JE, WATOTO WADOGO NAO WANADHAMBI?

Salam tena ndugu zangu katika jina la Bwana,

Leo niko hapa tena kuzungumza na kanisa la Mungu, kwanza namshukuru Mungu mwenye Enzi kwa kunifanya mtumishi kijana, nimeanza kuhubiri injili tangu nikiwa na miaka 12 hadi leo ninamiaka 24, ni takribani miaka 12 sasa katika utumishi.

Bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye mada yetu inayosema “JE! WATOTO WADOGO NAO WANA DHAMBI? Biblia katika kitabu cha kutoka inasema ‘mimi ni Mungu mwenye wivu nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao”. Kwa mujibu wa andiko hili unaweza kuona kana kwamba Mungu huwahesabia watoto dhambi ya baba zao. Lakini ikumbukwe kwamba Biblia inasema “Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe, wala mwana hatabeba mzigo wa babaye wala baba mzigo wa mwanaye” ikiwa kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe sasa huku kupatilizwa uovu wa baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne umetoka wapi?

Hapa nikuweke wazi tu kwamba “WATOTO WADOGO HAWANA DHAMBI” Biblia inasema Yesu akasema, ‘yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauigia kamwe’! pia akaongeza kusema “waacheni watoto wadogo waje kwangu maana ufalme wa mbinguni ni wao” anamaana gani kusema ufalme wa mbinguni ni wao? anamaanisha kwamba ufalme wa mbinguni ni wa watu wasiotenda dhambi, na kama yesu amesema ufalme wa mbinguni ni wao ina maana kwamba watoto hawana dhambi. na kama unabisha basi niambie watoto wadogo wanadhambi gani? ikumbukwe kwamba dhambi huhesabiwa kutokana na kujua kwamba lipi ni jema na lipi ni baya, kisha ukachagua kufanya baya, kumbuka pale edeni Adam na mkewe hali ya kuwa hawajajua mema na mabaya walikuwa wakitembea uchi, na kutembea uchi ni dhambi! lakini hawakuhesabiwa dhambi kwa sababu hawajuwi jema na baya. lakini baada ya kula katika mti wa ujuzi wa mema na mabaya wakatambua kwamba kumbe kutembea uchi ni dhambi wakaanza kujifunika majani ya miti, na kuanzia hapo adamu akaanza kuhesabiwa dhambi. Hivyo hivyo hata kwa watoto, mtoto hata kama atatembea barabarani uchi, au akivua nguo mbele za watu akabaki uchi hahesabiwi dhambi kwa sababu hajuwi jema na baya, lakini wewe ukitembea uchi utahesabiwa dhambi. Mungu aliposema “nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao” alimaanisha hivi: yeye huwahesabia Dhambi watoto wa kizazi kimchukiacho, kwa mfano: baba ni mchawi akazaa watoto akawarithisha uchawi nao wakaendela kuutenda kwa hiyo Mungu atawahesabia watoto dhambi ileile ya baba yao. ukiendelea na hiyo aya nzima inasema hivi: nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu, hapa ina maana kama baba alikuwa mchawi, mtoto akikataa kuungana na baba yake katika uchawi huo, hapatilizwi dhambi ya uchawi wa baba yake. Biblia inasema roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa, kwa hiyo hapa mtoto hata hesabiwa dhambi hata kama baba yake atamkabidhi kwa wachawi akiwa yungali mdogo hajuwi jema na baya, maadam ameshakuwa mtu mzima na akachagua kumfuata Mungu habebeshwi mzigo wa dhambi ya uchawi wa baba yake.

Lakini hapa najua wanatheologia mtaniuliza “ikiwa mtoto harithi dhambi ya baba yake, na adamu alihukumiwa kifo baada ya dhambi yake, Je! kwanini na sisi tunakufa hali ya kuwa hatukutenda dhambi ya Adam? jibu ni kwamba sisi tunakufa si kwa sababu ya hukumu ya adamu bali ni kwa sababu ya matokeo ya dhambi ya adamu. Mungu akinisaidia nitakufafanulia zaidi katika hili.

–Ev.Moses Mayila
mosesmayila@yahoo.com
http://www.newhopeworldwideministry.wordpress.com

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

3 Responses to JE, WATOTO WADOGO NAO WANADHAMBI?

  1. james says:

    hello moses how are you my dear brother in The Lord?

    Like

  2. cosmas mabonde says:

    soma rumi 8:12

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s