USHINDI KWA NJIA YA ROHO MTAKATIFU

Salamu katika jina la Bwana.

leo niko hapa kuzungumza mada mpya inayoitwa “ushindi kwa njia ya Roho mtakatifu” Biblia inasema Samson alikuwa akisafiri kwenda nchi ya wafiristi, alipokuwa njiani ghafla simba akamwungurumia, Roho wa Bwana akamjia Samason akamchana chana simba kama mtu amchanavyo mwanambuzi.Pia siku moja samson aliwapiga wafiristi wengi na kuwauwa kisha akakimbilia nchini kwake kujificha, wafiristi wakaja kuvamia nchi ya Samson na wafiristi walikuwa ni watu walioogopeka kivita ilibidi ndugu zake samson wamfunge samason kisha wamtoe kwa wafiristi, wakati wanataka kumfunga Samson aliwaambia niapieni kama hamtaniua, ndugu zake wakasema hakika hatutakuua ila tutakukaza sana kwa kamba kisha tutakukabidhi kwa wafiristi. Samson alikubli ndugu zake samson walimfunga wakamkaza kisha wakampeleka kwa wafiristi, nao wafiristi walipomwona samson hali yakuwa amefungwa walipiga kelele za kushangilia, ndipo Roho wa Bwana akamjia samso akazikata zile kamba kana kwamba zimepukutishwa na moto, akaokota taya la punda akapiga waume elfu.

Ndugu zangu kumbukeni kwamba maada yetu ni ushindi kwa njia ya Roho mtakatifu, Biblia inasema simba alimwungurumia samson Roho wa bwana akamjia akamchana chana kama mwanambuzi. tunajifunza nini? kumbe mtu ukiwa na roho mtakatifu hakuana kitu cha kukushinda kufanya,kwa mtazamo wa haraka haraka ni kwamba maisha ya Samso yalikuwa yamefika kiama siku hiyo, lakini Biblia inasema Roho wa Bwana akamjia akamchana yule simba kama mwana mbuzi.kumbe Roho Mtakatifu humpa mtu uwezo usiokuwa wa kawaida, ndio maana Paulo alisema “Maana siraha zetu zina nguvu katika Mungu hata kuangusha Ngome.

Yamkini matatizo yamekungurumia kama simba, unatazama namna ya kuyatatua unakosa, usikate tamaa uko msaada utokao kwa bwana utakaokuwezesha kuyachana chana matatizo hayo, yamkini ndugu zako wakekuwa tatizo kwako, wanakufunga kama walivyomfunga Samson, Roho wa Bwana na akujilie kamba hizo walizokufunga zikatike mara moja kwa jina la YESU.

yamkini wako watu wanaokungoja wakuangamize kama wafiristi walivyomngoja samson, nao wanapiga kelele za shangwe kwa sababu wameona kuwa mtego wao unakwenda kufanikiwa, basi Roho wa Bwana na akujilie uwapige adui zako wote kiroho katika Jina la Yesu.

Bwana akulinde uwe salama katika Jina lipitalo majina yote.

Ev.moses mayila

+255715961270

mosesmayila@yahoo.com

http://www.newhopeworldwideministry.wordpress.com

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

2 Responses to USHINDI KWA NJIA YA ROHO MTAKATIFU

 1. PASTOR EDWARD FEDHA says:

  GOD BLESS YOU NGUGU MOSES MAYILA, WAS SO BLESSED BY YOUR MASSAGE, NATUMAI TUTAFAHAMIANA ZAIDI,
  UKO WAPI TZ, MJI NA JIJI?
  PASTOR EDWARD
  facebook edward musih fedha

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s