VIZUIZI VYA KUKUA KIROHO

Salam katika jina la bwana wetu yesu kristo.

leo nipo hapa kukufundisha vizuizi vya kukua kiroho au mambo yanayokuzuia kuendelea katika imani. yesu alitoa mfano wa mpanzi aliyeondaoka kwenda kupanda mbegu,katika huko kupanda mbegu zingine zilianguka kando ya njia ndege wakaja wakazila, zingine zilianguka kwenye miiba, zikaota ile miiba ikazisonga zikashindwa kuendelea, zingine zilianguka kwenye mwamba zikaota lakini kwa kukosa mzizi jua likazipa zikanyauka. zingine zilianguka kwenye udogo mzuri zikaota zikakua zikazaa matunda moja thelathini, moja sitini na moja mia. yesu hakutuacha katika fumbo gumu hili bali alifafanua maana ya mfano huu, akasema “zilizoanguka kando ya njia ni mtu yule ambaye hulisikia neno na kulipokea mara kwa furaha lakini huja shetani na kuling’oa, zilizoanguka kwenye miiba ni yule ambaye hulisikia neno na kulipokea lakini kazi za dunia humsonga kiasi kwamba anashindwa kuendela na lile neno, zilizoanguka kwenye mwamba ni yule ambaye hulipokea neno lakini ndani yake hana mizizi na mara apatwapo na taabu huanguka.na zilizoanguka kwenye udongo mzuri ni yule mtu alisikiaye neno na kulipokea kisha kudumu nalo katika taabu zote na kuvumilia katika shida hata mwisho.

mpendwa wangu katika bwana, kumbuka leo nipo hapa kuzungumzia vizuizi vya kukua kiroho, hapa tumeona vizuizi vya aina tatu, yaani shetani, dunia na shida.aslimia kubwa ya waaminio duniani wanafahamu kwamba kizuizi cha kukua kiroho ni shetani, sawa wako sahihi lakini kumbe vipo pia vizuizi vingine ambavyo ni dunia na shida. hapa havijatajwa vizuizi vyote, pia vipo vingine vyenye nguvu sana kwa mfano: mwili, lakini hapa sipo kuzungumzia mwili bali shetani, dunia na shida.hapa tumeoa kwamba kumbe mtu anapolipokea neno huwa kuna nguvu ya upinzani ambayo hutoka katika ufalme wa shetani, dunia na shida zake. na nia ya upinzania huu ni kuhakikisha kwamba huendelei katika imani, maana nia ya shetani ni kuchinja kuiba na kuharibu.shetani hayuko duniani kuujega ulimwengu bali yuko kuupotosha ulimwengu ili kwamba watu wasimwelekee mungu bali wageukie katika njia ya upotevu ili siku ya kuhukumiwa kwake shetani aende nao motoni.biblia katika ufunuo wa yohana inasema ole wa nchi na bahari maana mwovu ametupwa kwenu akiwa mwenye uchungu mwingi hali akijua kuwa muda wake ni mfupi.lakini ikumbukwe kwamba mungu anapopanda neno lake ndani yako anahitaji kuliona likiota lakini mpango halisi sio kuota bali anahitaji kukuona ukikua katika neno, sera hasa sio kukua tu, bali sera halisi uzae matunda huo ndio mpango wa mungu, lakini dunia na mambo yake hujitahidi kuhakikisha kwamba huendelei katika neno, nakusihi ujitahidi umshinde shetani, dunia na mambo yake katika jina lipitalo majina yote, jina la Yesu kristo.

imeandaliwa na mwinjilisti moses mayila http://www.newhopeworldwideministry.wordpress.com
mosesmayila@yahoo.com

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

4 Responses to VIZUIZI VYA KUKUA KIROHO

 1. MWESIGWA KAMULALI says:

  NI MAFUNDISHO MAZURI, ISIPOKUWA SIKUWEZA KUJUA YAMESIMAMIA NENO GANI
  KATIKA BIBLIA. NAAMINI NI MUHIMU MAFUNDISHO YAONYESHWE YALIPOTOKA
  KWENYE BIBLIA(vitabu, milango na mistari). PIA SIJAONA UTATU MTAKATIFU UKIJITOKEZA.
  sina nia ya kukukatisha tamaa bali kukutia Moyo kuwa Mungu akubarikubariki na Roha Mtakatifu
  azidi kukuongoza katika huduma yako katika Jina la Yesu Kristo AMEN

  Like

 2. Ev eline william says:

  Praise God ni kweli kabisa hata mimi napenda kukuunga mkono mwana maombi mwenzangu kuwa hakuna kitu kizuri kama mistari itakayo tuongoza ili tuzidi kupanuka na kuijua biblia kwa wingi na kudumukatika kukua kiroho Mungu akubariki

  Like

  • MTUMISHI says:

   ndiyo kabsa mafundsho n mazuriiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa lakini yajengwe ktk neno kwa kwel yameleweka tena n msaada il tukuwe kiroho ila ambatanisha na neno n

   Like

 3. honest ludovick says:

  mungu akubariki mtumishi wa mungu ila injili hujengwa katika neno

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s