JE, NI SAHIHI KWA WAIMBAJI KUKODI UKUMBI KISHA KUWATOZA WATU FEDHA NDIPO WAINGIE KUSIKILIZA MAHUBIRI KWA NJIA YA NYIMBO?

Salamu tena ndugu zangu katika jina la Bwana wetu yesu kristo!
Ni siku nyingine tena tumekutana hapa kuweza kuzungumza kuhusu ufalme wa Mungu tena. Hoja yangu ni juu ya waimbaji wetu. Zamani waimbaji wetu walikuwa wanaimba vizuri kabisa, na hata sasa wanaimba vizuri kabisa lakini kinachonitatiza mimi ni kitu kimoja, hii tabia ya kukodi ukumbi na kuwatoza watu pesa ndipo waweze kuingia kusikiliza mahubiri kwa njia ya nyimbo mimi sikubaliani nayo. Hii ni biashara ambayo watu kwa kutomwogopa Mungu wameamua kuianzisha katika Injili. Jamani maandiko yako wazi “mmepewa Bure toeni Bure”. Niliwahoji baadhi ya waimbaji wakadai kwamba wanarudisha gharama zile walizotumia katika kukodi ukumbi, lakini mimi nikaona ile sio sababu ya kuniridhisha hata kidogo, kwa sababu wanakodi ukumbi ili wapate kuwatoza watu fedha. Kama ni kweli wanahubiri kwa ajili ya Mungu kwa nini wasiende kuimba katika viwanja visivyokuwa vya kulipia kama viwanja vya mpira, au kwa hapa Dar es salaam viwanja vya Manzese, Bakhresa na Jangwani, kwa nini ukodi ukumbi?

Jamani hii imekuwa Biashara. Waimbaji Mwogopeni Mungu msije mkapata ujira wenu duniani kisha mkaukosa ule wa Mbinguni. Mimi huo ni mtazamo wangu, ikiwa wewe unamtazamo tofauti na huo au unataka kunishauri hata changamoto usisite kuandika na mimi niko tayari kukusikiliza.
Mbarikiwe wote.

Ev. Moses Mayila

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

One Response to JE, NI SAHIHI KWA WAIMBAJI KUKODI UKUMBI KISHA KUWATOZA WATU FEDHA NDIPO WAINGIE KUSIKILIZA MAHUBIRI KWA NJIA YA NYIMBO?

  1. JWM says:

    Nakubaliana na wewe kabisa mwinjilisti. Kwamba kuna gharama haihalalishi kutoza watu wengine pesa. Lakini tukiangalia kwa upande mwingine, waimbaji walio wengi wa injili wakifanyacho ni sanaa na biashara tu – japo wanaweka ionekane “kiibada” na “kimungu” (kutokana na maneno yaliyopo katika nyimbo zao). Uimbaji siku hizi si wa kiibada tena, bali wa kiuburudishaji (entertainment) zaidi.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s