JE NI HALALI KWA WAIMBAJI WA INJILI KUIMBA KATIKA MATAMASHA YA KI-DUNIA?

Yesu wetu apewe sifa ndugu zangu, jamani kunamatamasha ya ujasiliamali ambayo yanajulikana kama Street university ambayo huedeshwa na akina Erick Shigongo, matamasha haya yameleta sura mpya baada ya waimbaji wa Neno la Mungu kama: Christina Shusho, Bonny Mwaitege, Abass Hamis Kinzasa, Glorious Singers na Pastor Wambura. kuonekana wakitumbuiza katika moja ya matamasha hayo lililofanyika mjini Arusha 27 November 2011. watu walifurika na walifurahi kwa kile walichokiita ni Burudani kutoka kwa waimbaji hao, jamani waimbaji hii si halali, ninyi mmeitwa na Mungu ili mmwimbie Mungu, yeye Mungu hajawaita muwaimbie wajasiliamali wala kuimba kwa kuwaburudisha wanadamu! hii sio sahihi kabisa, tena mnakutanishwa jukwaa moja na waimbaji wa Duniani wenye kusifu zinaa! si vizuri nyinyi muimbe pamoja na waimbaji wa ki-dunia katika jukwaa moja mkisisitiza jambo flani kwa nia moja huku wenzenu wakiimba nyimbo za kusisitiza uasherati, au ndio mtaniambia “Mwanasimba atalisha pamoja na mwanakoo siku za mwisho?” Jamani hawa wajasiliamali dhamira yao sio kumtukuza Mungu ila ni kujipatia wateja katika programu zao, sasa wanawatumia nyinyi kama vivutio vya wateja wao.

Ndugu zangu katika Bwana, hebu tafakarini katika hili, mumejikwaa acheni kufanya hivyo.

Na Nyinyi Wajasiliamali acheni kuwatumia waimbaji wa Mungu katika kampeni zenu. Tena kama wewe Erick unamjua kabisa Mungu vizuri lakini Shetani unampa Nafasi akuvute ili uzidi sana katika kumchukiza mungu! acha mara moja. Tafuta njia mbadala ya kuvuta wateja lakini usitumie chochote kitokacho Madhabahuni kwa Bwana, kama unasikio na usikie Acha kabisa usirudie tena.

Bwana awasaidie katika jina la Yesu.
=======================================================================

Ndugu msomaji tunaomba mtazamo wako na uelewa wako kuhusu jambo hili, je wewe unasemaje katika hili, Ni sahihi?

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

3 Responses to JE NI HALALI KWA WAIMBAJI WA INJILI KUIMBA KATIKA MATAMASHA YA KI-DUNIA?

 1. Frederick Marandu says:

  Bwana asifiwe!Mimi hapa naona pamoja na kwamba kama wana kosea lakini hapo kuna andiko linatimia ya kwamba injili itahubiriwa kila mahali na kwakila kiumbe!wengine wasiopenda kuhudhuria ibada ambao hawajui hata ninyimbo gani zinaimbwa ktk ibada nao wana pata mda wainjili ya njia ya uimbaji na hawata kuwa na nafasi ya kusema sikusikia injili,labda basi wenzetu mnao imba mkipata nafasi hiyo jiandaeni mpate watu waokoke kwa njia ya kuhubiri kwakuimba ili msitoke bure najua wapo wengine huwapati hadi katika matamasha ya mchanganyo! tumieni nafasi mpate kondoo hapo hapo mkiwa na Erick,najua kuna samaki wanapatikana baharini lakini wapo wa bwawani lakini wote nisamaki ukiwa mvuvi mzuri utavua kila eneo ukiwa baharini utavua ukiwa ziwani utavua! fanyeni kazi kwa mitindo mbali mbali watu waje kwa YESU!
  mbarikiwe
  Frederick Marandu

  Like

 2. Meinrald says:

  Tatizo hata nyimbo nyingi za injili nyingi ni entertainment zaidi,hazipo kiinjili,watu wanasikiliza kujifurahisha,pale ilikuwa ni burudani zaidi,

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s