 24-45.

Kufuatia ndoto hiyo ya mfalme, inasemekana kuwa kuna falme ambazo ziliinuka baada ya utawala wa mfalme Nebkadreza, miongoni mwa falme hizo ni pamoja na utawala wa Rumi, utawala wa Mjerumani na utawala wa Mwingereza. Lakini pamoja nahayo upo utawala ambao uemsemwa kuwa ni utawala uliochanganyikana chuma na udongo ambao watu wake watakuwa pamoja lakini hawana umoja, na huu ndio utawala nne katika mlolongo wa tawala zilizotajwa hapo juu. Nimetazama hivi sasa nimeona kuna jumuiya ambazo nchi nyingizimefanya lakini jumuiya hizo hazina umoja hata kidogo ndani yake, kwa mfano Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika, Jumuiya hiyo bado ipo haijavunjika lakini cha kushangaza raia wake hawapatani kabisa, hebu chukulia mfano kule nchini Afrika kusini, jinsi wageni walivyopigwa na kuuawa na raia wa Afrika kusini, chukulia mfano mwingine mzuri kabisa hapa nchini kwetu Tanzania, kuna umoja ambao ulifanywa na Raisi wa kwanza wa Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuziunganisha nchi hizi mbili na kuwa nchi moja na wakabadili hata majina ya nchi hizo, badala ya Tanganyika na Zanzibar wakaziita kwa jina moja la Tanzania, umoja huu umedumu kwa muda mrefu, lakini cha kushangaza hivi sasa raia wa Tanganyika (Tanzania bara) hawaruhusiwi kuingia Zanzibar bila hati ya kusafiria, sheria hii imewekwa mwaka 2008 na serikali ya Zanzibar, hii inaonyesha wazi kwamba watu hawa hawana umoja wa kweli kutoka mioyoni mwao, wana umoja midomoni tu. Na huu ndio utawala wa chuma mchanganyiko na udongo.

Mpendwa napenda kukujulisha kuwa, kama Daniel alivyosema kuwa baada ya utawala wa chuma mchanganyiko na udongo Mungu wa mbinguni atainua utawala wake ambao hautapita na hii ndiyo maana ya lile jiwe lililoiponda ile sanamu. Ninapenda kukujulisha kuwa jiwe hili ni Yesu Kristo ambaye Mungu wa mbinguni ammuweka kuwa kuhani milele. Waebrania 7 kifungu cha 24 pia anajulikana kama jiwe kuu la pembeni Zaburi 118 kifungu cha 12 na kama Daniel alivyosema kwamba jiwe hili (Yesu Kriso) litazivunja tawala hizo katika kipindi cha utawala wa chuma mchanganyiko na udongo ambao ndio utawala tulio nao sasa.

Hii inaonyesha wazi kwamba wakati wowote kuanzia leo Yesu atarudi kuihukumu Dunia na kuharibu tawala zote za Duniani, wala hatakuja kwa kutoa taarifa, bali atakuja kama mwivi, Ufunuo 3 kifungu cha 3 (“Tubu usipotubu naja kama mwivi) pia hakuna mtu ambaye anaifahamu saa ya kuja kwake maana inasemekana hata yeye mwenyewe Yesu haijui sik wala saa ya hukumu ya Dunia. Yesu mwenyewe alisema katika kitabu cha Mathayo 24 kifungu cha 36 (wala hakuna aijuaye siku wala saa iwe ni malaika wa mbinguni au mwana wa Mungu bali aijuaye ni baba peke yake) jambo hili linatuasa kujiweka tayari kwa kila saaa na kwa kila wakati kwa maana hatujui ni lini na saa ngapi atarudi.

SURA YA TATU

MAJARIBU

MAJARIBU NI NINI? – Majaribu ni kipimo ambacho hutumika kumpima mtu au kitu ili kutambua kuwa kinauwezo au anauwezo kiasi gani wa kufanya kazi katika sekta anayohitajika.

Inasemekana palikuwa na mtu mmoja jina lake Ayubu, mtu huyu ni miongoni mwa watu hapa duniani waliopata majaribu kwa kiasi kikubwa sana. Siku moja malaika walikwenda kujihudhurisha mbele za Mungu shetani naye akaenda kujihudhurisha mbele za Mungu, Bwana kamuuliza shetani “umetoka wapi wewe?” shetani akamjibu Bwana “nimetoka duniani kuzunguka zunguka huku na hna humo” ndipo Bwana akamuuliza “Je umemuona mtumishi wangu Ayubu? Kwani hakuna hata mmoja duniani aliye mkamilifu, mwelekevu na mwenye kujitenga na uovu na mwenye kumuheshimu Mungu kama yeye. Shetani akamuuliza Bwana “Je huyo Ayubu yuamcha Bwana bure? Wewe hukumzingira yeye na nyumba yake, umezibariki kazi za mikono yake makundi yake ya mifugo na ya kondoo yamesambaa nchini kote. Hebu sasa nyoosha mkono wako uyaguse hayo uone kama hatakufuru mbele yako. Bwana akamjibu Shetani “hayo yote yako mikononi mwako lakini usimguse yeye mwenyewe.AYUBU 1:6-12.Shetani akaondoka, siku moja watoto wa Ayubu walikuwa wakisherehekea ndani ya nyumba ghafla ukavuma upepo ukaangusha ile nyumba na wote kwa pamoja wakafa, wala hakusalia hata mmoja. Wakati huo huo wachunga mifugo wake wakavamiwa na majambazi na wakauawa isipokuwa mmojatu ndiye aliyebakia kumpelekea Ayubu habari, na baada ya kuuawa kwa wachungaji hao mifugo yote ilichukuliwa na majambazi hao.

Mtumishi wa Mungu Ayubu hakukufuru wala kumlalamikia Mungu, lakini mkewe alimshauri amkufuru Mungu ili afe, lakini Ayubu Mtumishi wa Mungu alimjibu mkewe kuwa wewe nawe u mmoja katika hao wanawake wajinga. Pamoja nahayo shetani aliona kuwa Ayubu bado amesimama na Imani yake shetani akaamua kumpiga Ayubu kwa Majipu mwili mzima ktoka uwayo hata kitosi cha kichwa chake, AYUBU 2 kifungu cha 7. Pamoja na kujaribiwa sana lakini Ayubu hakumkufuru Mungu wala hakufanya dhambi.

Hapa nimeona kuwa kumbe mtu ambaye anamcha Mungu kwa kumaanisha toka moyoni mwake kwanza Mungu huimarisha ulinzi wa kutosha kwa mtu huyo yeye pamoja na familia yake pamoja na mali zake, hii ina maana moja mke au mume au mtoto anapotangaza kumfuata Yesu usimzuie maanaKupitia yeye utapata rehema na ulinzi wa Mungu kwa sababu Mungu atamlinda yeye na familia yake pamoja na mali zake. Kwa maana nyingine shetani hataweza kumzuru mtu huyo maana Mungu amemzunguka, na ndiyo maana shetani alipoulizwa na Mungu kuhusu Ayubu alisema wewe (yaani Mungu) umemzunguka yeye na familia yake, kumbe ukimfuata Mungu nguvu zozote zile za shetani hazitakudhuru wala hazikutishi kwa sababu Mungu amekuzunguka, wala mchawi hakutishi akikuona hata kama alikuwa anaenda kuloga ataanza kutetemeka na kukimbia mbali na wewe.

Kitu kingine ukiumfuata Mungu kwa kumaanisha kabisa, kumbe Mungu atakubariki sana katika shughuli zako zote maana Ayubu alikuwa amembariki katika kazi za mikono yake na kuiongeza mifugo yake katika nchi. Lakini unapoamua kumfuata Mungu unatakiwa ufahamu kwamba kuna kitu kujaribiwa ndani ya hiyo safari, hivyo basi unatakiwa kujipanga kikamilifu ili kukabiliana na hayo majaribu yote utakayoyapata, mfano mzuri ni jamaa watatu vijana wa Kiebrania ambao ni Daniel Meshack na Abednego. Vijana hawa walilazimishwa kuabudu miungu ya mfalme wa Iraq, lakini vijana hawa walikataa kufanya hivyo mfalme huyo aliagiza wauawe. DANIEL 3:14-24 Mfalme akawaambia ni kweli kwamba ninyi mmkataa kuitumikia miungu yangu wala kuiabudu sanamu yangu? Sasa mtakaposikia sauti za filimbi na vinubi na kila aina ya muziki kama mtakuwa tayari kuanguka na kusujudia na kuiabudu sanamu yangunitawafanya vizuri sana, lakini msipofanya hiyo mtatupwa kwenye tanuru la moto, nitaona ni Mungu gani atakayekuja kuwaokoa mikononi mwangu.

Vijana hao wakamjibu mfalme “Ee mfalme Nebkadreza hatutaki kujitetea sisi wenyewe mbele yako katika jambo hili. Kama tukitupwa katika tanuru la motoyupo Mungu ambaye atakuja kutuokoa, hata kama asipotuokoa elewa ee Mfalme kuwa hatutaitumikia hiyo miungu yako wala kuiabudu hiyo sanamu yako” ndipo mfalme akakasirika sana akaagiza ile tanuru itiwe moto mara saba kuliko kawaida yake askari wakawafunga na kuwatupa katika atanuru hilo, kwa sababu ya ukali wa ule moto kiasi kwamba hata ukilisogelea tu lile tanuru unakufa, askari hao walikufa hapo hapo lakini cha kushangaza moto huo ulizikata zile kamba ambazo vijana hao walikuwa wamefungwa nazo, lakini haukuwadhuru wao hata kidogo. Mfalme akasimama akasema “hivi hatukuwatupa watu watatu tu ndani ya tanuru? Lakini mbona ninaona kuna watu wane wanatemea tu ndani ya tanuru hawajafungwa na wala hawadhuriki na moto, na huyo wa nne anaonekana kuwa ni mwana wa Miungu, (Mtu wa nne alikuwa ni Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai) ndipo mfalme akasimama akawaita vijana hao “Enyi Shadrack, Meshack na Abednego njoni nje ya tanuru, ndipo mfalme akasema “Na ahimidiwe Mungu wa Meshack, Shadrack na Abednego aliyemtuma malaika wake kuja kuwaokoa watumishi wake Meshack, Abednego na Shadrack ambao waliamua kuyapoteza maisha yao kwa ajili ya Mungu wao kuliko kujitia unajisi kwa kuabudu miungu mingine isipokuwa Mungu wao. Sasa ninaagiza mtu yoyote yule atakayesema neno kinyume na Mungu wa Vijana hawa atakatwa vipande vipande yeye na familia yake, maana hakuna Mungu mwingine anayeweza kuokoa namna hii.

Mpendwa wangu hapa tunaona wazi kabisa kwamba kumbe wakati wa kujaribiwa hautakiwi kuogopa uzito wa jaribu ni ahueni uyapoteze maisha yako kuliko kuupoteza uzima wa milele, hili hata Bwana wangu Yesu Kristo alilisema “Mwanadamu atanufaika nini kama akiupata ulimwengu wote kasha aukose uzima wa milele? Hapa kuna faida zaidi ya tatu, ya kwanza ukimshika Mungu sawa sawa kama Shadrack, Abednego na Meshack, Mungu mwenyewe atakutukuza, faida ya pili utapata uzima wa milele, faida ya tatu utasababisha na watu wasiomcha Mungu waanze kumcha Mungu kwa kasi nzuri sana. Kwa nini ninasema hivi? Kwa sababu mfalme alikuwa anaitegemea miungu yake lakini siku hiyo akasema hakuna Mungu anayeweza kuokoa kama Mungu wa Vijana hawa isitoshe akaagiza kwamba yeyote atakayesema neno kinyume na Mungu wa vijana hawa atauawa yeye na familia yake. Hii inaonyesha wazi kabisa kwamba kupitia Imani ya hawa vijana na miujiza ambayo Mungu aliifanya, Mfalme alimwamini sana Mungu wa Mbinguni na kuona miungu mingine haifai.

Kumbe katika imani yako unaweza kusababisha hata watu wengine waokolewe kupitia imani yako wewe hata unapokuwa katika kipindi cha majaribu, lakini unatakiwa ufahamu kwamba chanzo kikubwa cha majaribu ni shetani, yeye huenda mbele za Mungu na kuomba ruhusa ya kukujaribu, lakini kukujaribu anategemea kabisa kwamba atakuangusha. Lakini wakati ujaribiwapo Mungu naye yupo chonjo kukuangalia ni namna gani utamshinda shetani, na Mungu anapotoa ruhusa na wewe kujaribiwa huwa anataka wewe uyashinde hayo majaribu , pia ninamshukuru sana Mungu Baba Mwenyeezi kwa saababu huwa haruhusu kwetu yaje majaribumakubwa kuliko uwezo wa imani zetu soma 1WAKORINTHO 10 kifungu cha 13 biblia inasema hivi “Hakuna jaribu lililokubwa kuliko uwezo wako ambalo Mungu ataliruhusu likufikie ispokuwa ni lile lililo sawa na uwezo wako, pia Mungu ni mwaminifu hukuwekea mlango wa kutoke”.

Hii inaonyesha wazi ni jinsi gani Mungu anakupenda mimi naona kama vile Mungu humzihaki shetani kwa maana anapomruhusu akujaribu hamruhusu akujaribu zaidi ya uwezo wako, ina maana moja kwamba hamruhusu akuangushe wala akusumbue kiasi kwamba ushindwe kuvumilia. Hii ni thabiti kabisa kwamba shetani ni mjinga kwa sababu haiwezekani mtu akuagize kumuua nyoka lakini akuagize usimpige kichwani ila mkiani tu kweli utampiga hata mkia, lakini cha kushangaza huyo huyo aliyekuagiza kumpiga alipoona umemkata mkia anampa mkia mwingine tena anamwongezea na wa pili mbele yako. Je huyo mtu ni kweli kwamba anataka umuue huyo nyoka au anataka kukusumbua tu? Hapa nimeona kwamba Mungu humsumbua kijanja shetani, kwa sababu shetani hana busara halioni hilo. Mpendwa wangu napenda ufahamu kwamba hakuna jaribu linaloweza kukuua, pia hakuna jaribu linaloweza kudumu miaka yote ya maisha yako Mungu asiliondoshe. Mfano Ayubu watoto na mali zake wakati wa kujaribiwa vyote kwa mpamoja vilikwisha, lakini baada ya jaribu kupita alipata mara mbili zaidi ya yale aliyokuwa nayo mwanzo. Soma AYUBU 1 kifungu cha 1-3, hapa ilikuwa ni kabla ya kujaribiwa. Kisha soma AYUBU 42 kifungu cha 12 – 15, hapa ni baada ya kujaribiwa. Hivyo hivyo tumeona hata kwa hawa vijana wa Kiebrania akina Meshack na jamaa zake, baada ya kutoka katika tanuru la moto mfalme aliwaweka kuwa watumishi wa ngazi za juu sana katika ikulu ya Iraq.

Hapa moja kwa moja nimeelewa kuwa hata kama ulikuwa mtumwa kwa kumcha Mungu na kuvumilia katika majaribu Mungu atakufanya kuwa Mtawala. Hata kama ulikuwa maskini sana atakufanya kuwa Tajiri maana hata Ayubu aliishiwa kila kitu kwa maana moja alikuwa masikini lakini kwa kushinda majaribu alipata mara mbili ya yale ya kwanza. Lakini nimekuandalia mada hii ili kukujulisha kuwa unapoamua kumfuata Yesu elewa kuwa umetangaza vita, hata mambo ambayo ulikuwa huyapati utayapata hivyo basi kuwa mvumilivu katika hizo dhiki Mungu yupo pamoja na wewe wala hajakuacha. Jitahidi majaribu yako yasigeuke kuwa mateso kwako, nina maana moja kusema hivyo. Kuna tofauti kati ya majaribu na mateso mtu ambaye anapata mateso akiwa kwa Yesu huyo ndiye anajaribiwa ambapo asipotenda dhambi katika hayo mateso atapewa zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe. Lakini yule ambaye anapata mateso akiwa kwa shetani huyo yeye anateswa tu wala hatapata faida yoyote ile ya mateso yake.

Ninakusihi katika jina la Bwana wangu Yesu Kristo usitende dhambi ndani ya majaribu hayo ukaikosa zawadi ambayo Mungu alikuwa amekuandalia.

BWANA YESU AKUSAIDIE SANA UMSHINDE SHETANI

SHUKRANI

Ninamshukuru Mungu Baba Mwenyezi aliyezifanya mbingu na nchi kwa kuniwezesha kutengeneza kitabu hiki. Ni dhahiri kabisa kuwa kwa akili zangu tu mimi Moses nisingeweza kufanya kazi hii hasa kulingana na umri wangu kuwa ni mdogo sana. Vile vile ninamshukuru sana kwa kunifanya kuwa mtumishi wake katika umri mdogo sana.

OMBI LANGU KWAKO

Mpendwa wangu katika Bwana ninaamini Mungu wa mbinguni humpenda na humbariki sana yeye atangazaye habari zake duniani, hivyo basi ninakuomba mpendwa wangu kama ukiweza angalau uzalishe nakala moja tu ya kitabu hiki na umgawie mtu mwingine ili kuweza kusambaza msaada huu wa injili kwa watu wengi zaidi ulimwenguni mwote.

MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUFANYA HIVYO

MKAKATI NA LENGO LA KITABU HIKI

Mkakati na lengo langu ni kukisambaza kitabu hiki katika nchi zote zinazotumia lugha ya Kiswahili hususani Afrika Mashariki, na katika nchi zisizotumia lugha ya Kiswahili tayari nimeshaanza kukiandaa kitabu hiki kwa lugha ya Kiingereza. Kitabu hicho kitatoka hivi karibuni na kitaanza kusambazwa huko nchini Nigeria, Swazilandi, Marekani, Tahailandi, India na hata Tanzania pia. Lengo hasa la kufanya hivyo ni kueneza msaada zaidi wa maandiko duniani pote.

Hivyo basi ninakuomba uniombee sana kwa nguvu zako zote ili niweze kufanikisha suala hili, pia uniombee sana ili Mungu anitie nguvu zaidi niweze kumtumikia zaidi ya vile nilivyopanga kumtumikia.

BWANA AKUTENDEE YALIYO MEMA MAISHANI MWAKO.

AMINA

HAKI YA KURUDUFU

Kitabu hiki kinaruhusiwa kukizalisha na kukisambaza sehemu yoyote lakini kisambazwe bure kisiuzwe kwa gharama yoyote iwe ya juu au ya chini. Pia kitumika katika misingi ya Mungu na katika mashauri mema na si katika uhalifu. Hairuhusiwi kutumia neno lolote la kitabu hiki katika uovu wa aina yoyote ile.

ENDAPO UTAHITAJI MSAADA ZAIDI:

Wasiliana na mimi kupitia simu namba: 0755 961270 au +255 715961270

Barua pepe: mosesmayila@yahoo.com

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

3 Responses to KITABU CHA KWANZA CHA MOSES MAYILA KIITWACHO “THE POWER OF GOD”

 1. bet365 says:

  hi I was luck to discover your subject in baidu
  your subject is brilliant
  I get a lot in your Topics really thanks very much
  btw the theme of you blog is really wonderful
  where can find it

  Like

 2. tumaini says:

  amina mtumishi,uweza wa munu uwe juu yako kwa nguvu zaidi kufikisha injili ya bwana ,halelujah

  Like

 3. tumaini says:

  uweza wa mungu sorry,sio munu

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s