APONA KICHAA BAADA YA KUOMBEWA

Kijana mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa Sengerema Mwanza, aliyeugua kichaa tangu akiwa mtoto amepokea uponyaji mara baada ya kuombewa na watumishi wa Mungu Ev.Moses Mayila na Ev.Frola Stefano, kijana huyu alieleza mara baada ya kufunguliwa kwamba alifanyiwa tambiko na babu yake ili kwamba awe mchaga halisi maana baba yake ni msukuma na babu yake alikuwa hataki mtoto yule awe Msukuma, hivyo aliamua kumchukua na kwenda naye moshi ili kumfanyia tambiko.

Kijana huyo alieleza kwamba mara baada ya kufika huko Moshi alitengezewa pombe ya kichaga wakamnywesha na nyingine wakamnyunyiza, lakini babu yake alidai kwamba bado hajawa mchaga halisi hadi wamfanyie kitu kingine tena, lakini cha ajabu mara baada tu ya tambiko hilo, kijana huyu alijikuta na hali ya tofauti kwani alianza kuona mambo yanakwenda kinyume, maana alianza kusikia hata mimea ikimsemesha, migomba ya wachaga akiisogelea ilikuwa ikimwambia “usiniguse wewe si damu yetu” ni jambo la ajabu kwamba kijana alikataliwa hata na mimea, basi tangu hapo akaanza kuwa kichaa na kadri siku zilivyozidi na yeye alizidi kuwa kichaa. Lakini inasemekana kwamba waliwahi kumpeleka kwa waganga wa kienyeji wakaambiwa kwamba mizimu ya wasukuma na wachaga inamgombania, ni jambo la kusikitisha kwamba mtu anagombaniwa na mashetani! Kijana huyu alichanganyikiwa na kuondoka nyumbani akatokomea kusikojulikana, amekuwa hivyo kwa miaka mingi ndipo mama mmoja alipomwona akaamua kwenda kuwaita watumishi wa Mungu Ev.Frola Stefano na Ev.Moses Mayila ili wamwombee.

Mama huyu alisema kwamba amejaribu sana kumpeleka kwa watumishi wa Mungu mbali mbali na kufanyiwa maombi lakini hajafunguliwa. Watumishi wa Mungu Ev.Moses na Frola walifika na kumwombea yule kijana wakamtoa mapepo, na mara kijana akawa mzima akaomba maji ya kuoga maana alikuwa hajaoga siku nyingi. Hadi leo hii kijana yuko katika hali ya kawaida wala huwezi kumjua kama ndiye aliyekuwa kichaa, kwani hata mtumshi wa Mungu Ev.Moses hakuweza kumtambua alipokutana naye jana nyumbani kwa Ev.Frola maana kijana amependeza anaongea vizuri hana tena hata chembe ya kichaa, huku uvumi ukienea kati ya watu waliokuwa wanamfahamu kwamba Ev.moses na Ev.Frola wametumia dawa kumponya maana haiwezekani kwa maombi tu mtu akapona kichaa.

Akizunguma na mwandishi wetu mtumishi wa Mungu Moses alisema “Hakuna lisilowezekana kwa Mungu, tatizo ni kwamba watu wanaamini sana kwamba Shetani ndiye mwenye uwezo mkubwa wa miujiza kuliko Mungu, wamesahau kama Miujiza ya Shetani haikuifikia miujiza ya Mungu huko Misiri zama za mfalme Farao, acheni kuteseka njoni kwa Bwana awapumzishe”

Hii si mara ya kwanza kwanza kwa mtumishi Moses kumwombea mwenye kichaa na kupona papo kwa papo, nakumbuka mwaka jana Moses alikuwa kwenye basi akotoka Dar es salaam kwenda Mwanza, ndani ya basi kulikuwa na binti mwenye kichaa ambaye alianza kupiga kelele akitukana matusi na kupiga watu, Moses alimkamata na kumkemea pepo, mara pepo wakamwacha akawa mzima, akaeleza kuwa kwao ni Shinyanga, Moses akamwambia aende zake akatafute Kanisa awe anakwenda kuabudu pale.

Hakika Mungu wetu ni mkuu sifa zake na zivume Duniani pote.Amina

A crazy has been healed after Ev.moses mayila prayed for him, he became crazy since many years ago, the reason which caused this person to become crazy is his grand father, he committed him to the traditions of Chaga tribe in Tanzania, after he committed him, a young who has been committed began from there to see the changes in his life, he saw even the trees were speaking to him, the banana trees said to him “Do not touch me you do not belong to our blood” so he was confused, then he was confused day after day. According to the days he became a crazy and he run away from home went to unknown place.

After several years an woman saw him she took him to her house then she went to call the servants of God, Ev.Moses and Ev.Frola they came to pray for him, they drove out demons and he was healed until today.

God is might, let his fame be spreaded around the world. Amen

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s