SHERIA YA MUNGU IMEFUNGWA KATIKA KILA MOYO WA MWANADAMU

Salamu ndugu zangu katika Jina la Yesu.

Leo niko hapa kuzungumza na nyinyi kuhusu sheria ya Mungu. Biblia inasema mwanangu zishike amri zangu uziandike katika kibao cha moyo wako. kwa hiyo tunajifunza kwamba kumbe sheria ya mungu hukaa katika moyo wa mwanadamu! kichwa cha habari kinasema kwamba “SHERIA YA MUNGU IMEFUNGWA KATIKA KILA MOYO WA MWANADAMU” bila kujali mwanadamu huyo anadhambi lakini sheria ya mungu imefungwa moyoni mwake, kumbuka kwamba dhambi huja palipo na sheria kama hakuna sheria dhambi haihesabiwi.

Katika kila moyo wa mwandamu kuna sheria ya Mungu imefungwa katika moyo huo, na sheria za Mungu ni kama: “Usiibe, Usiseme uongo, Usizini, Usiue, n.k. ili ukubaliane na mimi kwamba sheria ya Mungu iko katika kila moyo wa mwanadamu angalia wezi wanavyoiba, hawaibi hadharani wanaiba kwa kujificha, hata wazinzi huzini kwa kujificha hawazini hadharani, hata waongo humngoja kwanza aondoke mtu yule ambaye wanataka kumsemea uongo ndipo waseme uongo wao. mambo haya ni dhahiri kabisa kwamba wanafahamu kwamba wayafanyao ni kinyume cha sheria, wala hakuna aliyewafunduisha kwamba ukitaka kuzini nenda kajifiche ila ni mioyo yao wenyewe, kama mioyo yao inajua kuiba ni makosa basi iko sheria katika moyo inayouongoza moyo kutenda sawasawa na mapenzi ya Mungu lakini kwa tamaa tu ya mwili na vishawishi vya shetani mtu huyatenda hayo. moyo wa mtu unajua kwamba kuiba ni dhambi, kuna jamii moja huko America ya kusini wao walikuwa wanajua kwamba kuiba ni sifa,  wezi walikuwa ndio watu wenye sifa na majina makubwa na wenye kuheshimika katika jamii ile. watu walikuwa wanaiba kiasi kwamba ukimkaribisha nyumbani kwako pale sebuleni akiona kitu kizuri atakiokota kwa miguu na kuondoka nacho kwa ujanja mwingi. sasa siku moja wakaona kitu kikitokea baharini, na kitu hiki kilionekana kikubwa sana walistaajabu, wakadhani kwamba miungu yao imekuja kuwatembelea, vitu vilivyoibiwa majumbani kwa watu vikaanza kurudi kimoja baada ya kingine. hapa tunajifunza kwamba watu hawa wanajua kabisa kwamba kuiba ni makosa. kwa hiyo seheria ya Mungu iko katika kila moyo wa mwanadamu kumuongoza katika kutenda yale yampendezezayo Mungu.

Imeandaliwa na Mwinjilisti: Moses Mayila

0715961270

mosesmayilatz@yahoo.com

http://www.newhopeworldwideministry.wordpress.com

 

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

3 Responses to SHERIA YA MUNGU IMEFUNGWA KATIKA KILA MOYO WA MWANADAMU

  1. Martin says:

    I love you Jesus!

    Like

  2. Hakika, YESU NI MUNGU DAIMA.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s