JINSI YA KUFANIKIWA KATIKA MAOMBI

Salamu ndugu zangu katika jina la Yesu.

Leo niko hapa tena kukuletea mada nyingine, katika mada hii tutajifunza namna ya kufanikiwa katika maombi, watu wengi huwa wanaomba kwa muda mrefu sana lakini wanajikuta kwamba mambo yako pale pale au hata kuzidi kuwa mabaya kuliko hata hali ya mwanzo.  nataka leo tupate kujifunza, mambo haya hutokea kwa sababu watu hawajuwi namna ambayo Mungu hufanya kazi. Siku zote Mungu hufanya kazi na wanadamu kwa makubaliano kwa kitalaam yanaitwa ‘AGANO’ Mungu alifanya agano na Ibrahimu, hata Ibrahimu akamtoa mwana wake wa pekee Isaka kuwa Sadaka ya kuteketezwa, Mungu alifanya agano na wana wa Israel ambalo kwa sasa katika biblia linaitwa agano la kale, walikubaliana na Mungu kwamba wasimwabudu mungu mwingine isipokuwa Yeye pekee ili Mungu asiwaletee magonjwa ya wamisiri.

Pia katika Biblia kuna watu walifanya Agano na Mungu wakimtaka awafanyie jambo flani nao watamfanyi jambo flani. Yakobo alikuwa akisafiri akafika sehemu akalala akaota ndoto malaika wanashuka na kupanda, mahara pale yakobo akafanya Agano na Mungu akasema “Kama Bwana atanilinda katika safari yangu niende salama nirudi salama, nitamtolea sehemu ya kumi ya mali zangu” Mungu alimlinda Yakobo hata kaka Yake Esau aliyekuwa anatafuta kumuua alipomwona badala ya kumuua alimkumbatia kwa upendo.

Mtu mwingine ni mama yake nabii Samweli, mama huyu tunaambiwa kwamba alikuwa tasa kwa miaka mingi, hata baadhi ya watu walikuwa wakimdharau kwa sababu yeye ni tasa hazai. siku moja mama huyu akaamua kufanya agano na Bwana, akasema “Bwana nipe mtoto utakaponipa mtoto huyo hakika nitamtoa sadaka akae nyumbani mwako daima” Mungu akaiangalia ahadi ya mama huyu akakubali akampa Samweli.

Ndugu mpendwa, hapa tunajifunza kwamba kumbe Mungu husimamia makubaliano, Biblia inasema yeye ni mwaminifu, kwa sababuMungu ni mwaminifu inamaana kwamba hatavunja makubaliano. ikiwa unatatizo kama hili yamkini kwa muda mrefu umekuwa na mahitaji yako, hebu fanya kama Yakobo, mwambie Mungu akutendee hivi nawe utamfanyi hivi. ni watu wengi wamefanikiwa kupitia somo hili, wengine uchumi wao sasa hivi unakimbia kwa kiwango cha juu sana kwaajili ya somo hili. lakini ukiweka Agano na Mungu ukumbuke kutekeleza. maana utalaaniwa ikiwa utavunja agano la Bwana.

Ikiwa unatafuta kazi, fanya hivi kama mama yake Samwel lakini usiombe haba kama mama yake Samweli alivyoomba kwani aliomba mtoto na akapewa mtoto mmoja tu kama alivyoomba, bali wewe utakapofanya makubaliano na Bwana Omba mambo makubwa, kama ni kazi omba mshahara mkubwa, maana Mungu ni mwaminifu hatakupa jiwe hali ya kuwa umemwomba mkate. hii iliwahi kunitokea hata mimi nilimwomba Mungu nipate kazi ya mshahara wa sh. 60,000/= tu na kweli nilipata kazi ya mshahara wa sh.60,000/= tu sawa sawa na nilivyoomba ndipo nikajifunza kwamba hatupaswi kuomba kidogo.

Bwana akusaidie katika Jina Lipitalo Majina Yote (Yesu Kristo)

Ev.Moses Mayila

mosesmayila@yahoo.com

www.newhopeworldwideministry.wordpress.com

0715961270

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

3 Responses to JINSI YA KUFANIKIWA KATIKA MAOMBI

 1. Rev.Forcus Rutaba says:

  Bwana Yesu asifiwe sana! Mimi ninaitwa Rev. Forcus Rutaba, wa Dayosisi ya Kagera Tanzania. Nimeoa nina mke mmoja na tuna watoto watatu, mke wangu anaitwa Dafroza Forcus, mtoto wa kwanza anaitwa Godbless na wa pili Remus. My first comments it’s about thanks for you! The second one is to encourage you for persisting to serve the Lord through this way. And lastly, I would like to know how long period have you been serving the Lord through this way? Why am I asking this question, because your teachings it’s very important for those who are careering. My self I have got experience, so let me wish you a good responsibilities and the Lord be with you.

  Like

  • Shalom mtumishi,
   Asante sana Mtumishi kwa ujumbe wako. kwa kifupi ni kwamba nimeanza huduma ya kumtumikia Mungu mwaka 2000 nikiwa muimbaji wa kwaya. na baadaye nikawa mhubiri mwaka 2006, mwaka 2009 nilianzisha hii huduma kwa njia ya mtandao. Bwana akubariki sana.

   Ev.Moses Mayila

   Like

 2. yusuph lugelo says:

  thanks for your ministry it encourages me to have successfully prayer

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s