JIHADHARI NA MAFUNUO

Wiki ya Kwanza

MAFUNUO

Neno hili MAFUNUO linatokana na neno FUNUA. Hili neno FUNUA limetafsiriwa toka kwenye neno la kiingereza la ‘Reveal’. Neno ‘Reveal’ kwa kiswahili lina maana ya funua, fumbua, fichua, dhihirisha, eleza siri, onyesha au vumbua.

Kwa hiyo neno ‘Mafunuo’ lina maana ya;

1. Mambo yaliyofumbuliwa ambayo yalikuwa yamefumbwa;

2. Mambo yaliyofichukuliwa ambayo yalikuwa yamefichwa;

3. Siri iliyowekwa wazi;

4. Mambo yaliyodhihirishwa ambayo yalikuwa yamesitirika.

Wakristo wengi hasa waliookoka wanalitumia neno ‘Mafunuo’ bila kujua na kujali uzito wa maana yake. Utawasikia wanasema nimefunuliwa hili au lile. Lakini ukiangalia matokeo ya mafunuo hayo katika maisha yao yamewaletea madhara badala ya kuwaletea baraka.
Historia ya Mafunuo:

Mungu alipomuumba mtu kwa mfano wake, alitaka akae, aishi, afurahi na huyo mtu katika utukufu na utakatifu wake milele milele. Lakini mtu alipoasi maagizo ya Mungu, kulitokea mafarakano katika uhusiano huo. Mtu huyo akafukuzwa toka katika uwepo wa Mungu, na akaondolewa kabisa toka katika bustani ya Edeni. Mungu akawaweka Makerubi wailinde njia ya mti wa uzima. Soma kitabu cha mwanzo sura yote ya tatu.

Madhara ya uasi huo yalileta mauti kwa mwanadamu. Bwana Mungu alipomwambia Adamu ya kuwa hakika atakufa, hakuwa anamaanisha kifo cha kimwili, bali kifo cha kiroho ingawa kifo cha kimwili kilifuata baadaye. Maana yake ni kwamba Adamu na kizazi chake chote kitatengwa na uso wa Mungu. Uhusiano ule wa karibu uliokusudiwa na Mungu ukapotea. Kukaingia ukuta wa giza kati ya Mungu na mwanadamu. Imeandikwa hivi:

“Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa; wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zime uficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong’ona ubaya. Hapana adaiye kwa haki wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili; hunena uongo; hupata mimba ya madhara na kuzaa uovu.” (Isaya 59: 1 – 4)

Kwa maneno mengine Nabii Isaya anatuambia sababu za uso na sauti ya Mungu kutokuwa wazi kwa Mwanadamu. Kitabu cha 1Yohana 3:4, kinatuambia ya kuwa dhambi ilipokaribishwa katika jamii, ilimfanya Mungu kuwa FUMBO kwa mwanadamu. Mpaka hivi leo dhambi ikiendekezwa katika moyo wa mtu, mambo ya Mungu yanakuwa ni kitendawili kigumu kwa huyo mtu.

Tangu wakati dhambi iliporuhusiwa na mwanadamu imtawale, imekuwa haiwezekani kwa mwanadamu kumwona au kumsikia Mungu, bila ya Mungu mwenyewe kujifunua kwanza kwake kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Kwa kuwa Mungu amekuwa fumbo kwa mwanadamu, Fumbo hili linafumbuliwaje? Yanenaje Maandiko? Imeandikwa hivi;

“Lakini kama ilivyoandikwa, mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu), Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. Lakini Mungu AMETUFUNULIA sisi kwa Roho. Maana roho huchunguza YOTE, hata MAFUMBO YA MUNGU. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu” (1 Wakoritho 2: 9-12).

Watu wengine wanadhani wanaweza kumfahamu Mungu na mambo yake kwa uwezo wao wenyewe. Lakini Biblia inasema hivi “Mambo ya Mungu HAKUNA ayafahamuye ila Roho wa Mungu”. Kwa maneno mengine ina maana ya kuwa, ikiwa tunahitaji kuyafahamu mambo ya Mungu inatubidi tujifunze kushirikiana na Roho Mtakatifu.

Ndani ya mafunuo hayo ya Roho Mtakatifu, Mungu anatufundisha, anatukumbusha, anatuongoza, na mambo yajayo anatupasha habari yake. Yesu Kristo alisema; “Lakini huyo msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, ATAWAFUNDISHA YOTE, na KUWAKUMBUSHA YOTE niliyowaambia ….. ATAWAONGOZA awatie kwenye kweli YOTE; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na MAMBO YAJAYO ATAWAPASHA habari yake. Yeye atanitukuza mimi; kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari” (Yohana 14:26; Yohana 15:13,14)

Ukiendelea zaidi kuzisoma habari za Roho Mtakatifu, utazidi kuona ya kuwa bila msaada wake, mwanadamu hawezi kabisa kuyafahamu makusudi na siri ya Mungu. Nawasikitikia watu wale ambao wanadai kuwa wao ni wakristo, lakini hawampi Roho Mtakatifu nafasi anayostahili katika maisha yao. Mafanikio ya ukristo wetu yanategemea sana jinsi sisi tunavyoshirikiana na Roho Mtakatifu.

Roho zenye uwezo wa kufunua mambo:

Kuna roho za aina tatu zenye uwezo wa kufunua mambo mbali mbali ambayo yalikuwa yamefichwa. Roho hizi ni 1. Roho Mtakatifu; 2. roho ya Mwanadamu; 3. roho ya shetani.

Ni muhimu ufahamu ya kuwa wakati mwingine roho ya mwanadamu au roho ya shetani inafunua mambo na kudai ya kuwa mambo hayo yametoka kwa Mungu. Wakati mwingine mafunuo hayo yanasindikizwa na mistari mingi ya biblia, lakini ukiyachunguza kwa uwezo wa Mungu utafahamu kuwa mafunuo hayo si ya Mungu.

Maisha, ushuhuda, huduma za wakristo wengi zimeharibika kwa kutokuwa waangalifu mafunuo yanapotokea. Kuna wengine hata wamefikia hatua ya kuidharau biblia, na kusema kuwa wao wanaishi na wanakwenda kwa mafunuo wanayodai kuwa wanayapata moja kwa moja toka kwa Mungu. Mawazo ya namna hii ni ya uharibifu na ya upotovu kabisa. Mafunuo ya Mungu hayawezi kupingana na neno lake lililomo katika biblia.

Tukiziangalia na kuzichunguza hizi roho tatu zenye uwezo wa kufunua mambo, tunaona habari zifuatazo:

1. Roho Mtakatifu:
“ Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu” (1 Wakoritho 2:10,11)

Kama tunavyofahamu “ Mafumbo ya Mungu” maana yake ni “Siri za Mungu”. Pamoja na kufanya kazi zingine, Roho Mtakatifu ana wajibu wa kutufunulia siri za Mungu.

Nilipokuwa natafakari juu ya jambo hili, niliweza kuona ya kuwa katika agano jipya, Roho Mtakatifu ana wajibu wa kutufunulia siri zisizopungua saba toka kwa Mungu. Ndani ya siri hizi, kumefichwa utajiri mkuu na makusudi makuu ya Mungu juu yetu.

Wakati mwingine Mungu akipenda, nitaandika juu ya siri hizi saba kwa undani lakini katika somo hili nitazitaja tu na kuonyesha mahali zilipoandikwa. Siri hizi saba ni hizi zifuatazo:-

(a) Siri yake Kristo – Waefeso 3:4

(b) Siri ya Mapenzi ya Mungu – Waefeso 1:8

(c) Siri ya ndoa na uhusiano uliopo kati yake na uhusiano wa Kristo na Kanisa – Waefeso 5:32

(d) Siri ya injili iletayo Wokovu – Waefeso 6:19, Warumi 1:16; 17

(e) Siri ya Mungu yaani Kristo – Wakolosai 2: 1- 3

(f) Siri ya utauwa, au Utatu Mtakatifu – 1Timotheo 3:16

(g) Siri ya Kristo ndani yetu tumaini la Utukufu – Wakolosai 1:26 – 29

Hakuna mtu anayeweza kufahamu yaliomo ndani ya siri hizi bila kufunuliwa na Roho Mtakatifu. “Lakini sisi hatukupokea roho ya dunia, bali Roho (Mtakatifu) atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa (tuliyopewa bure) na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni” (1Wakoritho 12 – 14)

2. Roho ya Mwanadamu:

“Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake?” (1 Wakorintho 2:11a)

Tafsiri nyingine ya swali hili tunaweza kuulizwa hivi; ‘Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya moyoni mwako, kama siyo roho yako mwenyewe iliyo ndani yako?

Nadhani utakubaliana na mimi ya kuwa, unayo mambo fulani moyoni mwako ambayo hujamwambia mtu yeyote. Hayo mambo wakati mwingine yanaitwa siri ya moyo. Siku ukiamua kuitoa, basi inakuwa ni siri iliyowekwa wazi au siri iliyofunuliwa. Mambo hayo uliyoyaficha moyoni mwako, siku ukiyasema yanakuwa mafunuo kwa wengine.

Wakati fulani tulikuwa katika semina nzuri sana ya Neno la Mungu, na uwepo wa Mungu ulidhihirika wazi mbele ya watu wote waliohudhuria. Karama mbalimbali zilijitokeza kwa kadri ambavyo Roho Mtakatifu alivyoamua kuwatumia watu waliokuwepo.

Katikati ya baraka hizi kuliinuka mtu mmoja ambaye alisema hivi; “Wewe uliyechukua vitu vyangu urudishe.” Jinsi ambavyo maneno haya yalisemwa, ilionekana kana kwamba ni ujumbe kutoka kwa Mungu unaotolewa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Lakini ukiyachunguza maneno hayo kwa undani, mtu huyu hakuwa anatumiwa na Roho Mtakatifu, bali ni roho wa mtu huyo alikuwa akifunua mawazo yaliyokuwa ndani yake. Labda alifikiri kuwa akisema kwa njia ya kutoa ‘Ujumbe’ yule aliyechukua vitu vyake ataogopa!

Kuna jumbe nyingi zinazotolewa hasa katika vikundi vya uamsho na katika makusanyiko walipo watu waliojazwa Roho Mtakatikfu, ambazo si zote zinakuwa zimetolewa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Kuna unabii mwingine unakuwa umechanganywa na mawazo ya mtu anayetoa ujumbe. Lakini tumshukuru Mungu kwa kuwa kuna watu wanaotumiwa na Roho Mtakatikfu kutoa ujumbe bila ya kuongeza mawazo yao ya kibinadamu ndani yake.

Kuna ugonjwa mwingine ulioingia kwa wahubiri, hasa kati ya wale wasiopatana au walio na uchungu na wenzao. Utakuta akisimama kuhubiri badala ya kusema Neno la Mungu lilivyo, anaanza kulitumia neno hilo kuwasema watu asiopatana nao, na huku anadai kuwa ni mafunuo ya Mungu!

Je! Ni vizuri kuzitumia nafasi tulizopewa na Mungu kuhubiri Neno lake, kwa kusemana na kulaumiana! Je! Hayo ni mafunuo ya Mungu? Ni wazi ya kuwa hayo si mafunuo ya Mungu bali ni mawazo ya roho ya binadamu.

Bwana Mungu alisema na kuuliza kwa kutumia kinywa cha Nabii Yeremia maneno haya; “Maana ni nani aliyesimama katika baraza la Bwana, hata akalifahamu neno lake na kulisikia? Ni nani aliyelitia moyoni neno langu na kulisikia?

“Mimi sikuwatuma manabii hao, lakini walikwenda mbio; sikusema nao, lakini walitabiri. Lakini kama wangalisimama katika baraza yangu, ndipo wangaliwasikizisha watu wangu maneno yangu, na kuwageuza waziache njia zao mbaya, na uovu wa matendo yao. Mimi ni Mungu aliye karibu, asema Bwana, mimi si Mungu aliye mbali…..

“Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema Bwana. Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande? (Yeremia 23:18,21-23, 28, 29)

Kwa hiyo ni vizuri uwe mwangalifu, kwa kuwa si kila mtu anayesema ana mafunuo ya Mungu, amepewa ufunuo huo na Mungu kweli. Wengine wana ufunuo wa Mungu lakini wengine wanasema maneno yao na kudai ni mafunuo ya Mungu.

3. Roho ya shetani :

“Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali kijakazi kimoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika akageuka akamwambia yule pepo, nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.” (Matendo ya Mitume 16:16 – 18)

Jambo la kushangaza juu ya tukio hili ni kwamba huyo pepo wa uaguzi alijificha ndani ya mtu kwa kujifanya anasema kweli juu ya utumishi wa Paulo na wenzake!

Kuna mambo muhimu sana ya kujifunza katika habari hii ikiwa tunataka kufahamu jinsi ambavyo shetani anaweza kupenyeza mafunuo katikati ya wakristo na kuwadanganya wengi.

Hebu tuangalie na kujifunza kama ifuatavyo:-

(a) Shetani anapotaka kuleta machafuko katikati ya wakristo, – nyumbani mwao, katika makanisa na pia katika mikutano ya kiroho anatumia WATU au MTU. Imeandikwa hivi; “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi kimoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua.” (Matendo ya Mitume 16:16)

Tunaona hapa ya kuwa mtu huyu mwenye pepo wa uaguzi aliwafuata Paulo na wenzake mahali walipokuwa wakisali. Kwa lugha ya siku hizi tungesema aliwafuata kanisani, au kwenye mkutano wa kiroho, au kwenye semina ya kiroho, au kwenye somo la biblia, au kwenye kikundi cha maombi.

Huyu pepo wa uaguzi, kwa nini alimwongoza mtu huyu kwenda mahali ambapo watu wa Mungu walikuwa wanafanya sala? Lazima alikuwa na lengo maalum. Huyu mtu mwenye pepo wa uaguzi hakuenda mahali pa kusali kwa sababu alikuwa anataka kusali, bali kwa kuwa alikuwa ana lengo la kutaka kuchafua ibada au sala zilizokuwa zinafanyika pale.

(b) Shetani akiisha pata nafasi ya kumweka mtu wake katikati ya wakristo, atatafuta kila njia ya kuchafua masikilizano yao huku akijitahidi kusema maneno ya Mungu wakati huo huo, ili ASIJULIKANE!

Imeandikwa hivi, “(Mtu huyu mwenye pepo wa Uaguzi) Akamfuata Paulo na sisi akipiga KELELE, akisema, watu hawa ni watumishi , wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu” (Matendo ya Mitume 16:17)

(c) Kwa sababu alishuhudia mambo ya kweli juu ya Paulo na wenzake kuwa ni “watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu;” aliweza kukaa katikati ya watu wa Mungu kwa MUDA MREFU BILA KUGUNDULIKANA. Ndiyo maana imeandikwa; “Akafanya hayo siku nyingi.”

Watu wa Mungu nataka kuwaambia ya kuwa iweni macho! Huu si wakati wa kusinzia! Si kila mtu asemaye ni mkristo – ni mkristo kweli. Si kila mtu asemaye ‘Bwana Asifiwe’ – ameokoka kweli! Wengine wametumwa na shetani.

Kuna watu ambao shetani amewaweka kati yenu ili kuwachonganisha na kuwatenganisha. Je! hujaona hali ilivyo katika makanisa, au vikundi vya maombi, ambapo kila wakati wakiwepo watu fulani, kunakuwa hakuna maelewano na mapatano, na wakati mwingine ibada na mikutano kuvurugika? Watu hao wasipohudhuria, kunakuwa na amani, mapatano na ushirikiano. Ukiona hali ya namna hii ujue inawezekana ya kuwa tayari shetani amekwisha weka askari wake katikati yenu.

Yesu Kristo akijua hili alitoa mausia kwetu sisi tulio watu wake; alisema: “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali. Mtawatambua kwa matendo yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? … Si kila mtu aniambiaye Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengine wataniambia siku ile, Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.” (Mathayo 7:15,16, 21 – 23)

Hii inaonyesha wazi ya kuwa, si kila mtu atoaye mafunuo ya neno la Mungu – ametumwa na Mungu kweli. Tuwe waangalifu na watu tunaoshirikiana nao katika sala na ukristo wetu. Tusisikilize maneno yao tu na kuamini kuwa wao ni wenzetu katika Bwana; bali tuangalie na mienendo yao kama ina ushuhuda wa kikristo! Tukumbuke ya kuwa, “Imani pasipo matendo imekufa.” (Yakobo 2:26)

(d) Mtu huyu aliyekuwa na pepo wa uaguzi alifunua jambo ambalo Paulo na wenzake walikuwa wanafanya, na pia alifunua ya kuwa wao ni watumishi wa Mungu aliye juu.

Ingawa mafunuo hayo yalikuwa kweli, yalimkosesha amani Mtume Paulo. Imeandikwa hivi, “Lakini Paulo akasikitika (akasononeka au akakosa amani) akageuka akamwambia yule pepo, nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu akamtoka saa ile ile.” (Matendo ya Mitume 16:18)

Nataka uone jambo moja muhimu sana hapa. Biblia inasema; “ Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule PEPO ….”

Kwa nini Paulo akamwambia yule pepo na siyo yule mtu aliyekuwa na pepo? Kwa nini Paulo aliamua kumkemea yule pepo na hakumkemea yule mtu ambaye alikuwa na pepo? Inaonyesha wazi kuwa Paulo hakusikitika kwa sababu ya yule mtu kuwa pamoja nao; bali alisikitika kwa sababu ya yule pepo kuwa pamoja nao, akiwafuata na kuwapigia kelele!
Tunajifunza nini katika hili?

Tunajifunza ya kuwa; “Ingawa tunaenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili …. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu …………” (2Wakoritho 10;3, Waefeso 6:12, 13a)

Unapoona Roho wa Mungu anakushuhudia ya kuwa kuna pepo anayemtumia mtu katikati yenu, mkemee pepo huyo amtoke huyo mtu kwa jina la Yesu, na matatizo yaliyokuwa yanawasumbua yatatoweka. Kushindana na mtu juu ya machafuko fulani katikati yenu, na kumbe ni shetani amejificha ndani yake, ni kukosa maarifa ya kiroho. Na hii haitatui tatizo, bali inachochea ugomvi na mafarakano.

Ugomvi unaoletwa na shetani katikati ya watu wa Mungu hautatuliwi na vikao vya usuluhishi wala mahakama, bali kwa kutumia mamlaka ya Jina la Yesu Kristo na kumkemea shetani aliye chanzo cha ugomvi pamoja na hekima ya Roho Mtakatifu.

Usikose kusoma somo la wiki ijayo ya pili tutakapojifunza juu ya:
“MAMBO MATANO MUHIMU UNAHITAJI KUJUA JUU YA MAFUNUO”

MWL.CHRISTOPHER MWAKASEGE
http://www.mwakasege.org

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in MWL. CHRISTOPHER MWAKASEGE. Bookmark the permalink.

16 Responses to JIHADHARI NA MAFUNUO

 1. Howler! Just marvellous! Your publishing style is delightful and the way you dealt the topic with grace is exemplary. I am intrigued, I take for granted you are an master on this subject. I am signing up for your updates from now on.

  Like

 2. It appeared his close associates were some questionable people spouting some pretty radical stuff.Obama came from nowhere, we still dont know that much about him. The real racists are the people who voted for him for no other reason than he was black.

  Like

 3. The weakness of the Steelers defense is their secondary. By putting pressure on Palmer they usually make him get rid of the ball quickly so their DBs dont have to stick with Cincys WRs for too long.

  Like

 4. This was an amazing program and left me depresses. Seems the US keeps on coming up with plan after plan to defraud the investor and keep the money rolling into US financiers and there is no way for an honest investment to pay off, Even if one cashes it all in and keeps it under the mattress, there will be a way to devalue the currency to make one lose ones savings.This show is worth sharing. Is there any way to get a copy of the show on a DVD? Please advise

  Like

 5. An impressive share, I simply with all this onto a colleague who had previously been doing little analysis during this. Anf the husband in fact bought me breakfast due to the fact I discovered it for him.. smile. So ok, i’ll reword that: Thnx to the treat! But yeah Thnkx for spending any time go over this, I believe strongly about this and enjoy reading more about this topic. Whenever possible, as you grow expertise, would you mind updating your blog site with a lot more details? It’s highly helpful for me. Massive thumb up due to this article!

  Like

 6. I simply could not leave your website prior to suggesting that I extremely enjoyed the standard info an individual supply to your visitors? Is gonna be again continuously in order to inspect new posts

  Like

 7. Hey there, You’ve done an incredible job. I’ll definitely digg it and personally suggest to my friends. I’m confident they will be benefited from this website.

  Like

 8. MUNGU ASIPOKUJIBU MAOMBI YAKO MUULIZE NI KWA NINI HAJAKUJIBU – By Mwl. Christopher Mwakasege

  Habakuki 1: 1 – 4
  ■Kuna maombi aliyokuwa anomba lakini Mungu akanyamaza
  ■Ukiwa kwenye mazingira hayo usije ukachoka/ ukakata tamaa usije ukanyamaza, muulize Mungu kwanini umekataa, ili akujibu kwa nini hajakupa maana hata akikuambia kwanini hajakujibu itakuma amani. Maana Mungu atabaki kuwa Mungu hata kama hajakujibu!
  ■Sababu mojawapo (zipo nyingi) ya watu kutojibiwa ni kwa sababu watu wanataka wajibiwe maombi yao nje ya NJOZI/ MAONO ya Mungu. Ukiomba nje ya njozi usitegemee kujibiwa! Kuna vitu Mungu amempa mwanadamu na ameviweka ndani ya njozi; na ukiviomba nje ya hiyo njozi fahamu kuwa atanyamaza!
  ■Habakuki 2:1 – 4 Kutokujibiwa kunazaa kulalamika; wengi wanasukumwa kulalamika, hata kama ulikuwa hauombi kwa mungu; kama unaomba kwa bosi wako kwa siku nyingi na amekataaa utaanza kulalamika!
  ■Katika kulalamika (Habakuni 2: 2 – 4) Mungu akajibu kulalamika kwake
  ■Mungu alikuwa anazungumza na Habakuki kuwa abadili namna anavyoomba, kutoka kuomba kwa kulenga mtatizo yanayokuzunguka kwa kuomba ni ya badilishe niyabadilishe yaweje, na kwenda katika maono/ njozi! Majibu ya mambo yote yapo ndani ya njozi.

  NJOZI/ VISION

  Njozi ni kusudi la Mungu linalofunuliwa ndani yako kwa mfumo wa kipicha. Unaona picha ndani yako

  a). Na ile picha inakupa sababu ya kuwepo kwako, kama ni njozi yako; inakupa kuwepo kwa kampuni kama ni njozi ya kampuni; inakupa kuwepo kwa nchi kama ni njozi ya nchi nk. Lazima ijibu swali la why! Jibu limo ndani ya njozi.

  b). Inakupa picha ya mwisho mwanzoni; ili ikupe msukumo wa kuanza, usipoona mwishoni utakata tama

  c). Ndani yake inakupa dhamira/ motive/ kusudio la kuwepo hiyo njozi; unafanya hicho kitendo kwa kusudi gani?

  WITO & MAONO (calling & vision)

  Wito na maono havifanani
  ■Wito kazi yake ni kukusaidia ufikie maono
  ■Wito usio na maono unayumba yumba
  ■Malengo sio maono; malengo ni hatua ya kufikia maono/ vituo vilivyowekwa kwenye safari yako ya unapoelekea ndio maana kuna malengo ya muda mfupi na malengo ya muda mrefu!
  ■Mtu mwingine anataka maono anauliza mpango; Mpango unafuata baada ya maono kutokea!

  MAMBO 7 AMBAYO YAPO / YANAPATIKANA NDANI YA MAONO; mambo ambayo Mungu alikuwa anazungumza na Habakuki. Kama hauna hivyo vitu saba usijaribu kuvitafuta nje,ila ndani ya maono!
  ■Mambo yapo/ sababu zipo nyingi sana na hizi ni chache tu (Moshi na Arusha sikuzigusa)
  ■Si kwamba kwa sababu Mungu hajakujibu basi huna maono!

  1. IANDIKE NJOZI

  Maana yake, njozi ipo;kama huna muulize Mungu akupe!
  ■Iandikeili usije ukaisahau
  ■Lipo kusudi la wewe kuwepo/ kusudi la kampuni kuwepo/ kusudi la nchi kuwepo/lipo kusudi la ndoa yako kuwepo; kama hufahamu muulize Mungu

  2. IWE WAZI SANA
  ■Uweze wewe mwenyewe kuielewe
  ■Mambo yanayopitia katika maisha yako uweze kuelewa; usipo ielewa njozi/ vision hautaelewa mambo yanayopitia kwenye maisha yako

  3. ILI AISOMAYE AWEZE KUISOMA KAMA MAJI

  Watu wengine wakikutazama katika maono yako waweze kukuelewa (kuelewa maono yako) na wakikuelewa watakukuunga mkono/ watakushauri; si kwamba watu wote wataelewa!
  ■Si kwamba watu wasipoelewa Mungu ataondoa maono yake; ukiogopa macho ya wanadamu yatakusumbua kweli kweli.
  ■Hao watu wachache wanaoelewa utaenda nao hao hao wachache watakutia moyo mpaka hapo baadae ambapo wengine watapewa kuelewa; wengine wao sio rahisi kutofautisha hindi na gugu.

  4. NI KWA WAKATI ULIAMRIWA

  V.3 … ni kwa wakati ulioamriwa …/ at the appointed time!
  ■Ni wakati appointment yako; ni wakati ambapo unakutanishwa; kama unatembea ndani ya yale maono; ndani ya yale maono kuna time – time ya appointment (kuna muda uliofungwa). Maono yanakupa maandalizi ya appointment, maandalizi ya mabadiliko, maandalizi ya misimu.
  ■Maono yanakupa maandalizi ya mabadiliko katika msimu; si mabadiliko yote ni mazuri
  ■Kuna mabadiliko yatakutoa gamba/ kukuumiza na maono yanakuandaa ili upite katika mabadiliko! Mabadiliko mengine yanaweza kuondoa nywele, mengine yanaweza kukufanya uwe mwembaba. Maono hayataruhusu uwe-taken by surprise. Maono yanakuandaa!
  ■Mungu anasema jambo kabla ya kutokea kwa sababu anataka UJIANDAE – Mungu anasema “Mtumishi wangu anapokufa tega sikio kwa sababu kuna instructions zinakuja”; hakuna siku mtumishi anaondoka na walinaobaki wasielezwe; mwangalie Musa na Joshua, haiwezekani Musa aondoke na Joshua asijue; mwangalie Eliya na Elisha,haiwezekani Eliya aondoke na Elisha asijue; haiwezekani Paulo aondoke na Timotheo asifahamu. – Wanaombeana wanakabidhishana kazi vizuri, ukiona hayo hayapo basi hayo mabadiliko hayapo kwenye maono! Lazima huyu anayechukua ajua mwenzake ameishia wapi!
  ■Mabadiliko yakitokea na watu wanaobaki wasielewe ujue watu hao wapo nje ya ndoto/ maono
  ■Maono yanakupa maandalizi – kwa muda uliamriwa
  ■Mabadiliko ya kiholela yapo nje ya maono!
  ■Kuna vitu vinakuja kwenye maishayako na kama hukuandaliwa vitakuyumbisha
  ■Maono yanakupa thamani ya muda; maono uliyopewa yatakupa matumizi ya muda (thamani ya muda), maono niliyopewa hayawezi kufanana na ya mtu mwingine i.e thamani ya muda zitatofautiana kati yangu mimi na mwingine.
  ■Mithali 19: 18 – pasipo maono watu huacha kujizuia/ wanaishi kiholela; hawajali muda kwa kuwa hawana maono
  ■Kwa wanafunzi; kabla haujaingia kwenye mgomo fikiri juu ya muda! Degree ya miaka 3 uipate kwa miaka 5 ati kwa sababu ulikuwa kwenye migomo! Masomo yapo timed; Aliye kwenye maono yupo timed; he / she is connected to time and cannot afford to lose time; kama unagoma wewe goma lakini hauwezi kuwa kiongozi wa kesho!
  ■Huwezi kuwa kiongozi bila kuwa na maono; huwezi kuwa na maono halafu upoteze muda!
  ■Siku ya kuzaliaw kwako inakuwa noted na siku ya kufa kwako inakuwa noted ili kwamba kama upo kwenye maono lazima tujue lini umeingia kwenye maono na lini umetoka ili tujue/ tupime uliondoka kabla halijaharibika!
  ■Maono ya Mungu yapo timed; maono ya Mungu hayapo hewani!
  ■Ukienda kukopa pesa, ukisema mimi nina maono wanakuuliza tupe time-frame; lini kiwanda kitajengwa, na lini kitamalizika na kuanza production? Kama wanadamu wanakuuliza hivyo ni vipi uende kwa Mungu na akupe nje ya NJOZI/ akupe bila kuwa na MAONO?
  ■Jizoeze kwenda mbele za Mungu akuambie akupe kuzijia siku zangu/ mwombe akupe thamani ya muda. Muulize mambo ya watoto wako na uwe na uhakika kuwa hatanyamaza.

  Maono yanakupa kuwianisha maono yaliyopo maeneo mbali mbali; Mungu anamaono makubwa ya kanisa la ulimwenguni mwote, kanisa la nchi, kanisa lako na maono yako binafsi. Muulize Mungu maono ya kanisa, naye ataambia! Maono ya kanisa ni makubwa kuliko maono ya mchungaji hivyo mchungaji ajifunze kuwianisha maono yake na maono ya kanisa na mchungaji asiyeuliza maono ya kanisa atakuwa na confusion – hayupo connected na watumishi wa kanisa la nchi kwa muda huo.
  ■Lazima uweze kuwianisha maono mbali mbali
  ■Lazima kuwe na connection kubwa ya kanisa la ulimwenguni mwote; lazima maono yako yaende sawa sawa na maono mengine ulimwenguni.

  (2Timotheo 4: 1 – 8) V. 6 … kwa maana mimi sasa NAMIMINWA, NA WAKATI WA KUFARIKI KWANGU KUMEFIKA… alijua anaondoka na hakutaka kuondoka bila kumueleza anaye muachia ofisi; katika maono makubwa ya kanisa la ulimwenguni, kila mtu anasehemu yake na mwisho wa kufanya sehemu yake; Paulo anamuambia Timotheo kuwa kuna maono yangu na nimeyamaliza maono yangu na muda wangu umefika na ninakuachia na nimevipiga vita vizuri i.e Timotheo kuna kazi mbele yako; ni lazima awianishe maono yake na maono ya kanisa dunia nzima!
  ■… mimi nimeifanya sehemu yangu na muda wangu umeisha! Na wewe uendeleze maono yale yale
  ■Au unafikiri utaishi milele? Mimi na mke wangu tunajilizaga “hivi tukifa itakuwaje?”
  ■Sulemani alisema nimefanya kazi vizuri laini sijui atakayekuja kama ataiendeleza – na huu ni ubatili; haina maana kuwa kazi ya Mungu italala; there is no success without a successor!
  ■Huwezi kusema umefanikiwa wakati huwezi kutafuta nani atakaye kupokea kijiti chako!
  ■Ukiona hufikiri kitu gani kitatokea, nisipokuwepo kwenye ofisi/ family/ huduma i.e nikifa – fahamu huna maono; na unataka ukifa ufe na maono!
  ■Simama kwenye nafasi yako, nataka ujue kuwa hata kama serikali ipo au haipo maono yako yatasonga mbele! Kamuulize Daniel kama angesubiri msaada wa Nebkadneza ndio sijui kama angefanikiwa.
  ■Ndani ya maono pana surviving plan ya Mungu ya kukusaidia; hata kama mambo ni magumu vipi ndani ya maono ipo surviving plan ya kupita mahali pagumu.
  ■Gideon aliyejificha kwa sababu mazingira aliyonayo hayakumruhusu maana Wamedian wangefahamu wangeichukua ile ngano. Malaika akamweleza Gedion maono ya Mungu juu yake kuwa Mungu anataka awe kiongozo na Mungu amtumie ili kuwatoa kwenye mikono ya Wamedian; Gedion akatoa visingizio/ malalamiko – sisini maskini; mimi ni mdogo katika family! Kama maono ya Gedion yangetegemea Wamedian ndio wamsaidie asingefanikiwa! Malaika akasema naye kwa mambo yasiokuweko kama vile yangalipo.
  ■Kuwa kiongozi inawezekana wengine wasikuelewe; kuwa kiongozi unachochea kuwa na maadui lakini chukua hatua kuwa wewe ni shujaa na uwatoe watu; huwezi kuwatoa watu mahali walipo kama hujaona mahali pengine palipo bora zaidi. Ili wale wanaotaka kwenda ng’ambo ya Jordan na wewe wavuke na wewe na wasiotaka wabaki.

  5. INAFANYA HARAKA ILI KUUFIKILIA MWISHO WAKE

  Njozi hiyo inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake

  Neno MWISHO WAKE lina maneno ya mawili

  I). Kituo cha wisho cha safari yako (Destiny)

  II). Alama unayoacha kwenye kituo cha mwisho kwa kuwepo kwako na Mungu wako (legacy)
  ■Kama ni maono ujue pana alama ya destiny na alama ya kumbukumbu – legacy ya Mungu; kama ni maono ya Mungu basi ujue Mungu anataka uache alama ili watu wakukumbuke; kama ni maono ya shetani utaacha alamaya destiny na alama ya legacy ya shetani;
  ■Yeremia 29: 11 mwisho wa mpango wa Mungu unakita kwenye vision/ maono; Mungu anajua mwisho wa maono ya Mungu, mwisho wa maono kuna mpango wa Mungu ili ufike mwisho. Ndio maana Mungu haruhusu mipango ya wanadamu kuingilia maono ya Mungu.
  ■Mungu hawezi kuruhusu mipango ya wanadamu ifike kwenye maono yake; je umejenga kwa nyasi au kwa miti au kwa dhahabu safi (neno la Mungu lisiloghushiwa) kila kazi ya mwanadamu itapimwa kwa moto, na kama umejenga kwa nyasi yatateketea na hautakuwa na hautavikwa taji, maana umefuata maono yako mwenyewe au maono ya dhehebu na sio maono ya Mungu.
  ■Mungu hawezi kukupa maono kama hana mpango wa kukufikisha kule! Watu wanapewa mpango halafu wanafikiri ni maono!
  ■Mungu akikupa mpango na ukijua amekupa usisite lakini chukua hatua, na kila hatua atakupitisha hata kama kuna upinzani wa namna gani; kama huna uhakika rudia maono ya Mungu na ondoa maotea, ondoa visivyo vya Mungu, usiweke maono ya kwako, then chukua hatua
  ■Inafanya haraka kuifikilia mwisho wake; maana yake ipo on-course na ipo kwenye mpango wa Mungu!
  ■Mpango wa Mungu ukiachiliwa moyoni mwako unabadili kufikiri kwako! Kama mtu anaondolewa lazima wengine waandaliwe!
  ■Kama hautembei ndani ya vision ya Mungu ng’ang’ana Mungu akupe maono ya kwako; kama huna maono ya kwako unaweza ukajikuta ukatumikia njozi ya mtu mwingine; lakini inawezekana kutumikia njozi ya mtu mwingine na nyozi yako isife, njozi yako inakua na njozi yake inakua; lakini inawezekana kuitumikia njozi ya mtu mwingine kunaweza kusababisha njozi yako kufa!

  Like

  • regina masalu says:

   Mimi Regina Masalu,mkarismatiki wa Dar es salaam,sasa nipo Brazil kwenye huduma mpaka may,nimebarikiwa sana,MUNGU AWABARIKI SANA WATUMISHI WA MUNGU,NIOMBEENI NITIMIZE KUSUDI LA MUNGU.

   Like

 9. Okuli Makere says:

  Nmefurahi sana kupata mafundisho ya mwalimu kupitia web yenu. Mungu wa baraka atawajazi na kuzidi

  Like

 10. MUNGU ninaye mwabudu awabariki watumishi wa MUNGU kwa kazi mnayo ifanya

  Like

 11. James A Mwambungu says:

  Nina shida sana ya kuonana na mtumishi Mwakasege lakini hata kwa namba yangu tu 0685 550101 atanipata,nimejaribu sna kweny mikutano yake nikashindwa kukutana nae.Mungu awabariki kwa huduma nzuri

  Like

 12. Davin mpanduji says:

  Amen!

  Like

 13. DAVID CAROLI Tembelea blog yangu kwa ajili ya kupata faida kubwa ya kujua Kweli ya Neno la Mungu.

  Like

 14. felister Elisamehe! says:

  Ninashukuru Mungu kwa ajili ya mafundisho haya.Mungu aliye hai awabarki na awatunze na awtie nguvu ya kusonga mbele watumishi wa Mungu!mafundisho haya yamekuja kwa wakati muafaka japo nilijua nimechelewa!!!! Mungu awabariki naomba maombi yenu ili niweze “KUDAKA”

  Like

 15. Benedict Mashimba Bahati says:

  nakuomba mchungaji uandike kitabu, pia nakuomba utuchambulie kuhusu freemason hawa ni akinanani

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s