MSAADA WA MUNGU WAKATI WA DHIKI

Karibuni tena katika kituo chetu cha kujifunza maneno ya Mungu wetu, Jina langu ni Ev.Moses Mayila.

Leo tutajifunza kuhusu ‘MSAADA WA MUNGU WAKATI WA DHIKI’ katika somo hili tutajifunza jinsi Mungu anavyokuja kukusaidia katika taabu na dhiki. Tutajifunza kupitia Injili ya Yohana 11, Biblia imesema Lazaro aliugua sana, dada yake akatuma mtu kwa Yesu ili kumpasha habari Bwana kwamba rafiki yake Lazaro ni mgonjwa sana. Yesu alipozipata habari hizo hakwenda kumponya Lazaro wala hakutamka neno lolote la uponyaji juu ya Lazaro. Pampoja na kwamba Yesu alimpenda sana Lazaro lakini hakwenda kumuangalia katika dhiki yake, mpaka ikafika hatua Lazaro akafa, hata alipokufa yesu hakwenda msibani kwa Lazaro hata zikapita siku tatu siku ya nne ndipo akaenda msibani kwa Lazaro. Unajua kwa nini alifanya hivi? alifanya hivi makusudi kwa sababu katika imani za wayahudi mtu akifa roho yake huwepo maeneo yale kwa muda siku tatu kiasi kwamba wakiomba sana ile roho inaweza kuurudia tena ule mwili, siku ya nne ile roho huwa imeondoka yaani kwamba hata wangefanya namna gani haiwezekani tena kwa mtu yule kuwa hai tena.

Sasa Yesu akakaa mpka siku ya nne siku ambayo inaaminika kwamba mambo ya Lazaro kuwa hai hayawezekani tena. hata dada yake Lazaro alipoambiwa na yesu kwamba lazaro atafufuka alisema ‘naamini atafufuka siku ya mwisho’ kwa hiyo hata yeye alikuwa amekata tamaa kwamba Lazaro hawezi kuwa hai tena. Ndipo Yesu alipoamuru waliondoe jiwe kwenye kaburi la Lazaro kisha akamwita “Lazaro Njoo Nje” Lazaro akatoka kaburini yu-hai. Watu wakastaajabu matendo makuu ya Mungu. Yesu alichelewa kwenda msibani makusudi maana kama angeenda siku ya kwanza wangesema roho ilikuwa karibu hata sisi tungeomba angefufuka. Lakini yesu akaenda walipokuwa wamekata tamaa wakisema mambo hayawezekani tena.

Ninachotaka kukuambia leo ni kwamba, yamkini umekata tamaa kama dada yake Lazaro unaona Mambo hayawezekani tena, Jipe moyo leo uamini kwamba Bwana atakuja kukusaidia. haijalishi umeshindwa. Pale unapoona umeshindwa huwezi tena yeye atakuja wakati huo huo na atakusaidia. Yamkini watu wanakucheka usikate tamaa wala usiwaangalie hao wewe mtazame Bwana katika dhiki zako, yeye yu-karibu nawe anasema mwanangu jipe moyo naja kwako upesi, acha kwanza ulimwengu useme umeshindwa ndipo nikusaidie mwanangu, hapo ulimwengu utanitukuza kupitia wewe.
Rafiki yangu usikate tamaa kaza mwendo katika Imani.
Bwana akusaidie sana katika jina lipitalo majina yote. Amina

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s