MAADUI WA MAISHA YA MWANADAMU

Habari zenu ndugu wasomaji wa habari hii njema ya ufalme wa Mungu. leo tena nimekuja ili kukufundisha mada hii, “ADUI WA MAISHA YA MWANADAMU.”

Watu wengi sana Dunia pote wanafahamu kwamba hakuna kitu amacho humzuia mwanadamu asimwelekee Mungu mbali na shetani peke yake. sasa naomba leo unisikilize kwa makini sana, Watu hawa hawakosei wako sahihi kabisa lakini vipo pia vizuizi vingine vyenye nguvu ambavyo hawavijui yamkini wanakomaa kutoka kimaisha katika maisha ya kiroho lakini wanajikuta kwamba wanashindwa. sikuzote siri ya kushinda katika vita ni kwamba, kwanza umjue adui yako alipo na ufahamu anatumia mbinu gani na siraha aina gani, ndipo utatafuta siraha yenye nguvu kuliko na kuweza kumpiga adui yako mahali alipo.
lakini tofauti na hapo hutashinda ng’o. kwa nini ninasema hivi? wako watu wengi ambao hufanya maombi kila siku ili waweze kuishinda dhambi lakini wanajikuta wako katika dhambi tena.huomba tena kwa kukemea sana “Shetani ushindwe kwa jina Yesu” lakini wanadumu siku mbili tu ya tatu wako kwenye dhambi tena, unajua ni nini hufanyika? ni kwamba hawamjui adui yao ni yupi. kwa kawaida adui wa maisha yako ya kiroho na hata kimwili pia ni hawa: (1) Shetani (2) Mwili (3) Dunia. lakini katika hawa maadui Adui mwenye nguvu kuliko wote ni mwili! kwa sababu mwili ndiye mshawishi wa zinaa, Tamaa, ulafi, n.k na dhambi inayoongoza duniani hivi sasa ni zinaa. hivyo watu wengi wanafahamu kwamba haya huletwa na shetani, mwili wako ndiye adui mkubwa wa maisha yako. Biblia inasema “Maana nia ya Mwili ni Mauti” kwa hiyo kumbe mwili shida yake ni kukutupa wewe katika bonde la mauti hiyo ndiyo nia ya mwili. mwili ndio ulimsababisha mama yetu Eva kutenda dhambi pale Eden si shetani kama wengi wana vyojua, unajua ilikuwaje? ilikuwa hivi shetani aliingia kwa nyoka akaenda kumshawishi yule mama. biblia inasema kwa sababu ya kuyaona yale matunda kuwa ni mazuri na kutamani kujua mema na mabaya kwa yule mwanamke alichukua tunda akala. Biblia haijasema kwamba kwakushawishiwa na shetani kula matunda yule mwanamke alitwaa akala. unaona sasa hapa mwanamke huyu alitamani kujua mema na mabaya na aliyaona matunda yale yakamvutia. kwa hiyo tunajifunza kwamba kilicho mwangusha Eva hapa ni tamaa, na tamaa hutokana na mwili. balaa sasa linakuja kwa mumuwe mkewe baada ya kumpelekea matunda yale na alipoona kwamba mkewe tayari kisha kula akajua kabisa kwamba imempasa mkewe kufa, akasema lah! huyu ni nyama katika nyama yangu na mfupa katika mifupa yangu nitakufa naye, Adam naye akaamua kula kwa sababu mtu aliyetokana na mwili wake amekula. hapa sasa tunaona wazi kabisa kwamba kilichomsababisha adam aamue kufa ni kuona mwili wake ambaye ni mkewe akifa. hapa tunajifunza nini? tunajifunza kwamba Adamu pasipo mwili asingalifanya dhambi.

Japo nimefundisha kwa kifupi neno hili lakini naamini kila mmoja ameelewa wiki ijayo nitafundisha juu ya Shetani na Dunia.
Bwana akusaidie umshinde adui Mwili.

Naitwa Mwinjilist Moses Mayila
simu:0715961270
au 0755961270

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

2 Responses to MAADUI WA MAISHA YA MWANADAMU

 1. frederick marandu says:

  Praise GOD!Nisomo zuri fupi litatia moyo hata wavivu wa kusoma wengi nimegundua wakiona somo refu sana hawasomi hivyo tunawakosa!
  by frederick Marandu

  Like

 2. mosespk says:

  ni kweli ubarikiwe sana Fedrick mtu wa Mungu.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s