GWAJIMA: TANZANIA IKO CHINI YA SHETANI


Mwasisi na Mchungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima mchungaji Josephati Gwajima alinukuuiwa kanisani kwake akisema tanzania iko chini ya shetani. Gajima alisema mwalimu ndiye aliyeikabidhi tanzania chini ya Shetani baada ya kukubali kuruka shimo huko bagamoyo ili kumtoa mkoloni. aliendelea kusema na ndio maana hatuendelei tuna vyanzo vya uchumi vingi lakini maendeleo hakuna. alitolea mfano marekani akasema Marekani wakati inaanzishwa watu walimwomba mungu na ndiyo maana hata fedha yao imeandikwa tunamwamini Mungu. lakini fehd ya Tanzania mara picha ya nyoka.

Mchungaji alisema Tanzania iko chini ya laana, na ndiyo maana matatizo hayaiishi. lakini alimaliza kwa kumlaani Mwanaanga mashuhuri Afrika mashariki Shekh Yahya Hussen kufuatia kutabiri kwake kwamba mgombea urais mmoja katika uchaguzi ulipita lazima atakufa na uchaguzi utaahirishwa. Gwajima alisema, Nataka kumuua Kikwete au Dr.Slaa? Hafi mtu hapa! na afe mwenyewe Shekh Yahya. Kama ijulikanavyo kwamba kinywa cha mpakwa mafuta kikitamka jambo ni lazima litimie Shekhe Yahya alifariki kabla hata ya kupita mwaka tangu gwajima atamke hivyo.

Watumishi kama hwa ni mfano wa kuigwa, watumishi walio tayari kukemea dhambi bila kujali serikali ni watu wanatakiwa kuenziwa sana hata baada ya kuondoka kwao Duniani, Kwa kweli Gwajima namfananisha na Yeremia kwenye Biblia Yeremia alikuwa ni shupavu mwenye ujasiri mwingi kukemea mabaya. Bwana amlinde mtumishi wake.

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

16 Responses to GWAJIMA: TANZANIA IKO CHINI YA SHETANI

 1. gershom Mwakila says:

  unajua watu wanaogopa kusema ukweli kwa sababu wanamwamini Mungu nusu nusu, unajua hakuna hekima mbele ya dhambi, dhambi inatakiwa kukemewa pasipo kuangalia sura, mtumishi halisi wa Mungu ni yule anayekemea uovu bila kuangalia aliyekosea ni nani, kwa kawaida viongozi wa nchi hasa Tanzania wanatakiwa kumuuliza Mchungaji Gwajima nini wafanye ili taifa liweze kusonga mbele. Mimi namwomba Mungu azidi kumjalia mchungaji Gwajima nguvu ili ainyoshe Tanzania ambayo inaamini ushirikina badala ya kumwamini Mungu, lakini kabla ya yote ni lazima Tanzania yote ije kwa Kristo. Amen

  Like

  • Peter says:

   Ndugu wapendwa katika Bwana,
   Napenda kuwajurisha kuwa usiku wa juma mosi kaka yetu marehem GREGORY PROTACE alimtokea mdogo wake DEOGRATIAS PROTACE na Kumuuliza kwanini walimuua? Huyu DEOGRATIS ndiye mwenye mke anayesadikiwa kumuua kaka yetu GREGORY.Tafadhari sana ninawaomba mzidi kuomba ili kumkomboa kaka yetu mpendwa.Ahadi yangu baada ya kumkomboa kaka kutoka mikononi mwa shetani ni kuokoka mimi na familia yangu yote na familia ya kaka yetu. Ninawaomba mnisaidie.

   Ishengoma.

   —–Original Message—–
   From: Ishengoma, Peter [ICG-GTS NE]
   Sent: Friday, March 02, 2012 3:35 PM
   To: ‘prayer@ufufuonauzimaministries.org’
   Subject: THE DEATH OF MY ELDER BROTHER GREGORY PROTACE

   Dear Ufufuo na Uzima Ministries (GCTC) or (Majeshi ya Ufufuo)

   It is with much feeling that I received a bad news of my sad loss, My Elder brother GREGORY PROTACE NIWAGIRA he has passed away on Friday January 13,2011 at Rubya Hospital Muleba Kagera Region after short sickness .

   The burial of our beloved elder brother was taken place on Sunday January 15, 2012. at Buyera village.
   It is truly an irreparable loss. I feel the blank so much. I can yet hardly believe it is true. I have indeed been comforted by the knowledge that all was done for the best by the Divine wisdom . I know that God will relief my pain for is the Merciful One.
   Kindly assist to return him alive so that he may live a victorious life. Glory be to God. I desire to see the Holy Spirit’s miracle-working power.

   Thanks and Best Regards

   Ishengoma.

   Regards
   Peter Ishengoma.
   Cell. 0717 658610 / 0788 658610 / 0757 315899

   —–Original Message—–
   From: Ishengoma, Peter [ICG-GTS NE]
   Sent: Monday, February 27, 2012 3:04 PM
   To: ‘info@ufufuonauzimaministries.org’
   Subject: KIFO CHA KAKA YANGU GREGORY PROTACE

   Mchungaji Joseph Gwajima,

   Ninakuomba sana utumie uwezo na karama ulizopewa na mwenyezi Mungu umurudishe kaka yangu GREGORY PROTACE aliyefariki
   Tarehe 13/01/2012 katika Hospital ya Rubya Muleba Kagera na kuzikwa kataka kitongoji cha Buyera mnamo tarehe 15/01/2012.
   Kifo chake ni cha utata mtupu hadi kusababisha nyumba tatu za watu wanaosadikiwa kuwa wachawi kuchomwa moto na mmoja wapo
   Kufariki.

   Ninakuomba sana utusaidie.

   Peter.

   Like

 2. Mtumishi says:

  KATIKA HILI SIMWELEWI GWAJIMA HATA KIDOGO. NAHISI KAMA KASEMA UONGO. NAONA KAMA ANADANGANYA. HUENDA IKAWA KUNA UKWELI HAPO MWANZO, LAKINI LEO WATU WANAIOMBEA TANZANIA. KUKIRI TZ IKO CHINI YA SHETANI, KWA HIYO YY YUKO CHINI YA SHETANI? (KAMA TZ IKO CHINI YA SHETANI KAJITOA AU?)

  HATA SISI TULIZALIWA NA WAZAZI WENGINE WACHAWI, LAKINI TULISHAKOMBOLEWA BAADA YA KUOKOKA…………
  INA MAANA YY HAJAKOMBOLEWA?

  KINACHOISUMBUA TZ NI DHAMBI (yaani kuna idadi kubwa ya watu hawajaokoka)
  NA WALA SIO KUWEKWA CHINI YA SHETANI (japo dhambi ni ya shetani)

  ANASEMA KUHUSU DOLA YA MAREKANI INA MTAJA…. HE HE HHEHEHEEE. MWAMBIENI AENDE AKAISOME VIZURI DOLA YA MAREKANI (nahisi haijui vizuri)
  IMEJAA ALAMA ZA MASHETANI KIBAO. (MWAMBIENI AKAISOME KWA MAKINI DOLA MOJA)
  IMEJAA ALAMA ZA FREEMASONS KIBAO. ANATUPA PICHA GANI ANAPOTETEA ALAMA ZA SHETANI?

  MIMI NAKATAA KWA JINA LA YESU TZ HAIKO CHINI YA SHETANI.

  Like

 3. David says:

  kimsingi Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya kutotengamana na dini yeyote,viongozi wa serikali(wanasiasa) ndio wanaongoza nchi, ni mara ngapi umepata kushuhudia viongozi hawa wanamtanguliza mungu wanapowania nafasi zao? ninachojua mm huwa wanakwenda kwa waganga wao.kama watoa maamuzi na viongozi wa serikali wanawaganga wao, mungu ana nafasi gani apo? mola hapendi dhihaka kiasi hicho, mara ngapi umeckia habari za ufisadi Tanzania. wewe unayejitambulisha kama mtumishi hapo juu, hata yesu ktk wanafunzi wake 12 alikuwapo yuda msaliti,inawezekana unatumiwa pasipo kujielewa. seneor pastor Ngwajima anapingwa na viongozi wa makanisa, misikiti na serikali, na tunaendelea kumwombea mchungaji aendelea kuishoosha Tanzania mpaka kieleweke,tunajua upinzani ni mkubwa lakini kazi ya makanisa sio kuwaombea wafuasi tu kumiliki magari na nyumba lakini pia kunyoosha pale palipopinda.

  Like

 4. ARNOLD PETER says:

  Baba mm huwa nabarikiwa sana na mafundisho yako,kwa kweli yamenitoa sehemu ambayo ilikuwa n mbaya sana. Na kwa ss MUNGU ashukuriwe kwa kuwa huku niliko MUNGU namwona akitenda, nami akinitumia mpaka nashangaa,Songa mbele baba yangu na MUNGU aendelee kukupa ufunuo ili na sisi tuendelee kukua kisawasawa.

  Like

 5. nelsonkitutu says:

  ni kweli kabisa tz bila kutawaliwa na (Nguvu ya damu ya Mwanakondoo) hatuwezi kuona wema wa Mungu katika nchi ya walio hai!

  Like

 6. Mungu aliye mtakatifu awalinde watumishi wake wateule amen

  Like

 7. ANNALISA says:

  NAMUOMBA MUNGU KILA IITWPO LEO AZIDI KUKUPA UFAHAMU NA KUKUONGEZEA NGUVU MAANA MUNGU NDIYE MSAADA WETU KWA KILA JAMBO.LAKINI AMEWAWEKA WASAIDIZI WAKE HAPA DUNIANI ILI WATUFUNDISHE NA KUYAJUYA MAANDIKO NA TUPATE KUISHI KATIKA SHERIA ZA KIMUNGU NA ZAKIROHO. NAKUPONGEZA BABA YANGU GWAJIMA NA MUNGU AKULINDE KILA IITWAPO LEO,……………LAKINI YULE AMLAANIYE MTUMISHI WA MUNGU AJUE SIKU ZAKE ZA KUFA ZIMEKARIBIA.

  Like

 8. Shetani anatesa watu sana, anawatia magonjwa kisha anayaondoa, ili watu wamwamini.Tujihadhari sana na miujiza ya shetani,anaouwezo wakushusha moto kutoka mbinguni,

  Like

 9. bishop Eddie says:

  Nashukuru Mungu kwa kunifundisha kwa kumpitia mch Gwajima

  Like

  • herman says:

   vizur wapendwa ambao kwa muda angalau mfupi mnajadili mambo ya imani,
   nashauri sana tujadili namna ya kujivua ktk dhambi, na kuokoka kwelikweli, kuliko kujibizana kuhusu mtu mwingne kwanh hata angehamisha milima haitusaidii kufika mbinguni,
   hapa tusijibalaguze kwa imani ya mtu nawe utafanikiwa, sahau hilo,
   njia zake sio zako,kila mtu atatoa hesabu yake!
   ndg “mtumishi” umeandika jumbe tar15march 2012, kumpinga gwajima kuhusu dola ya marekani umeelewa nini alifikiri?
   lakini umenena vyema kuwa “unakataa kwa jina la YESU”
   sisi twajua tuko chini ya aliyetuumba,
   nawe ndg “david” umeandika jumbe tar24novemba, ukimkanusha vikali ndg “mtumishi”
   sijaona kibaya alichoandika japo amekosea kidogo,
   narudia haitusaidii kitu kuijadili iman ya mtu,
   hongereni sana.

   Like

 10. nakushukuru mtumishi kwa maelezo yako mazuri juu ya nchi yetu. kwani inashangaza nchi yetu kuwa nyuma kwa kila kitu ingali tunazo rasilimali nyingi zisizopatikana katika nchi yoyote ulimwenguni.

  Like

 11. erastus says:

  Tanzanians,,,,you are blessed and you cannot know,, are you blind that you cannot see????
  God raising his servant ( Baba ngwajima) for you and then you criticize him,,.??!.

  Like

 12. Aloyce Simon says:

  Bwana asifeweeeeeeeeeeeeeeee!!
  “jamani mungu ndiye anayetuongoza katika njia iliyo sahihi.. hakika bwana wa majeshi anena kipitia kinywa cha mtumishi wake Gwijima, kamwe nguvu za giza haziwezi kulishinda jeshi la bwana!. ”
  asntanteeeeni xsanaaa
  mungu atutie nguvu.

  Like

 13. Frajeth Phocus says:

  ilo ni jambo la ushujaa mungu akutie mafuta zaidi maana tunajifunza mengi wanadam hata walete vizuizi vya kila aina mungu ataendelea kujitukuza kupitia alowachagua yeye

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s