Mungu hungoja wakati kujibu maombi yako

Karibuni tena katika kituo chetu cha kujifunza neno la Mungu, jina langu ni Ev. Moses Mayila.

Kama Mada yetu isemavyo hapo juu, ‘MUNGU HUNGOJA WAKATI KUJIBU MAOMBI YAKO’ Biblia inasema katika Yohana 11:1……..Palikuwa na mtu mmoja jina lake Lazaro, mtu huyu aliugua sana ndugu zake wakatuma ujumbe kwa Yesu wakimwomba Yesu akamponye, lakini Yesu hakwenda kumponya. Lazaro akafa, na baada ya siku nne ndipo Yesu akaenda kwa Lazaro akakuta amekwisha kufa siku nne zilizopita. Martha dada yake Lazaro akamwambia Yesu “Bwana kama ulingelikuwepo asingalikufa” Kauli hii ya Matha inaonyesha wazi kabisa kwamba maombi ambayo alimwomba Yesu aende amponye nduguye kabla hajafa hayakujibiwa. lakini yesu akamwambia Amini Lazaro atafufuka, Yesu alikwenda Kaburini alikozikwa Lazaro akamfufua.
Ndugu zangu kunawakati unaweza kuwa umeomba kitu katika majira uliyayotumai kwamba Bwana atakujibu lakini ukajikuta kwamba yamepita bila kuona majibu ya maombi yako. unaweza kukata tamaa, lakini kumbe leo tunapata kujifunza kwamba Mungu hujibu kwa majira ambayo yeye anaona yanafaa kwaajili ya utukufu wake ili kwamba Atukuzwe Duniani. kwa sababu hiyo Yesu alisema ugonjwa huu wa Lazaro si wa kufisha ila ni kwa ajiri ya utukufu wa Mungu. yatupasa tuwe na imani ambayo aliambiwa Martha awe nayo ya kwamba Tuamini tu hata kama tunaona haiwezekani tena, ghafla mambo yatakuwa sawa. na siku zote ukiona umefika sehemu ambapo hakuna msaada kabisa basi Mungu yu-mahala pale kujionyesha katika utukufu wake. Wana wa Israel walipofika ukingoni mwa bahari hapakuwa Meli wala Boti ya kuwavusha wakigeuka nyuma wanayaona majeshi ya Farao yakiwafuata kwa kasi, walipoteza tumaini,hapo hapo Mungu akajitokeza katika utukufu wake ili atukuzwe, akayagawa sehemu mbili maji ya bahari wakavuka pakavu.
Nakumbuka siku moja niliwahi kukosa pesa hata ya kununulia chakula, nikawa nimelala usiku njaa ikawa kali nguvu zikaondoka, nikakumbuka kwamba kulikuwa na mfuko wa pipi ambazo nilitakiwa kuwapa watoto Nikiwa katika Huduma. nikamwambia Mungu, Daudi alikuwa na njaa akala mikate ya hekaluni kinyume cha sheria, na mimi nachukua pipi hizi kama Daudi. nikataka nichukue pipi niziponde kisha nichukue maji nitengeneze kama juice walau ninywe nipate nafuu. nikainuka kitandani nichukue maji kwenye ndoo, ghafla nikaona mfuko wa plastic kwenye ndoo nikautwaa nikaona ni mzito, nilipoangalia ndani nikakuta kuna chips na na chupa ya juice! kisha nikakumbuka kwamba kulikuwa na rafiki yangu alikuwepo pale ndani kwangu labda atakuwa alileta yeye. lakini nikagundua kwamba Mungu amemuokoa mtumishi wake na njaa. kwa hiyo nikajifunza kwamba kumbe ukiona sasa mambo hayawezekani tena muujiza uko karibu mahala hapo usijikwae shetani akachukua nafasi utakuwa na hasara kubwa kuja kuupata tena muujiza huo itakupasa gharama upya ya majaribu mapya.

Bwana akulinde mtu wa Mungu.

Ev.Moses mayila

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

One Response to Mungu hungoja wakati kujibu maombi yako

  1. tumaini says:

    mungu akubariki mtumishi kwa ujumbe,akupe ufunuo mpya kila siku kwa ajili ya kazi kufundisha neno lake kwa ufasaha

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s