WALICHOKIFANYA UFUFUO NA UZIMA KUWAACHIA MADHABU AKINA SAMWEL SITTA NA MWAKYEMBE, JE! NI SAHIHI?


Bwana Yesus asifiwe wapendwa, Tumestaajabu kwa kitendo cha Dhehebu la Ufufuo na Uzima (Church of Christ) Dar es salaam makao makuu kwa mchungaji kiongozi Josephati Gwajima, kuwaachia Madhabahu wanasiasa Samwel Sitta (Waziri wa Jumuiya ya Africa Mashariki) na Herrison Mwakyembe (Naibu waziri wa Ujenzi) walisimama katika madhabahu hiyo na kutangaza kwamba Mwanasiasa Harrison Mwakyembe alipewa sumu. “Walimjaribu kwa Sumu, mimi nasema Hadharani ili taasisi inayofanya uchunguzi harakishe majibu” alisema Sitta.
Jamani sisi tunavyofahamu Madhabahu ni mahara pa kuheshimiwa ambapo mambo yanayotakiwa kuzungumzwa pale ni mambo yanayohusu Mungu tu. hawa wanasiasa wana sehemu zao za kusemea hayo mambo yao. Ufufuo na uzima tulikuwa tukiwa-support sana na ni rafiki zetu wazuri, lakini katika hili nahisi kama mmejikwaa hebu kaeni chini tena mlipitie hili, sina maana kwamba nawahuku mmefanya dhambi ila nina wasi wasi kama mmejikwaa vile. Gwajima ni mchungaji mzuri tunakupenda sana, hivyo hatutakubali kuona shetani anakutega halafu tukae kimya ni lazima tumpinge shetani. nakuomba, wanasiasa wasijiingize kisiri katika neno la Mungu ili wapate kutangaza majungu yao ya kisiasa, najua wanakufuata si kwa sababu wewe ni mtumioshi wa Mungu, bali kwa kuwa wanafahamu unawatu wengi basi watajipatia wapiga kura. ati wanasema wakuja kutoa ushuhuda! waongo hawa!

Na Nyinyi wanasiasa mkitaka kutangaza mambo yenu ya kisiasa jengeni jukwaa lenu, sio kwenda nyumbani mwa Bwana na kupaza sauti zenu kupondana kisiasa, acheni Mungu hachezewi.

Bwana awaongoze watu wake katika Jina la Yesu.

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

12 Responses to WALICHOKIFANYA UFUFUO NA UZIMA KUWAACHIA MADHABU AKINA SAMWEL SITTA NA MWAKYEMBE, JE! NI SAHIHI?

 1. Frederick Marandu says:

  Praise GOD!Jamani viongozi walipokwenda loliondo tuliwaon washirikina sasa wakija kanisani kuhuhudia tusiwafukuze ni MUNGU anawaleta tupange utaratibu na jinsi gani washuhudie mradi tusiwape madhabahu waka tumia kisiasa lakini kama wamekuja kujitakasa ushirikina na kumrudia MUNGU tuwahubirie wasimame waokoke ni watu ambao MUNGU amewauba anawahitaji sana waongoze nchi chini ya uongozi wake.
  mbarikiwe.
  na Frederick Marandu

  Like

  • mosespk says:

   Fedrick ubarikiwe sana, ni kweli kabisa Kiongozi akija kanisani hata kama kaja kwa nia mbaya atakutana Mungu ambadilshe, nakumbuka kunamflme alikwea kwenda kuwakata akina Elisha lakini alipokaribia sehemu ile yeye na jeshi lake wote wakaanza kunena kwa Lugha, kweli tuwaacheni viongozi, lakini wasitumie madhabahu katika nyanja za siasa. ubarikiwe mtumishi.

   Ev.Moses

   Like

  • frank says:

   mimi naitwa frank,ninapenda kukushauli wewe muuliza swari kama mtu wa mungu,usipende kuwa mwepesi wa kuongea maana biblia inasema katika kitabu cha “yakobo 1:19” tuwe wepesi wa kusikia ila tusiwe wepesi wa kusema wala kukasirika,gwajima alivyowaita wanasiasa huwezi kujua lengo lake ni nini! hata kama ningekuwa mimi ningewaita hao wanasiasa ili upate kujua nchi yetu inaendaje?maana watu hawa wakieleza ukweli juu ya nchi inakuwezesha wewe kama mtu wa mungu kuiombea nchi yako maana wewe ndio unayeweza kubadilisha nchi kwa kuiombea vizuri maana ukimjua adui yako ni vyepesi kumuangamiza.ndio maana hata yoshua alipokuwa anataka kuiangamiza nchi alituma watu wakapeleleze nchi na walipomaliza kuipeleleza yoshua na israeli walishinda “yoshua 7:2” ila mimi kinachinishangaza ni kwamba watumishi wengi baada ya gwajima kuinuliwa wamekuwa wanamuonea wivu! ndio maana hawaangalii ni mema mangapi ameyafanya ila wanatafuta mabaya mangapi atatenda! tukifanya hivyo kama watoto wa Bwanayesu hatutafika popote.maana timu moja ikishinda anayefunga goli ni mmoja ila washangiliaji ni wengi! hivyo sisi wote katika kristo ni timu moja akishinda gwajima sisi sote tutashangilia.tubadilike!!!!!!!!!!!!
   mungu atubariki!!!!!!!!!!!!!!!!

   Like

 2. Rose Paul says:

  Unajua kilicho kuwa kinazungumzwa? Mbona unaweka wing eti 2likuwa 2nampenda jisemee peke yako tatizo nyie wanadamu mkiona mchungaj anaongea na mwana siasa mnadhan anaishu nao au hujui watu wote ni watoto wa MUNGU pale haikuwa siasa kwan hawakuruhusiwa kutoa ushuhuda kwani wao wanaish dunia ya nan au hao wanasiasa hawana dini?
  Unajua alichoitiwa huyo Sitta?

  (From Facebook):

  Like

  • Eliya says:

   Sister Rose labda nikusaidie, si kila mtu ni mtoto wa Mungu, Biblia inasema Yh.1:12 “Wote waliompokea aliwapa uwezo kufanyika wana wa Mungu.” Kwa hiyo mtoto wa Mungu ni yule aliyempokea Yesu tu. swali linakuja Je! yeye asiyempokea Yesu ni mtoto wa nani? Biblia iko wazi inasema Atendaye dhambi ni wa Ibirisi. pia Yesu akasema wazi Yh.8:44 Nyinyi mnababa yenu ambaye ni Ibirisi. kwa hiyo dada mara nyingine tena usirudie kusema watu ni watoto wa Mungu.

   Like

 3. Meinrald says:

  Time will tell….

  Like

 4. Mpoki mwaki wa baba Groly says:

  Mnanipa wakati mgumu kuchangia mada ambayo suluhisho la majibu yake yapo,jamani mtoa mada mi nilifikiri unajua issu nzima,Pastor Gwajima yupo yuapatikana mda wote kawe simu zake na mawasilaiano mengine yakumfikia yapo wewe au nyie wenyewe mnapajua kawe kanisani,ni jambo la busara kwenda na kujua nini maana yake na madhumni yake,ili mwili wa Kristo ujengwe,sasa mwasema mnaona kapotoka keteleza jamani,nyie watumishi wa Mungu leteni maada yenye mashiko na iliyo kamilika,nawashauri mkamuulize Gwajima naamini ana jambo na maelezo ya kutosha,hapa na nyie mmepotoka.Mwamanini Mungu mtathibitika waminini watumishi wake mtafanikawa,nawaheshimu nawapenda,asante kwa kazi ya kuujenga mwili wa Mfalme Yesu,amina.

  Like

 5. samson, says:

  Ndugu zangu wapendwa Munaopendwa sana na Mungu Baba Wa Mbinguni ninaomba ridhaa yenu kuchangia hoja nikitaka kusema kuwa hapa duniani mwanadamu anaishi katika mitazamo miwili mtazamo wa ki mwili na mtazamo wa kiroho, na haya mambo mawili hayachangamani sana,
  kazi ya Mungu inaongozwa na Mungu kupitia Roho Mtakatifu, hivyo ukitaka kujuwa sana ya Rohoni lazima uwe Rohoni na Ukitaka kujuwa sana ya Mwilini pia inakulazimisha ufanye hivyo,

  Ninaamini Madhabau ya Bwana inamaagano yaani makubaliano au marithiano Baina ya Mungu na aliyekabidhiwa madhabau, hivyo Mpaka Mtumishi wa Mungu anawakaribisha wanasiasa madhabauni maanayake yeye anafahamu anachokifanya na ameona hakina madhara kwake na kwa kundi analolisimamia pia, mwisho niseme Mungu akiangalia chuni ya jua anawaona wanadamu tu, na haoni vyeo vya mtu yeyote, vyeo vyote hivi ni miundo iliyowekwa na wanadamu kurahisisha kazi, hivyo tusibaguane tusitengane tusichukuane tusichunguzane bali tusaidiane kwa kuombeana toba ya kweli na kushahuriana, Mungu awabariki kwa swali, na Mungu ampariki pia aliyetuonganisha katika blog hii,
  ni Mimi samson,

  Like

 6. godian says:

  Bwana yesu asifiwe!! najiuliza jambo moja.je kama shekhe yahya angeokoka na akawa anatoa ushuhuda mngesemaje?? halafu katika biblia Miriam alipata ukoma kwa sababu kama hii!! Swali langu sasa je kama mungu angelikuweka katika nafasi ya gwajima af akakwambia ufanye vile ungefanyaaa au ungepuuuza??? acheni kukurupuka ili mpate coment bhanaaa!!

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s