ROHO YA UVUMILIVU NA SUBIRA

                                   SOMO:ROHO YA UVUMILIVU  NA SUBIRA

Pastor M.A.Mtitu

Tunaishi katika nyakati ambazo  tabia ya  uvumilivu,subira ni changamoto kubwa,tunaishi maisha ambayo ni ya  mbio mbio,haraka haraka ,hakuna subira.Ulimwengu wetu wa kisasa wenye vitu na mambo ya kisasa ya haraka,mashine za haraka,huduma za haraka,vyakula vya haraka,usafiri wa haraka n.k. hii inafanya uvumilivu na subira kuwa hadimu kwa katika maisha yetu

Maandiko:                                                                                                                                  Wagalatia 5:23-22; Wakolosai 3:12-17.

Utangulizi:

Tunda la Roho ni Tabia ya kristo ndani yetu. kusudi la Mungu ni tufanane na Kristo. Ukomavu wetu wa kiroho unapimwa na tunda la roho: Msisitizo mkubwa leo katika kanisa  umekuwa katika Karama za roho Kuliko katika tabia,karama ni utendaji wa kristo ndani yetu, ni nguvu za kristo.tunahitaji uwiano wa vyote.kuwa na madhihirisho ya karama bila Tabia ya Kristo ni janga kubwa la kiroho.

1)      MAANA YA UVUMILIVU /SUBIRA: 

Uvumilivu ukoje,na unatendaje kazi?

Neno la kiyunani kwaajili ya uvumilivu ni makrothumia ambalo ni muunganiko wa maneno mawili. Makro  (long ) na-Thumos (- temper) “long-tempered”  ni knyume cha  neno “Short tempered.”Hasira iliyo mbali,isiyo ya haraka,uwezo wa kuzuia hasira,kutolipuka kwa hasira.Subira /uvumilivu  kuna husiana na kuwa na “Long fuse”,

 

a)      Ni uwezo wa kukaa nyuma na kusubiri matokeo yanayotarajiwa bila kuwa na hali ya wasiwasi ,kuhangaika, kufadhaika, au kukataa tamaa.

b)      Ni uwezo wa kuachia hitaji lako ambalo ungeweza kulilikidhi mara  au kulitimiza mara na kuwa tayari kusubiri.

c)       Ni tabia ambayo huonyesha kusthahimli wengine juu ya mawazo na fikra zao, pia kuonyesha huruma,kuwaelewa na kuwakubali wale walio taratibu,au wazito,polepple katika kukomaa kwao,na kuchukuliana na uwezo tofauti walionao wengine.

d)      Ni uwezo wa kubakia mtulivu katikati ya machafuko na ,misukosuko mbalimbali ya maisha kwa sababu unajua ya kwamba Mungu yupo anatawala mambo yote.

e)      Kuwa na uwezo wa kufyonza na kunyonya  maudhi,kero,masumbufu ya maisha bila kulipuka na hasira.Uvumilivu-makrothumia unafyonza mambo yana yokukasirisha, kuudhi,kusumbua na kukukera pasipo kukupoozesha wewe au kukudhoofisha. Ni kama  kuwa na “ shock absorbers”

Watu wenye uvumilivu nao pia wanakasirishishwa na kukerwa,kuudhiwa na mambo mbalimbali kama mtu mwingine yeyote.haamanishi uwe “door mate” kifutia miguu cha mlangoni.

Tofauti  ya watu wenye uvumilivu na wengine ni kwamba wanajua  wakati gani wa kusema,na  wakati  gani wa kulikablili jambo moja kwa moja.lakini mpaka wakati huo ufike, wana napo mahali pa kuweka kwanza yale yanayo wakasirisha,yanayo wa kera,  na kuwaudhi,bila ya kulipuka,bila ya kukosa kujitawala.”

2)      TABIA NA HISIA ZINAZOAMBATANA NA KUKOSA UVUMILIVU:

Mtu asiye na uvumilivu huonekanaje,yupo vipi,anatenda vipi?

a)      Kuwa mtu usiye na subira, kutoridhika,kufadhaishwa(upset) na kuwa na hasira juu yako mwenyewe na juu ya wengine kwa mambo mbalimbali hasa yasiyo ya msingi na madogo madogo. (makosa ya kibinadamu)

b)      Kuwa mtu   ambaye mara zote huna uwezo wa kujizuia na kulipuka kwa hasira mara kwa mara na kupelekea kuiharibu siku yako mwenyewe na  kuharibu siku  ya wengine-kuifanya siku yako kuwa mbaya na wengine pia.

c)      Kuwa mtu unaye haribu mahusiano na watu wengine,kirahisi iwe ni kanisani, ofisini,shuleni n.k. kwa kutaka mambo yaende vile tu unavyotaka wewe .                   

fahamu ukweli huu:  

“si mara zote katika maisha mambo yatakwenda vile wewe unavyotaka na kwa haraka wewe unayoitaka.”

3)      MATOKEO YA KUKOSA UVUMILI/SUBIRA

Hisia utakazo shughulika nazo utapokuwa huna uvumilivu:

a)      Kukasirishwa kwa kila kitu au na kila mtu

b)      Kufadhaishwa/kuhamakishwa na watu walio polepole au wazito katika kufanya mambo

c)       Kukata tama –kwa maisha kwa ujumla

d)      Kuwa na uchungu-kwamba wengine wana yale/vile wewe unavihitaj

e)      Wasiwasi-juu ya kila wakati katika siku

f)       Kujawa na fadhaa-kwasababu utataka kufanya zaidi

g)      Kuwa na mfadhaiko-wakati wote upo chini ya msukumo-

h)      Kuchanganyikiwa  kwamba wengine  hawafanyi vya kutosha

i)        Hasira za haraka,mara kwa mara.

4)      FAIDA ZA UVUMILIVU KATIKA MAISHA YETU:                                                                                 

  uvumilivu unaleta nini katika maisha yetu,kwanini tuutafute?una faida gani?

a)      Uvumilivu huleta Amani katika maisha yetu. Wagalatia5:22

b)      Uvumilivu hutusaidi kustahimili mambo magumu  Yakobo 5:7-11

c)       Uvumilivu huweka wazi kusudi la maisha yetu kwetu Zaburi 40:1 War. 8:25

d)      Uvumilivu hutusaidi kuendeleza mahusiano yatakayo dumu kwa muda mrefu. Zab.15:18

e)      Uvumilivu hushawishwi watu wengine pia .Mithali 25:15

f)       Uvumilivu ni sifa tunayohitaji ilikuweza kukabili hali ngumu .Yakobo 5:7-11

g)       

5)      JINSI GANI TUNAWEZA KUTENGENEZA NA KUKUZA UVUMILIVU NDANI YETU:

“UVUMILIVU si rahisi kwetu kwasababu chanzo chake si asili yetu ya mwili ,unatoka katika upendo wa Mungu,ukweli ni kwamba hatujazaliwa na uvumilivu.Upendo ndio ufunguo unaotupelekwa kwenyew uvumilivu,mahali pa kuanzia ni upendo ili kupata uvumili.”

 

a)      Kujijua na kujitambua wenyewe katika ufahamu wetu na mioyo yetu  na kuuona ugonjwa tulionao.kuliona tatizo ndani yetu na kulikubali.

b)      Kufahamu ya kwamba uvumilivu unaweza kuendelezwa na kukuzwa ndani yetu  na Roho wa Mungu pekee . (Wag 5:22-23),Huwezi kudhihirisha tabia ya Kristo kwa nguvu zako mwenyewe.  Ni Roho Mtakatifu peke yake aliye na nguvu za kufanya mabadiliko anayotaka kufanya Mungu katika maisha yetu. 

c)       Mungu hukuza  tunda la Roho katika  maisha yako kwa kukuruhusu upite katika  mazingira ambayo unajaribiwa  kutenda kinyume kabisa cha sifa ya tunda la Roho!  Kukua kwa tabia daima kunahusu uchaguzi, na majaribu hutoa nafasi hiyo.  Kwa mfano

 • Mungu hutufundisha upendo kwa watu wasiopendeka karibu yetu.  Haihitaji tabia kupenda watu wanaopendeka na pia wanaokupenda.
 • Mungu hutufundisha furaha halisi katikati ya huzuni tunapomgeukia. Raha (happiness) hutegemea mazingira ya nje, lakini furaha (joy) hutegemea uhusiano wako na Mungu.
 • Mungu hukuza amani halisi ndani yetu, siyo kwa kufanya mambo yatendeke kama tulivyopanga, lakini kwa kuruhusu nyakati za machafuko na vurugu. Mtu anaweza kuwa na amani akitazama machweo ya jua yanayopendeza au akistarehe mapumzikoni.  Tunajifunza amani halisi kwa kuchagua kumwamini Mungu katika mazingira ambayo tunajaribiwa kuhofu au kuogopa. 
 • Vivyo hivyo, uvumilivu unakuzwa katika mazingira ambayo tunalazimika kusubiri na tunajaribiwa kukasirika. Wakati mwingine ni watu wa familia yetu wenyewe watatumika kutengeneza uvumilivu ndani yetu,watu walio karibu ndani yetu na walio wapendwa wetu ndio hasa wata waujaribu na kuupima uvumilivu wetu..

 

Basi kwa kuwa mmekuwa kama wateule wa Mungu ,watakatifu wapendwao,jivikeni… uvumilivu”  Wakolosai 3: 12

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

4 Responses to ROHO YA UVUMILIVU NA SUBIRA

 1. Meimutie Ngigwana says:

  Mungu nijalie uvumilivu wa moyo

  Like

 2. Jumaa Kijazi says:

  Its More Proffessional, Psychological And Phylosophical Kinds Of Information.

  Like

 3. ahsante sana. Mungu awe nanyi.
  UVUMILIVU NI WA MUHIMU SANA HASA KATIKA DUNIA YA SASA ILIYOJAA KILA NAMNA YA CHANGAMOTO. MVUMILIVU HULA MBIVU

  http://jesusisalive2016.wordpress.com
  Lackson Tungaraza.
  Mtumishi wa Bwana.
  0764793105 whatsapp.

  Liked by 1 person

 4. ayoub ismail says:

  daah mm kwa upande wng, nadhani nimeshindwa kurejesha subira kwa sababu kila kukicha majukumu yana niandama kiasi cha kukosa amani kabisa.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s