TUWAOMBEE WAIMBAJI WA TANZANIA MAANA WAMETEKWA NA DUNIA NA SHETANI PIA.

Shalom tena watu wa mungu!

Ni mara nyingi sana nimekuwa nikipiga kelele juu ya waimbaji wetu kujihusisha na mambo yaliyo kinyume na sheria ya mungu katika huduma zao. nilipiga kelele juu ya suala la kuwatoza watu pesa ili waingie ukumbini kusikiliza ujumbe wa neno la Mungu kwa njia ya Nyimbo. Juzi juzi tena nimepiga kelele juu ya waimbaji waliotumiwa kama kivutio cha biashara za akina Eric Shigongo. na leo tena napiga kelele juu ya jambo flani.

Kusema kweli mimi sitanyamaza, nitaendelea kusema, kukemea na kuonya mara nimwonapo mwamini mwenzzangu anakwenda kinyume. Juzi juzi kuna mashindano yaitwayo Eeast African Music Awards, cha ajabu hapa ni kwamba waimbaji wa nyimbo za kumwimbia Bwana wamekwenda kushindana katika mashindano hayo! hii Ni ajabu sana ndugu zangu.

Biblia katika wafilipi 2:14 inasema “Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano mpate kuwa wana wa Mungu” kwa hiyo tunajifunza kwamba kumbe katika mambo ya mungu tukiyafanya pasipo mashindano, mfano: tukihubiri bila kushinda, tuiimba bila kushindana, tukisali na kufunga bila kushindana, basi tunapata kuwa wana wa Mungu. Bali tukisali na kufunga kwa kushindana, tukihubiri kwa kushindana, tukiimba kwa kushindana, basi sisi si wana wa Mungu, na asiye mwana wa mungu ni mwana wa shetani. Ikiwa tumekosa sifa za kuwa wana wa Mungu basi baba yetu ni Shetani Yoh.8 44 (Nyinyi mnababa yenu ambaye ni ibirisi).

Nimekaa chini nikaghadhabika sana kwa mambo haya, kisha nikafadhaika, kwanini nduguzangu wanafanya hivi? badaaye nikawaza nikadhani yamkini katika haya mambo manne ndiyo yanayosababisha waimbaji wamwimbiao Mungu wetu wachukuliwe mateka. mambo hayo ni: (1) Pesa (2) Tamaa (3) Sifa (4) Ibirisi. Mambo haya ndiyo chanzo kikubwa cha anguko la waimbaji. jamani ndugu zetu wametekwa, hatutakiwi kuwacheka maana tutakuwa wapumbavu, wala hatutakiwi kunyamaza maana tutakuwa wajinga, wala hatutakiwi kuwasema vibaya maana tutakosa busara, wala hatutakiwi kuwanung’unikia maana tutakosa hemika, lakini tunatakiwa tuwaombee, tena kwa Nguvu zote kama tulivyoombea mgomo wa madaktari ndani ya masaa 20 mgomo ukasitishwa. Shetani amewateka ndugu zetu, basi sisi tukiwa Askari wake Bwana Yesu, yatupasa kuingia kuvipiga vita hivi vikali. maombi yetu ni siraha kubwa.

Tutaomba kama ifuatavyo:-
(1) Tutaomba toba kwajili yao.
(2) Tutamkemea Shetani awatoke watu wanaowaendea waimbaji na kuwashawishi kushiriki machukizo mbele ya Bwana. Huyo shetani anyamaze kimya.
(3) Tutamkemea shetani anayewapelekea tamaa watumishi hawa, huyo shetani anyamaze kimya.
(4) Kisha tutamwomba Mungu ampeleke Roho wa Bwana awatawale waimbaji.

Hivyo basi popote pale ulipo Duniani pote, ukiwa wewe ni mtu wa Mungu, tafadhali omba sana kwajili ya waimbaji hawa, maana Mungu anakwenda kufanya kitu cha tofauti kwa waimbaji, msihi Mungu atulize ghadhabu yake juu yao, bali awaonee huruma watumishi wake, hata awape rehema. Bwana akubariki sana.

NEW HOPE MINISTRY – INFORMATION DESK.

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

3 Responses to TUWAOMBEE WAIMBAJI WA TANZANIA MAANA WAMETEKWA NA DUNIA NA SHETANI PIA.

  1. Meinrald says:

    Nafikiri tatizo ni malezi ya kiroho,mahali ninapo abudu tuna mwimbaji mmoja maarufu,ni mwezi mmoja sasa hayupo kanisa yupo busy na huduma, muda wa huduma hauna uwiano na Muda wa kuwa na Mungu.Kazi ya Mungu imewekwa mbele kuliko mwenye kazi mwenyewe.

    Like

  2. Mpoki mwaki wa baba Groly says:

    Mungu akabariki sana kiongozi kwa kuliona hilo,yangu machache,wengi wao waimbaji moja,wanamwimbia Mungu lkn hawaimbi na Mungu,kingine wengi wao huwa hawapewi baraka za baba zao wa kiroho wanakoabudu,na mara nyingi huwa hawapendi sana kujifunza neno na kuwa karibu na viongozi wao wa kiroho ili wajue kutunza moto wa madhabahu na kwenda nao wakimwimbia Mungu,hivyo wanatembea na kuishi chini ya laana ya viongozi wao wa kiroho.Huduma yoyote inapoonekana au kukua ukiwa chini ya kiongozi wako wa kiroho,ukaanza kujiendea unavyotaka bila ruhusa na kibari baraka za huyo kiongozi wako unatembea chini ya laana.Asante sana.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s