BADO TUNAMKUMBUKA FANUEL SEDEKIA

Bila shaka jina hili si geni kwa walio wengi, Mtumishi wa Mungu Fanuel Sedekia alitutoka usiku wa kuamkia 05/01/2009 huko Israel. Mwili wake ulirejeshwa nyumbani kwake na mazishi yake yalifanyika 10/01/2009. ameacha pengo kubwa sana hasa kwa watumishi. bado tunamkumbuka sana, tunakumbuka kazi zake katika utumishi zikiwemo tungo zake zenye mguso kiroho. Ni kweli tulikuwa bado tunamhitaji sana huyu mtumishi lakini Bwana alikusudia kumuondosha. Ingawa tunayo matumaini ya kumuona tena huko nyumbani kwa Baba lakini tunaumia sana tukimkumbuka Fanuel, lakini hatuna budi kukubali matokeo. Bwana alimtoa Bwana amemtwaa Jina lake lihimidiwe.Amina

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

3 Responses to BADO TUNAMKUMBUKA FANUEL SEDEKIA

 1. Christopher Mwakasege says:

  USHUHUDA WA KIFO CHA SEDEKIA
  Roho mtakatifu akwambiavyo omba hiyo haina MJADALA ni kuingia kwenye maombi mpaka upate unachokiomba kwa kuwa gharama ya kuingia kwenye maombi ili kupata ulichotakiwa kukipata ni ndogo kuliko gharama ya kukosa kile ulichoambiwa ukipate katika Maombi hayo.

  Roho mtakatifu anapokupa mzigo wa kuombea jambo anakupa na muda ukizembea muda huo ukipita kinakuwa ni kiporo, na kiporo kinaweza kikalika na kipo ambacho hakiliki. .

  “Tulipoenda Israel na Fanuel Sedekia kisha akaanza kuumwa madaktari waliniambia ubongo wake kwa asilimia tisini haufanyi kazi. Lakini walishangaa kwa nini kila mara niko pale Hospitali wakasema kwa nini usikae tu Hotelini kisha ukawa unapiga simu kuulizia hali ya Mgonjwa? Wao hawakujua kwa nini naenda pale kwa kuwa suala la kupiga simu tu sio tatizo ningeweza kurudi Arusha kisha nikawa napiga simu.

  Suala hapa ni kuwa nilikuwa naenda kila mara kwa ajili ya kumfanyia maombi, nilikuwa nakaa kandokando ya Bahari ya Galilaya nafanya maombi juu ya Sedikia kwa masaa sita nikitoka hapo nasikia upako wa ajabu sana kIsha napanda Taxi kuelekea Hospitali. Nikifika Hospitali madactari na watu wa ICU walikuwa washanifahamu hivyo naenda moja kwa moja kwenye chumba cha nguo nabadili nguo kIsha naingia ICU alikolazwa.

  Nikifika nambana Mungu kwa maswali Mengi namuuliza Sedekia, hivi unaongea nini na Yesu muda wote huo si urudi? na kisha namuuliza Yesu, hivi Yesu si unafahamu kuwa Sedekia anamke ukimchukua mkewe atamuachia nani? Kisha baada ya maneno hayo naweka mkono juu yake. Nilipokuwa nikiweka mkono juu yake ghafla upako wote unakuwa kama umenyonywa.

  Baada ya hapo narudi hotelini naanza tena kumuuliza Mungu hivi Mungu kama basi husikii maombi yangu sikia maombi ya watanzania kwa kuwa saa hiyo nilijua watanzania wengi wanamuombea Sedekia.

  Inafikia wakati nakata tamaa lakini ndani yangu najisemea Mwakasege haiwezekani jitie moyo kisha nabadili aina ya maombi, kwa kuwa nilikuwa na nguo zake pamoja na passport yake nikawa naviweka kati kisha nikawa naanza maombi ya Yeriko, nikawa niko hotelini usiku nazunguka nguo zake na paspot yake huku nikifanya maombi.

  Taratibu Mungu akaanza kuniambia kuwa sedekia harudi, Kipidi hicho mimi na familia yangu tulikuwa tumepanga kwenda kupumzika nchini Uingereza wakati wa skukuu ya Chrismass, na booking mpaka ya Hotel tulikuwa tumeshafanya, na watoto wote wako nyumbani wakijiuliza tunaendaje kupumzika wakati Sedekia anaumwa? Chrismass ikapita na mwaka mpya pia kisha Sedekia akafariki.

  Baada ya kifo hicho sikuchoka nkarudi tena kwa Mungu nikamuuliza kwa nini Mungu umeamua kumchukua Sedekia mikononi mwangu? Mungu alinijibu vitu ambavyo siwezi kuvisema hapa.

  Kila siku mimi ni mgeni katika maombi namhitaji ROHO anifundishe kwa upya kwa kuwa sijui vita gani ninakwenda kupambana nayo, Mungu anabaki kuwa Mungu kwa kuwa hufanya atakavyo”

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s