ANASTAZIA MUKABWA TABIA ZAKE NI KAMA NYIMBO ZAKE

Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Kenya Annastazia Mukabwa imejulikana kuwa maisha yake ni sawa na nyimbo zake, Anastazia amekuwa miongoni mwa waimbaji wakemeaji wa maasi katika kizazi hiki. Moja ya nyimbo inayofananishwa na maisha yake ni ile iitwayo KIATU KIVUE. Mtumishi huyu amefuatiliwa na mwandishi wa mtandao huu maisha yake, tabia na mwenendo wake awapo mtaani na kujulikana kuwa mtu wa mungu huyu anatabia isiyokuwa ya kujikweza, ni mtu mwenye kujishusha na kumnyenyekea kila mtu. Na hii ilitokana na wahudumu wa Hotel moja ambayo alikuwa amepanga wakati akijiandaa kufanya tamasha, wahudumu hawa walimcheleweshea chakula na kusaabisha achelewe kwenye tamasha, lakini Anastazia hakuonyesha kuchukia wala kuwa na kinyongo moyoni mwake.

Bado aliwauliza kwa upole na kwa unyenyekevu mkubwa jambo ambalo si la kawaida kwa watu wengi. Watu wengi wakicheleweshwa kwenye shughuli zao na mtu yeyote huchukia na hata kutoa maneno machafu. Kufuatia kitendo hicho ambacho annastazia alionyesha kuwa yeye ni Mtumishi wa Mungu aliye mwingi wa Rehema. Akaonekana kuwa alishakivua kiatu cha Hasira.

Bwana amabariki mtumishi wake kwa jina lipitalo majina yote (YESU). Amen

(Na Mwandishi wetu.)

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

3 Responses to ANASTAZIA MUKABWA TABIA ZAKE NI KAMA NYIMBO ZAKE

 1. mosespk says:

  KUNGOJA NA KUVUMILIA

  Tungoje kama wakulima, mkulima huenda kuifukia mbegu yake na kuingoja iote ikue na mpaka itakapotoa matunda. Nilikuwa nasafiri na gari safari ilituchukua kwa siku mbili, nilikaa na dada na mmoja seat ya jirani alikuwa na mototo mdogo, na yule mtoto alikuwa akinisumbua ikafika hatua nikachoka kumbeba yule mototo nikata kumrudisha kwa mama yake, lakini nikasikia sauti ikiniambi kama wewe umeshindwa kitu kidogo tu hiki, je mimi Mungu nikuvumilia mara nagapi?

  Nakumbuka nilipokuwa nataka kurudi chuo kwenda kumalizia mwaka wangu wa nne lakini mpaka ikiwa imebaki siku moja kbla ya safari sijapata hata fedha kidogo kwa ajili ya mahitaji, niliamuka kuamuka a lfajiri, nikaomba nikamwambia Mungu kama imekupendeza kwamba niende nikasome halafu nisipate cheti changu, basi nitarudi huko nikafanye kazi mpaka nitakapopata hela ya kulipa.

  Nilipokuwa naondoka nataka kupanda basi nikapokea simu namba ambayo ni mpya nilipopokea dada mmoja akaniuliza wewe ndiye mchungaji Riziki akaniambia njoo ofisi ya makamu wa rais nikaambiwa huu ni mzigo wako nikapewa bahasha ambayo ilikuwa na kiasi cha mahitaji yote niliyoyahitaji.

  Kwa hiyo yakupasa kungoja katika safari yetu, nimejifunza kumngoja Mungu. Tusiwe kama baba yetu Adamu mungu alipokuja mahala pale ambapo alikuwa anamkuta akakuta Adamu hayupo ame jificha, kwa hiyo unaweza kujikuta kwamba umeukosa msaada wa Mungu mara Mungu akija na kukuta haupo katika uwepo wake.

  Mch. Riziki

  Like

 2. MISSANA A MISSANA says:

  MUNGU AZIDI KUBALIKI KAZI YAKE NA PIA NAPENDA KUJUA ANAWATOTO WANGAPI NA PIA DHEHEBU LAKE NA PIA NAMSHAURI AWAINUE NA WASANII WADOGO

  Like

 3. omar aula says:

  Natoa salamu kedekede na za zati kwako bi Annastazia. kakii, mekujua kwa jina hili toka darasa la 1 hadi 8 shule ya msingi, maweni. Tho am a muslim I love listening to your songs n feel blessed, am far from my loved country hom sweet hom n my pipo bt alwayz yua songs giv me strong companion. Blessed too classmate for the job well done.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s