MUNGU WA WAISLAMU NA MUNGU WA WAKRISTO NI MMOJA AU NI WAWILI TOFAUTI?

Salamu ndugu zangu katika jina la Yesu kristo.

leo niko hapa kusema na wewe kuhusu mungu wetu na mungu wa waislamu kama ni mmoja yule yule au ni wawili tofauti. yamekuwepo maneno ya wanasiasa katika kutafuta namna ya kuiunganisha jamii kisiasa wakiwadanganya kwamba Mungu wa wakristo na Mungu wa waislamu ni mmoja! na wanasema hivi si kwa sababu hawajuwi ila wanakwepa kuwepo kwa mpasuko wa kidini bayana ya jamii wanayoiongoza. nataka nikuambie ukweli kwamba wanasiasa hawana muda wa kutaka kuwaunganisha watu na Mungu kwanza wengi wao wanaamini kwamba hakuna Mungu, kwa sababu wanasiasa wako chini ya philosophy hawako chini ya theology. kwa sababu imani ya philosophy ni kwamba hakuna Mungu, bali imani ya Theology ni kwamba kuna Mungu. nimekuja kugundua kwamba imani ya philosopy ni imani ya kipumbavu, kwa sababu biblia inasema katika Zaburi:53 mpumbavu amesema moyoni mwake hakuna Mungu. lakini hebu tuachane na hayo ngoja turudi kwenye mada yetu, wanasiasa wanafanya hivi kwa manufaa ya kisiasa lakini si kwamba husema hivyo kumuwakilisha Mungu.

Lakini ukweli uko wapi? Hivi nikweli kwamba Mungu wetu ni mmoja? Jibu ni hapana, kwanini jibu liwe hapana? kwasababu hizi:-

kwanza qruani inajua kabisa kwamba mungu wake si mungu aliyeumba mbingu na nchi! kwasababu hii ndiyo maan hakuna aya hata moja ndani ya qruani ambayo mungu wa qruani anasema kwamba “mimi ndiye niliyeziumba mbingu na nchi” bali utakutana na aya ikisema “mwenyezi Mungu aliziumba mbingu na nchi”

Pia ujulikane kwamba kila kitu hutambulika kwa majina yake. hata wanadamu hutambulika kwa majina ndipo mtu utapata kuelewa kwamba anayekusudiwa ni fulani. Mungu wa biblia anaitwa Niko ambaye niko, Yehova, Bwana wa Majeshi, Alfa na Omega. Lakini mungu wa qruani jina lake ni Allah, sasa hoja inakuja hapa ili sasa mimi Moses nikubali kwamba mungu wa waislam na Mungu wetu ni mmoja, ni andiko gani katika Biblia linalosema kwamba  Mungu jina lake ni Allah? pia ni aya  gani ndani ya qruani inayokubali kwamba mungu jina lake ni Yehova?

Lakini katika kufanya utafiti nimegundua kwamba Allah si Mungu wa kweli bali ni Shetani kwamujibu wa qruani surat muhamad aya ya 15. inasema hivi “mfano wa pepo aliyowaandalia waja wake mwenyezi Mungu iko hivi, ndani yake kuna mito ya maziwa na mito ya ulevi wenye ladha kwa wanywaji.humo watapata kuburudishwa kwa matunda ya kila namna na samahani kutoka kwa mola wao.” lakini ukisoma qruani hiyo hiyo sura ya 5 aya ya 90, inasema hivi: “Enyi mlioamini bila shaka ulevi na kamari na kuombwa yeyote asiyekuwa mwenyezi Mungu ni uchafu na ni kazi ya shetani.” sasa rafiki yangu kwa mujbu wa aya hizi hebu fikiria sasa aya ya kwanza imesema Allah katika pepo yake kuna mito ya ulevi, lakini qruani hiyo hiyo imesema ulevi ni kazi ya shetani, kama aya zenyewe ndizo hizi hoja yangu inakuja hapa: Yeye Allah kama siye shetani amepata wapi ulevi hali yakuwa ulevi ni wa shetani? lakini Biblia imesemaje kuhusu ulevi: walevi na wachawi na wazinzi hawataurithi ufalme wa mbinguni. Mungu anasema katika isaya Ole wao waamkao asubuhi na kufuata ulevi. mpendwa kuwa macho hizi ni nyakati mbaya za mpinga kristo.

wiki ijayo nitaweka hapa somo la mpinga kristo naomba usilikose, ni somo zuri linafundisha jinsi ya kumjua mpinga kristo na mpinga kristo ni yupi? kwa kifupi ni kwamba mpinga kristo sio mwanadamu kama watu wengi wanavyodai, pia  elewa kama mpinga kristo yupo duniani anafanya kazi kwa kiwango cha juu sana hivi sasa. naomba usikose tafadhali kusoma somo hili.

imeandaliwa na: Mwinjilisti Moses Mayila

email: mosesmayila@yahoo.com

mobile: 0715961270

0755961270

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

10 Responses to MUNGU WA WAISLAMU NA MUNGU WA WAKRISTO NI MMOJA AU NI WAWILI TOFAUTI?

 1. shaban says:

  NIMEISOMA HII MADA YAKO INAONEKANA KWANZA HAUIFAHAMU QURHAN HATA BIBLIA NNA MASHAKA NAYO, ULICHOANDIKA AU KUNUKUU KUTOKA KTK QURHANI SIVYO KABISA UMEDANGANYA

  Like

  • mosespk says:

   rafiki yangu si uchukue qruani usome utaona kama nimenukuu kweli au uongo, usitake kuleta ubishi usiokuwa na maana, watu wanasoma watakushangaa, kuwa na akili za kupinga jambo siyo ushabiki.

   Like

 2. anomous says:

  Huwa mara nyingi vijana wanahangaika kutafuta namna ya kutafuta kipato, sasa kuna njia nyingi sana za kutafuta kipato wengine huamua hata kumkosea mungu lkn wakati huo huo wanajifanya ni watu wa mungu kwelikweli, sasa kijana mwenzangu njia zipo nyingi za kutafuta kipato lkn hiyo unayotumia haifai.

  Basi km wewe ni mchungaji umeshafeli mapema kazi yako, mimi nakushauri ufanye kazi nyingine lakini sio hii ya kuzungumzia vitabu vya watu ambavyo haujavisoma wala huvijui vizuri, kumbuka hata hivi vitabu vya kidunia ambavyo wamevitunga wanaadamu wenzetu, mfano vya kisheria, ikiwa kutakuwa na kipengele hakifahamiki basi sio kila mtu anaweza kutoa ufafanuzi, mpaka hakimu, mwanasheria au bungeni.
  Nasema hivi ndugu yangu unafikiri kila kilichoandikwa ktk kitabu basi maana yake ni hivyo unavyoiona moja kwa moja. Ni bora ukaacha kuzungumzia vitu ambavyo huvifahamu na ukawaelekeza watu wako kile unacho kifahamu kuliko kuwadanganya itakuwa umefanya kosa kubwa sana kwa watu wako, kwako wewe mwenyewe na kwa mungu wako unaemjua wewe mwenyewe.

  Like

  • mosespk says:

   sio kama sikiielewi kitabu hiki nilichokizungumza hapa. lakini ushauri wako ni mzuri na mimi nimeona si vyema nizungumzie vitabu vya watu wengine, nitazungumza tu kitabu cha Mungu wangu ili wale wenye kumtafuta Mungu wapate kujifunza. nashukuru kwa ushauri wako, lakini kama wewe ulivyonishauri mimi na mimi nakushauri wewe naomba na wewe uutafakari ushauri wangu pasipo ushabiki, Naomba ujaribu kuwa Mkristo Biblia inasema onjeni muone ya kuwa Bwana ni mwema, naomba uonje Rafiki yangu, asante sana.

   Ev.moses mayila

   Like

 3. George says:

  Mosesi tatizo ni kwamba hata Shabani hajui hiyo qura-an yeye kakaririshwa tu lakini Biblia imetafsiriwa ktk lugha nyingi na Mungu ametusaidia imetafsiriwa kwa lugha yetu akatujalia roho mtakatifu ili tuielewe. Pia ajaribu kufikiri biblia imetaja mitume na manabii kabla na baada ya Yesu nawengine wote wamekufa na wapo makaburini hata huyo Mohamed (a.s) lakini Yesu mwana wa Mungu yupo hai na yupo mkono wa kulia Wa baba hata wenyewe waislamu wanajua hilo.

  Like

 4. Emeran Haule says:

  Mungu akubariki,
  akupe nguvu na uwezo wa kuendelea kumhubiri Yesu kwa kila kiumbe.
  Ukifuatilia historia utaona kuwa Waislamu wamewaua sana Wakristo kwa Jihads kwa mfano Afrika ya Kaskazini,
  Mashahidi wa Uganda nk, nkipata citations rasmi ntakutumia Mwinjilisti!
  Mungu akubariki kwa Jina la Yesu… Amina

  Like

 5. Kwa ukweli katika Jina la YESU Allah Mungu wa waislam siye Mungu wa kweli kabisa. Kwanza jinsi anavyo ombwa na waislam ni kimaajabu sana na kwa kushangaza.Eti Allah awezi kusikia sala ya muislam mpaka atakapo geukia KIBLA na ndio maana misikiti yote dunian waislam wanageukia kibla.na pia awezi kusikia sala ya muislam mpaka atakapo kuwa ametawaza au kuoga inamaana Allah anasikia kichefuchefu?mimi nashangaa sana, alafu pia awezi kusikia sala ya muislamu bila ya kuomba kwa kiarabu hii ni ajabu
  https://mosespk.wordpress.com/2011/02/03/mungu-wa-waislamu-na-mungu-wa-wakristo-ni-mmoja-au-ni-wawili-tofauti/

  Like

  • waJuhudi says:

   Mctoe maandiko bila kujua mantiki..ktk semi kadha wa kadha za madhehebu kadhaa wanaamini paradiso itakuwa na kila kitu na kule hakutakuwa na unajic na mbwa ataishi na paka,punda,simba na swala,chui,sungura,mwewe,kuku..bila kudhulumiana.lipi la ajabu..Yesu mwenyewe anausubiri mviinyo huo ktk paradiso Mark14:25someni mcbwatuke .

   Like

 6. Albert achevi says:

  Yesu ainuliwe mtumishi wa Mungu, naomba tu kwa jina la yesu, uongelee na kufafanua pia kuhusu Imani ya wakatoliki, kama imetoka kwa MUNGU mtakatifu. asante

  Like

 7. Zedd Hassan says:

  QURAN 5:72-73
  72. Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu!
  Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.
  TAFSIRI:
  Wenye kudai kuwa Mwenyezi Mungu yu katika Isa bin Maryam hata akawa yeye Mungu, kama wasemavyo Wakristo hii leo, hakika wamekufuru! Yeye Isa hana dhambi ya haya, kwani hakupata kudai hivyo hata mara moja. Bali yeye aliwaamrisha Wana wa Israili wamsafie imani Mwenyezi Mungu peke yake kwa kusema: Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye niumba mimi na nyinyi, na ndiye anaye niendeshea mambo yangu yote, na kwamba kila mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu malipo yake ni kuwa hatoingia Peponi kabisa, bali ataingia Motoni, kwa kuwa amekiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kuvunja mipaka yake hataepuka na adhabu.(Yesu kasema: “Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja.” Marko 12.28. “Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe”.Yohana 5.30 “Ninapaa kwenda kwa…Mungu wangu naye ni Mungu wenu.” Yohana 20.17 )

  Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja.
  Na ikiwa hawaachi hayo wanayo yasema, kwa yakini itawakamata adhabu chungu wale wanao kufuru
  TAFSIRI:
  Haiwi mwenye kudai kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja katika Utatu, kama wadaivyo Wakristo sasa, awe anamuamini Mwenyezi Mungu.!! Na hakika iliyo thibiti ni kuwa hapana mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja pekee. Na ikiwa hawa walio potoka hawatoacha itikadi zao potovu, wakarejea kwenye ut’iifu wa Mwenyezi Mungu, hapana budi ila itawasibu adhabu kali. (Biblia inasema kuwa ya kwanza katika Amri Kumi alizo pewa Musa ni: “Usiwe na miungu mingine ila mimi.” – Kutoka 20.3. “Wewe umeonyeshwa haya, ili upate kujua ya kuwa Bwana ndiye Mungu, hapana ila yeye.” – Kumbukumbu la Torati 4.35. Katika Injili ya Yohana 17.3 Yesu anamsemeza Mwenyezi Mungu: “Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.”)

  usipende kupost usichokuwa na elimu nacho. jiulize ikiwa yesu asingezaliwa ungekuwa unajiita mnini?/ wenda ungejiita mzedd ikawa dini yako.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s