MAMLAKA YA KUFANIKIWA AU KUTOFANIKIWA KATIKA MAISHA YAKO CHINI YA YAKO

Bw. wetu YESU KRISTO apewe sifa ndugu zangu,
Leo niko tena katika eneo hili ili tupate kujifunza tena. kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu kwamba, “Mamlaka ya kufanikiwa au kutofanikiwa katika maisha yako chini yako mwenyewe”.
Biblia katika kitabu cha Nabii Yeremia inasema “Uzima na Mauti u-katika ulimi wako. kwa mujibu wa andiko hili tunajifunza kwamba kumbe ulimi wako unanguvu ya kuamua iwe hivi na ikawa, lakini mtu anaweza kuniuliza kwamba “Moses ulimi wawezaje kuamua jambo na likawa?” Biblia katika kitabu cha mwanzo sura ya 1:26-27 Inasema hivi: “Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, akatawale ndege na wanyama na viumbe vyote, Mungu akamfanya mtu mwanaume na mwanamke.” ukiichambua Aya hii utakuta kwamba katika aya hii kunamaana mbili za muhimu sana, maana ya kwanza ni kwamba Mungu aliposema na tumfanye mtu kwa Mfano wetu, alimaanisha kwamba mtu atakuwa mtawala maana Mungu ni mtawala na ndio maana alisema akatawale Ndege na wanyama na viumbe vyote, pia aliposema “kwa sura yetu” alimaanisha muonekano wa wanadamu utakuwa kama muonekano wa Mungu.

sasa tulejee katika uchambuzi wa mada yetu, Mungu aliumba vitu vyote kwa neno isipokuwa mwanadamu pekee ndiye alimuumba kwa mkono wake kutoka katika udongo. Mungu alikuwa anatamka maneno tu “Uwepo Mwanga” na mwanga ulitokea.

Sasa basi ikiwa anauwezo wa kutamka jambo bila kugusa na mkono wake na linatendeka, na sisi wanadamu tumetengenezwa kwa mfano wake inamaana kwamba sisi pia tunao uwezo wa kuumba kwa kutamka kama Baba yetu Mungu alivyo. na ndiyo maana Mungu akatuambia kwamba Uzima na mauti uko katika ulimi wako, inamaana kila utakalolitamka litatendeka! nakumbuka mimi nilipokuwa mdogo nasoma darasa la nne, mtu mmoja aliniambia kwamba ” muda si mrefu wewe utakuwa pastor, na kweli leo mimi ninasoma Theology ngazi ya degree ni lazima nitakuwa pastor hivi karibuni. kwa hiyo maneno ya mtu yule yaliumba, japo Mungu alinichagua tangu siku nyingi lakini neno la mtu yule naweza kusema aliongozwa na Roho mtakatifu, kwanza nilikuwasipendi kuwa pastor nilikuwa sipendi hata kidogo, lakini leo natamani nimalize masomo upesi ili niwe pastor.
Pia nakumbuka binti mmoja kule Tanga alikuwa anaondoka kwenda Dar es salaam kusoma, Baba yake alimwambia hivi: “Binti yangu unakwenda mjini, lakini mimi natarajia kuwa utaniletea mambo mawili tu, kama sio Mtoto basi UKIMWI, mzee huyu alitamka maneno haya yamkini bila kujua, lakini Biblia inasema kila Andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho, Biblia inasema Uzima na Mauti u-katika ulimi wako, Basi mzee huyu aliumba, maneno yake yalifanyika kiumbe katika ulimwengu wa roho na matokeo ya kiumbe hicho yakaja katika ulimwengu wa Mwili. Yule Binti alikuwa anabeba Mimba anatoa Hatimaye sasa hivi ameamua kuzaa mtoto ili ampelekee baba yake kama alivyomtamkia maneno yake, kwa sasa anamimba Kubwa tu karibu ajifungue. Yule mzee bilashaka atamlaumu sana binti yake kwamba ni binti asiyekuwa na adabu, ni malaya kachukua mimba kabla ya kuolewa. Lakini kwa kawaida anayetakiwa ulaumiwa ni yule babaye maana alimuumbia binti yake mimba na UKIMWI kwa njia ya Ulimi wake.
kwa hiyo hapa tunajifunza kwamba hutakiwi kumtamkia mwanao neno lolote baya maana hakika litamtokea, bali mtamkie kila lililoheri maana atakuwa heri.
bila shaka utakuwa umepata kitu kutokana na somo hili ni somo refu sana lakini najitahidi kulifupisha.

Asanteni Mbarikiwe.

Tenda hivyo ukaishi katika jina la Yesu.Amina

Ev.Moses Mayila
mosesmayila@yahoo.com
+255 715 961270
http://www.newhopeworldwideministry.wordpress.com

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

2 Responses to MAMLAKA YA KUFANIKIWA AU KUTOFANIKIWA KATIKA MAISHA YAKO CHINI YA YAKO

 1. Emmanuel says:

  Mtumishi nashukuru kwa somo zuri Mungu akubariki kwa kazi njema, ila katika somo hili nimepatwa na swali moja kama si mawili kwamba nikweli na nineno la Mungu kuwa Uzima na mauti u katika ulimi, na kwamba kama ulivyo eleza kila tutalolitamka litatendeka, je nikitamka kuwa mimi ni tajiri bila kuchukua hatua ya kujishughulisha ni kweli nitakuwa tajiri? Kwa ufafanuzi wako umesimamia uumbaji wa Mungu, Mungu alitamka ikawa. Hapa kukoje mtumishi!

  Like

  • mosespk says:

   Bwana wetu Yesu kristo apewe sifa mtu wa Mungu.

   Nashukuru kwa swali lako zuri, wewe ukitamka kuwa umekuwa tajiri halafu usichukue hatua ya kufanya kazi unatwanga maji ukitemea kupata unga!
   Biblia inasema “Mkono wake mwenye bidii huleta utajiri, bali wa mvivu huleta njaa katika nyumba yake” kwa hiyo biblia imetuweka wazi kabisa. hata Mtumishi wa Mungu Paulo alisema asiyefanya kazi asile! pia Biblia inasema mwenye busara hujikusanyia akiba ya chakula wakati wa hari.Kwa hiyo tunapotamka kwamba sisi ni washindi ni lazima tuingie vitani tupigane ili tupate kushinda, tukitamka kwamba sisi ni matajiri ni lazima tufanye kazi ndipo tupate huo utajiri, kumbuka kuwa utajiri hutokana na sadaka! angalia katika Malaki, biblia inasema “Leteni dhaka kamili kikawemo chakula nyumbani mwangu, mkanijaribu kwa namna hiyo muone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni niwabariki hata isiwepo nafasi ya kutosha kuhifadhi katika nyumba zenu” kama hatufanyi kazi hiyo sadaka iletayo utajiri tutaipata wapi? kwa hiyo ni lazima tusema jambo kwa imani tulithibishe kwa vitendo, Biblia inasema Imani pasipo matendo imekufa. kwa hiyo tukitamka sisi ni matajiri hali ya kuwa hatutaki kufanya kazi maneno yetu yamekufa. bila shaka umenielewa mtu wa Mungu.

   ubarikiwe

   Ev.Moses Mayila
   mosesmayila@yahoo.com
   http://www.mosespk.wordpress.com

   Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s