MGOMO WA MADAKTARI PROFESSIONAL WAANZA RASMI HOSPITALI YA MUHIMBILI

Ikiwa ni siku chache baada ya kuanza kwa sakata la mgomo wa madaktari nchini Tanzania na serikali ya nchi hiyo kuwataka madaktari kurejea kazini mara moja, hali imekuwa tofauti na sauti ya serikali, madaktari professinal wa hospitali ya muhimbili walianza mgomo rasimi hapo jana tarehe 06/02/2012. hadi saa 10 jioni wazazi wapatao 400 walikuwepo hospitalini hapo huku wakibaki hawana huduma, hivyo Tanzania kutarijia vifo vya wazazi 400 kwa siku ya jana. wakati huo huo vilio na maombolezo vilisikika katika baadhi ya vyumba vya kulaza wagonjwa vya hospitali hiyo. akizungumza na chanzo chetu cha habari pasipo yeye kujua, msemaji wa hospitali hiyo alisema, “tumeamua kugoma baada ya serikali kupuuza malalamiko yetu” lakini pamoja na haya mchungaji kiongozi wa kanisa la GRC Antony Lusekelo alikaririwa na chombo kimoja cha habari akisisitiza madaktari wasitishe mogomo warudi kuokoa maisha ya watanzania. Lusekelo alisema “usibishane na mjinga, nenda kaokoe maisha ya ndugu zako” Wakati huohuo mtandao huu ulimtafuta mwasisi wa New Hope Ministry Ev.Moses Mayila naye alitoa kauli. “Mchungaji Lusekelo ametoa ushauri mzuri sana, lakini Madaktari wamejaribu kufanya hivyo siku za nyuma wakaona mambo yako kimya, na ndio maana wameamua sasa kukataa kufanya kazi, najua hawajagoma kuwahudumia watanzania lakini wamegoma kwa sababu mwajiri wao anaonekana kutowajari, na ndio maana wameamua kusitisha huduma” Moses alipoulizwa na mwandishi wetu kwamba yeye anamaoni gani ya kuishauri serikali alisema “Ni jambo ambalo serikali ingelifikiria tangu mwanzo katika bajeti yake, kwani tatizo la madaktari halijaanza leo. Serikali ilipaswa kutoongeza wizara ya uchukuzi badala yake pesa za kuilipa ile wizara zingetumika kulipa madeni ya wizara ya afya, pia serikali ingepunguza posho ya wabunge ili kubalance na pesa hiyo ingewalipa wataalamu wa wizara zingine. kwa hiyo naishauri serikali ivunje wizara moja badala yake iiunganishe katika wizara nyingine kama ilivyokuwa hapo awali ili kuokoa jahazi la Tanzania” alisema Moses. Hata hivyo shukrani kwa serikali ya Tanzania na Jeshi la ulinzi kwa kupeleka madaktari kutoka jeshi la ulinzi, Pamoja na madktari hao lakini hali bado ni tete Hospitalini hapo. Jamani taifa hili linahitaji maombi kwani hali ni tete kwa sasa. watu wanakesha wakiomba wasiugue, kwani ukiugua tiba kwa sasa ni ngumu. Bwana aisimamie tanzania, Bwana awapatanishe madatari na Serikali yao.

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

4 Responses to MGOMO WA MADAKTARI PROFESSIONAL WAANZA RASMI HOSPITALI YA MUHIMBILI

 1. jonson says:

  Ev.Moses nakuunga mkono, ni kweli tumejaribu sana kupiga kelele hapo mwanzo lakini serikali haikutusikiliza, wamechukua mada wakaipeleka bungeni lakini ikapuuzwa. hata waziri mkuu tumemwomba sana lakini cha ajabu hakutokea mapema, na alipojitokeza akaona madaktari wamechelewa akakasirika akaamuru turudi kazini mara moja, yeye alisahau kwamba tulimwomba aje kwa muda wa siku kadhaa lakini hakuja. sasa na sisi tumeamua sasa mpaka kieleweke, kama hawataki sisi tutakwenda nje tutakwenda private na sehemu zingine kawani daktari sio kama mwanasiasa kwamba anabanwa na mipaka ya nchi yake. serikali mkipenda mtusikilize na kama hamtaki sawa hatuna shida.

  Dr.Jonson
  some where in Tanzania

  Like

 2. peter joe says:

  kweli kabisa Dr.Johnson, kazeni msuri, lakini angalieni huko nyuma ndugu zenu tunakufa. huruma basi kidogo.

  Peter Joe-Arusha

  Like

 3. sifa says:

  Madaktari mngekuja kwanza kuona matatizo ya wananchi, watanznia wanataabika sana, tumepoteza ndugu zetu wengi. hebu jaribuni kuangalia tena katika hili.

  Like

 4. Alamokola says:

  Ni kweli wapendwa mnagoma, sikatai inawezekana serikali haijawatendea haki lakini kumbukeni kazi yenu ni kama huduma. Hivi kweli wanaokufa kutokana na huu mgomo si ni watu kama sisi. Kwa nini tusifanye kazi, ina maana hatujui hata neno moja la Quran au Biblia juu ya kuwahurumia wahitaji? hasa wagonjwa? Hawakupenda kuwa wagonjwa na yeyote kati yetu aweza kuugua unaonaje ukigomewa na unayetegemea akupe tiba.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s