KUBARIKIWA SIYO KUWA NA MALI

Karibuni tena katika kituo chetu cha kujifunza maneno ya Mungu wetu, Jina langu ni Mwinjilisti Moses Mayila.

Bwana wetu Yesu kristo apewe sifa!

Leo tutajifunza kuhusu “KUBARIKIWA SIYO KUWA NA MALI” ni somo jipya ambalo litatupa mwangaza zaidi wa kujua nini maana ya kubarikiwa na ni mtu wa namna gani aliyebarikiwa.

Watu wengi wanafahamu kwamba aliyebarikiwa ni mtu mwenye mali nyingi na utajiri mwingi! na ndio maana hata baadhi ya waamini hutamani maisha ya matajiri kwa sababu
wanafahamu kwamba matajiri wamebarikiwa. na badhi ya watu hudhani kwamba Mungu amewabariki wenye dhambi matajiri kuliko watu wake walichao jina la Bwana, na husema
hivi kwa sababu wacha Mungu wengi hawana mali.

Biblia inasema “Heri yeye aliyesamehewa dhambi zake” Neno ‘Heri’ kwa lugha ya kingereza linatamkwa ‘Blessed” maana yake ‘Amebarikiwa’ Hivyo kwa kiswahili chepesi
ni “Amebarikiwa yeye aliyesamehewa dhambi” Hivyo basi kubarikiwa sio kuwa na mali nyingi wala utajiri, bali kubarikiwa ni kusamehewa dhambi. hivyo si kweli
kwamba matajiri wamebarikiwa, maana matajiri wengi wamejipatia mali kwa njia za udanganyifu, kutoa kafara, kupora, kuiba, dhuluma na kuua wenzao, hivyo mtu aliyesamehewa dhambi ndiye aliyebarikiwa! Mfalme suleman alikuwa tajiri kuliko mtu yeyote aliyewahi kutokea kbla yake Duniani, alikuwa akijiburudisha vya kutosha katika mali zake. Aliweka ulinzi wa kutosha ili kumlinda. kuna wafalme wengi katika kizazi hiki tunaona wanalindwa kwa kiasi kikubwa sana, wanalindwa na mitambo ya kisasa, Askari na mbwa, lakini hajawahi kuwapo mfalme anayelindwa kama alivyokuwa akilindwa sulemani, sulemani alikuwa akilindwa na askari na simba, simba mmoja alisimama mkono wa kuume na mwingine mkono wa kushoto wa mfalme. Sulemani akazidi sana katika utajiri, sifa zake zikavuma ulimwengini mwote, watu walimwendea na zawadi zenye thamani kubwa. Sulemani akazidi tena na tena katika utajiri, akaiambia nafsi yake “Jiburudishe na mali nilizonazo” lakini mwisho wa yote Sulemani akaulaani utajiri wake akisema “Huu ni ubatili na kujilisha upepo” Hebu fikiria, kwa nini sulemani alisema hivi! Sulemani alisema hivi baada ya kugundua kwamba kumbe kubarikiwa sio kuwa na mali, bali kubalikiwa ni kusamehewa dhambi!

Ndugu yangu katika Bwana usilalame tena kwa Bwana ya kwamba hajakubariki, maadam dhambi zako umesamehewa, tayari umekwishabarikiwa. Wala usitaabike kuhangaikia mali za ulimwengu huu ukidhani kwamba hizi ndizo baraka, bali mwambie bwana akupe mali na utajiri, naye atakupa kama akipenda. usilazimishe kwa nguvu kuwa na fahari za ulimwengu huu, kumbuka falme na fahali zote za ulimwengu huu ni za shetani (mathayo 4:8-9). Simaanishi kwamba watu wa Mungu hawapaswi kuwa na mali, Mungu wetu pia huwapa watu wake mali na utajiri, Biblia inasema “Mkumbuke Bwana Mungu wako wakupaye utajiri” hivyo ikiwa wewe ni mtu wa Mungu tayari huhitaji kuomba baraka tena, maana ulibarikiwa siku ile uliposamehewa Dhambi. Hivyo usisononeke tena moyoni mwako kwamba Mungu hajakubariki, Bali furahia katika bwana maana umebarikiwa tayari.

Kaa katika uwepo wa Bwana, tembea katika baraka, katika jina la Yesu. Amina

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

4 Responses to KUBARIKIWA SIYO KUWA NA MALI

  1. Meinrald says:

    Kazi nzuri Mtumishi,Neno Hili linatumika vibaya leo,Baraka zimehesabiwa ni za material things pekee,lakini baraka za rohoni ,kama kusamehewa,ulinzi wa Mungu N.K Hazionekani kama ni baraka.

    Like

  2. Anna Nyanda says:

    ubarikiwe mtumishi moses kwa kutuma mkate wa leo. Amen

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s