HASARA ZA KUBISHANA NA MUNGU

Ni Jumapili nyingine tena nikiwakaribisha katika kituo chetu cha kujifunza mambo ya Mungu wetu, Jina langu ni Ev.Moses Mayila.

Leo tutajifunza kuhusu hasara za kubishana na Mungu. Biblia inasema Zakaria alipokuwa mzee alitokewa na malaika kumpasha habari za kwamba mkewe Elizabeth atachukua mimba atamzaa Yohana mbatizaji. Lakini zakaria aliposikia maneno haya akasahau kwamba hakuna lisilowezekana kwa Mungu akaanza kubishana na yule malaika, akisema litawezekanaje jambo hili? mimi ni mzee sana na mke wangu pia amezeeka sana. ndipo malaika akamjibu akamwambia, “Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema. Na tazama! Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu; nayo yatatimizwa kwa wakati wake. (LUKA 1:19-20).

Tazama kwa Zekaria, mzee huyu alipata taabu kubwa ya bila kuzungumza kwa muda wa zaidi ya miezi nane, na hii ilikuja mara baada ya kubishana na Mungu, Mungu alimwambia nataka nikupe mtoto, lakini Zekaria akaanza kubishana na Mungu akisema hili haliwezekani! kwa maana nyingine Zakaria alimaanisha kwamba Mungu hana uwezo kuweka mtoto tumboni mwa Elizabeth kwa sababu Elizabeth ni mzee sana na yeye Zekaria ni mzee sana! alisahau kwamba Mungu ndiye aliuweka mfumo wa kuzaa uwapo kijana na kuacha kuzaa uzeekapo, kwa hiyo kama yeye ndiye kaweka mfumo huo basi anauwezo wakubadilisha mfumo, anaweza akakubadilishia mfumo, badala ya kuzaa ujanani, basi utazaa uzeeni. Zacharia hakuangali hilo, kwa sababu alionesha ubishi mungu akaamua kumpa adhabu Zekaria , na hii adhabu hata mimi nasema alistahili apewe kwa sababu yeye alikuwa kuhani, tena alizaliwa ukoo wa Ibrahim, kawa hiyo alikuwa anafahamu kabisa historia ya baba yake Ibrahim, Mungu alimwahidi Ibrahim kumpa mtoto lakini hakumpa alipokuwa kijana akamwacha mpaka akawa mzee sana, hata mkewe (Sarah) naye akawa ni mzee sana ndipo Mungu akawapa mtoto (Isaka). haya yote Zekaria alikuwa akiyafahamu lakini akaanza kubisha tu. Mungu akampa adhabu akawa Bubu!

Mtu mwingine ni Nabii Balaam, Balaam alitaka kwenda kuwalaani waisrael walipokuwa wakitoka Misiri, Mungu akamzuia, lakini Balaam hakusikia akaendelea kumuuliza Mungu, “niende kuwalaani?” Mungu akamzuia, Balaam akaenelea tu kumuuliza Mungu “Niende nikwalaani?” hatimaye Mungu akakasirika, hivyo kwa hasira akamwambia “Nenda” Alipokuwa njiani akienda kuwalaani waisrael, akafika sehemu flani punda wake akaacha njia akaanza kuingia vichakani, alimpiga na kumrudisha barabarani, lakini alipofika tena ile sehemu punda akaacha njia tena akaingia vichakani, Balaam akampiga tena, basi yule Punda akaongea! akamuuliza “Hivi wewe hujiulizi ni kwa nini nafanya hivi? kila siku unanipanda sifanyi hivi, kwa nini leo nafanya hivi? Kisha akamuona malaika ameshika upanga mkali amesimama mahara pale ambapo punda aligoma kupita, yule malaika akamwambia unabahati punda aliniona nilikuwa nataka nikumalize kabisa!

Angalia, Balaamu kwa sababu ya kubishana na Mungu alikoswa koswa na kifo! laiti kama angemsikia Mungu yote yale yasingempata.

Mpendwa wangu, yamkini na wewe umefananishwa na Zekaria au umefananishwa na Balaam, Mungu anataka akufanyie kitu flani katika maisha yako lakini wewe wasema hayawezekani haya. yamkini Mungu anazungumza na wewe kwa njia mbalimbali kama maono, ndoto nk. na mara nyingi sana mungu huzungumza na watu wengi sana kwa njia ya ndoto, halafu bahati mbaya watu wengi huwa hawaelewi kama Mungu ndiye amesema nao kwa njia ya ndoto, itabidi niandae somo hili ili kuwasaidia watu wa namna hii. Mungu amesema na wewe kuhusu hayo maisha yako, yeye anataka kuyabadilisha lakini wewe unabisha unasema hawezi. Yamkini Mungu amekuwa akikuzuia jambo flani kama alivyokuwa akimzuia Balaam, lakini wewe umekuwa mbishi kama balaam! yamkini Mungu amekupa onyo la mwisho juu ya ubishi wako kama alivyo muonya Balaam, kuwa mwangalifu, Mungu takupa adhabu kama alivyomwadhibu Kuhani Zekaria! au kuwa mtiifu kama yusufu, kubali Mungu afanye ayatakayo kwako. mwambie bwana tenda lolote utakalo kwangu. na mara ukigundua Mungu amesema na wewe hakikisha unatii ulichoambiwa.

Bwana awabariki nyote, kwa jina la Yesu. Amina

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s