JINSI HOFU INAVYOWEZA KUKUWEKA KATIKA HATIA!

Na DAVID MGOGONGOLWA:

HOFU :- Ni kuogopa mambo yaliyopita, yaliyopo au yajayo. Kibiblia : hofu ni kukosa imani! “ mwenye haki wangu ataishi kwa IMANI naye akisitasita roho yangu haina furaha naye” (waebrania 10:38) neno “kusitasita AMPLIFIED BIBLE inasema “draws back or shrinks in fear” unaona sasa Hivyo imani ni kinyume cha hofu! Kibiblia.
AINA TATU ZA HOFU
1) Kuogopa mambo yaliyopita!
Watu wengi wapo kwenye hofu leo kutokana na mambo waliyopitia zamani,
Mfano : Dhambi walizotenda zamani , uongo waliofanya zamani n.k. nao wanaishi katika hofu kwa kuwaza, je kweli Mungu atawasamehe , watu watawachukuliaje?, watarudi kwenye hali ya mwanzoni? Lakini biblia inasema “hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya” (2Kor 5:17).

2) Kuogopa mambo yaliyopo!
Kutokana na hali ngumu ya maisha watu wengi wamejikuta kuishi kwenye hofu ya mambo yaliyopo hii inatokana na watu wengi , kuangalia hali wanayopitia bila kushirikisha uweza wa Mungu na hii inasababishwa na mtu kukosa muda wa kumtafakari Mungu na neno lake. biblia inasema “kitabu hiki cha torati kisitoke kinywani mwako bali yatafakari maneno yake mchana na usiku ,ukapate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote, yaliyo andikwa humo maana ndipo utakapo ifanikisha njia yako , kisha ndipo utakapo stawi sana” (Yoshua 1:8)

3) Kuogopa mambo yajayo!
Kutokana na kutojua ya kesho watu wengi wameingia kwenye hofu ya mambo yajayo, ila Yesu alitunya mwanzo kuwa “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake na hayo yote mtazidishiwa. Basi msisumbukie ya kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake” (Mathayo 6:33-34)
VYANZO VYA HOFU (kibiblia)
Kutokuwa na mwongozo wa Roho mtakatifu!
Kukosa mwongozo wa Roho mtakatifu kutakufanya ukose uhakika wa pale unapoelekea na ndio maana Yesu alisema “lakini mtakapo pelekwa pelekwa, msifikiri fikiri mtakayo sema , maana mtapewa saa ileile mtakayosema ,. Kwa maana si ninyi msemao bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu” Mathayo 10:19-20 , kukosa mwongozo wa Roho kuna mletea mtu hofu na kushindwa kuamua.
Kutokufunga na kuomba
Mtu asiyeishi maisha ya maombi anakuwa na imani dhaifu, ambayo inasababisha hofu, tunajifunza Yesu alipoona mateso anayoyaelekea kuwa ni mazito sana, akachukua hatua ya kuomba Yesu alijua hofu ni dhambi na kuyaogopa mateso ni dhambi akaamua kushindana dhambi hiyo hadi kutoa machozi ya damu, biblia inasema “hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi” Waebrania 12:4, Yesu alipambana kuishinda dhambi ya hofu! Lazima tupambane na hofu!
Kutokusoma na kutafakari neno la Mungu
Mtu asiyesoma neno la Mungu imani yake inakuwa ndogo, ambayo haijalishwa neno la kutosha, mfano wa Petro, alimwona Yesu anaelea kwenye maji akataka kumfuata Yesu akamwambia njoo, katikati akaona shaka akataka kuzama sasa angalia maneno ya Yesu “Mara Yesu akamshika mkono akamwambia , Ewe mwenye imani haba , mbona uliona shaka” uhaba wa imani unasababishwa na upungufu wa maneno ya Mungu, ukisoma neno la Mungu unaikuza imani yako na kwa kutafakari unaimarisha ulichoingiza! Hapo hofu itakosa nafasi kwako kabisa!
Kitokuwa na Imani
Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo , ni bayana ya mambo yasioonekana kwa macho. Kutokuwa na imani ni kutokuwa na uhakika wa mambo ya tarajiwayo, hii ni sababu moja wapo ya hofu kama tulivyoona hapo juu. Watu wengi wameishi kwenye mateso kwasababu ya hofu yamkini hata wanaomwamini Yesu kristo! Hii ni kukosa imani na kuishi maisha yasiyoya imani ni dhambi mbele za Mungu! “kwa kuwa tendo lolote lisilotoka katika imani ni dhambi” 1kor 14:23
MADHARA YANAYOSABABISHWA NA HOFU
Unakuwa mtumwa
Hofu inaweza kumfanya mtu akawa mtumwa , biblia inasema “….mlipokuwa watumwa wa dhambi…..”warumi 6:17,20 , hofu ni dhambi ambayo inatuweka katika utumwa , utahofia kila kitu , kila mtu n.k. umelala unasikia kitu kinapiga kelele nje unajikuta umeogopa, utumwa! Ila Yesu alituokoa kutoka kwenye utumwa wa hofu “maana Kristo naye alikufa ili kwa njia ya mauti amwaribu yeye aliyekuwa na nguvu,ili awaweke huru wale ambao maisha yao yote kwa sababu ya hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa”
Ni kumdharau Mungu na neno lake
Hofu ni kumdharau Mungu na neno lake, kwenye biblia neno usiogope limeandikwa zaidi ya mara 365, hii ni kuonyesha hofu haitakiwi “…maaana hofu ina adhabu…” kwahiyo hatutakiwi kuwa na hofu, kabisa! “….maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku” Yakobo 1:6
Maombi yako hayatajibiwa
“Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kutoka kwa Bwana” Yakabo 1:7 hivyo hofu huzuia maombi yako yasijibiwe, na Mungu kwahiyo yanakuwa kama kelele tu! Wala Mungu hayajibu jiulize ushaomba mara ngapi ukiwa na hofu ukajibiwa?
Itakupelekea kutupwa Jehanum
“Bali waoga , na wasioamini na wachukizao,na wazinzi, na wachawi…..sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kibiriti..” ufunuo 21:8 . unaona wenye hofu ndo miongoni wa watu wa mwanzo kutupwa Jehanamu, Hofu ni dhambi yenye uwezo wa kukupeleka motoni jiangalie maisha yako yakoje je unaishi katika hofu? biblia inasema “Basi msiutupe ujasiri wenu, maana una thawabu KUU” neno KUU lina maana sana hapo!
Nitatokaje kwenye maisha ya Hofu.
Hofu haikutoka kwa MUNGU “MAANA Mungu hakutupa Roho ya hofu , bali ya nguvu na ya moyo wa kiasi” 2 timotheo 1:7 Kama tulivyoona hofu ni dhambi, kama ni dhambi unatakiwa uchukue hatua ya kutubu kwanza kutoka ndani, halafu uichukie kabisa hofu, kutubu huku kunatakiwa kuendane na kuanza kusoma neno la Mungu na kulitafakari, kufunga na kuomba ili kupata nguvu ya kuishinda hofu! Mwombe Roho mtakatifu akupe ujasiri zaidi na zaidi, utaona maisha yako yatabadilika utaanza kumuona Mungu yuko karibu na maisha yako! KUMBUKA BAADA YA KUTUBU USIRUDI TENA KWENYE UTUMWA WA HOFU!!! UBARIKIWE,
e-mail: davidmgongolwa@ymail.com

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

8 Responses to JINSI HOFU INAVYOWEZA KUKUWEKA KATIKA HATIA!

 1. Nice post. I learn one thing tougher on totally different blogs everyday. It can all the time be stimulating to learn content from different writers and observe just a little one thing from their store. I’d desire to make use of some with the content material on my blog whether or not you don’t mind. Natually I’ll provide you with a link on your net blog. Thanks for sharing.

  Like

 2. apartamenty says:

  WONDERFUL Post.thanks for share..more wait .. …

  Like

 3. I am probably not much older than you John, but I also dont understand a lot of the technology I see around me. For example, when I see kids, about in groups, they dont seem communicate with each other, at least not in person. Instead they seem to be constantly texting their other friends. I find it bewildering and rude.

  Like

 4. Levi's Jeans says:

  Wonderful goods from you, man. I have understand your stuff previous to and you are just extremely excellent. I actually like what you have acquired here, certainly like what you’re saying and the way in which you say it. You make it enjoyable and you still care for to keep it sensible. I cant wait to read much more from you. This is really a tremendous web site.

  Like

 5. Loyd Girres says:

  I like this blog very much so much wonderful info .

  Like

 6. I adore your producing design, do keep on writing! I’ll be back!

  Like

 7. Joshua Megson says:

  Nabarikiwa sana na mafundisho pastor ,Mungu akubariki sana

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s