MATOKEO YA MAOMBI NA SADAKA

Nawasalimu tena katika jina la Yesu,

Leo niko tena mahara hapa kuzungumza mada iitwayo, ‘MATOKEO YA MAOMBI NA SADAKA.’ Biblia katika kitabu cha Matendo ya mitume inasema kulikwa na mtu jina lake cornelio, mtu huyu alikuwa anaomba sana kwa Mungu na kuwapa sadaka masikini, kutokana na kufanya hivyo, siku moja Malaika wa bwana alimtokea kornelio, baada ya malaika huyo kumtokea kornelio alimwambia hivi “SALA ZAKO NA SADAKA ZIMEKUWA UKUMBUSHO MBELE ZA MUNGU.”

Kwa mujibu wa maneno haya ambayo malaika alimwambia kornelio ni dhahiri kwamba Mungu huhitaji kuona kitu kutoka kwako ili kiwe ukumbusho mbele zake, na mara akionapo kitu hicho hukukumbuka wewe, hapa kuna mtu atanihoji “Moses unasema kitu gani, tangu lini Mungu akasahau?” ni kweli Mungu hasahau lakini huhitaji kitu kutoka kwako ili atende au asitende jambo. Kumbu Mungu alifanya agano na kizazi cha Nuhu katika kipindi kiitwacho kipindi cha wazazi, unajua Historia ya wanadamu imegawanyika katika sehemu tatu kwenye biblia, sasa Mungu alifanya agano na nuhu baada ya Gharika alifanya agano na Nuhu akamwapia akisema sitauangamiza tena ulimwengu kwa maji, akaweka upinde wa mvua akasema kila atakapouona ule upinde wa mvua atakumbuka kwamba alishaapa kwamba hatauangamiza tena ulimwengu kwa maji.

Kwa hiyo ule upinde unasimama kama ukumbusho ambao Mungu akiuona anakumbuka alishaapa kutoangamiza ulimwengu huu kwa maji, na kiapo hakivunjwi inamaan
+a kwamba Mungu hawezi kuuangamiza ulimwengu kwa maji hata kama ulimwengu utaasi kiasi kikubwa. Hivyo ndivyo na sadaka pamoja na maombi ya kornelio yalivyofanyika ukumbusho mbele ya Mungu.

sasa kutokana na haya, je Tunajifunza nini?
Tunajifunza kamba: kumbe Maombi na sadaka yanaweza kufanyika pia ukumbusho mbele ya Mungu, Mungu hutazama kitu hata kama alikuwa ameruhusu mabaya yakupate akiona kitu kinachomfanya akukumbuke ataghairi, angalia kwa mfalme Hezekia, Hezekia aliendewa na Isaya akaambiwa kwamba Mungu amesema tengeneza mambo ya nyumba yako maana utakufa hakika, Hezekia aliposikia haya akageuza uso wake kwenye ukuta akalia akasema “Kumbuka ee bwana nilivyoenenda kwa ukamilifu mbele zako” Mungu alighairi akamwongeza Hezekia miaka 15. hapa hakughairi kwa sababu hezekia alimlilia, bali alighairi kwa sababu aliona kitu kwa Hezekia ambacho kilimfanya amkumbuke hezekia na kitu hiki ni wema na utiifu wa hezekia mbele za Mungu. hapa tunapata nyongeza kwamba kumbe hata wema tu na utiifu pasipo sadaka Mungu anakukumbuka, lakini simaanishi kwamba usitoe sadaka, Sadaka utoe sawa sawa na maagizo ya bwana maana na sadaka nayo i katika sehemu ya utii. na sadaka sio lazima upeleke kanisani, unaweza kuwapa masikini, kwamfano mimi huwa nawakusanya watoto Yatima na omba omba kisha nawalisha nawapa na hela ya matumizi, nimemuona Mungu kwa kiasi cha juu sana, maisha yangu ni tofauti sana na zamani.

Hivyo kornelio alifanyika kumbukumbu kwa Mungu kwa sababu ya sala zake na sadaka, hivyo basi kunaumuhimu wa kutokoma kuomba maana maombi hufanyika kumbukumbu mbele za Mungu.itafika hatua Mungu atasema na wewe kama livyosema na Israel kwamba “Je, Mwanamke aweza kumsahau mtoto amnyonyeshaye wala asimwonee huruma mwana wa tumbo lake? naam hao wanaweza kukusahau lakini mimi sitakusahau wewe tazama nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu kuta zako ziko mbele zangu daima.

Bwana wabariki wote katika jina lipitalo majina yote (YESU KRISTO).

Imeandaliwa na:
Ev.Moses Mayila
moses mayila@yahoo.com
+255 715 961270
http://www.mosesok.wordpress.com

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

4 Responses to MATOKEO YA MAOMBI NA SADAKA

 1. Ombeni says:

  Mbabikiwe wapendwa.
  Katika somo lako mimi nimejifunza kitu kimoja nacho ni kuwasaidia watoto wa mitaani
  Tafalidhali siku ukipanga kukusanyika na watoto yatima na omba omba nami nitafurahi kujiunga nawe

  Amen

  Like

 2. mosespk says:

  Ubarikiwe pia kwa moyo wako wa kutaka kuwasaidia watoto yatima na masikini, asante sana kwa kuungana nami katika jukumu hili, mwezi huu nitakuatana na watot hawa tarehe 30 mwezi huu, ningependa kujua wewe uko wapi ili iwe rahisi kukutana, mimi niko dar es salaam, na pia ningependa kupata simu yako ili iwe rahisi kuwasiliana, asante sana ubarikiwe sana katika jina lipitalo majina yote.

  Ev.Moses Mayila
  mosesmayila@yahoo.com
  0715961270

  Like

 3. tumaini says:

  barikiwa mtumishi,unatuinua na wengine pia,

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s