Usiondoke Bethelem Yako!

Somo:Usiondoke Bethelemu yako.

Pastor Mtitu.

MAANDIKO:RUTH 1:1-7,19-21

Wazo kuu la somo: Kukaa katika Mapenzi ya Mungu  katika Mazingira na Hali zote

Utangulizi wa somo: Naomi na Mume Elimelek waebrania toka Bethelem ya Yuda,waliondoka Mahali waliposwa kuwa sawa na Mapenzi ya Mungu “Bethelemu” na kwenda “Moabu” Mahali ambapo Hapakuwa ni mapenzi ya Mungu kwao,mahali ambapo Mungu alikataza,matokeo yake Wakiwa Moabu ,Mume na watoto wakafa na Naomi akarudi Bethelem baada ya gharama Kubwa.

Watu wa Mungu hawana budi kudumu katika mapenzi ya Mungu bila kujali mazingira, hali au majaribu yanayowakabili.

KANUNI TATUZA KUTUSAIDIA KUDUMU KATIKA MAPENZI YA MUNGU KATIKA HALI NA MAZINGIRA AU MAJARIBU YANYOTUKABILI

 1. KANUNI YA 1# FAHAMU KWAMBA KUNA WAKATI MUNGU HURUHUSU TUPITE KATIKA HALI,MAZINGIRA NA  MAJARIBU MBALIMBALI: Ruthu 1:1
 • Bethelemu “Nyumba ya Mkate” kuna njaa na “hakuna makate”,kukosekana “mkate” katika nyumba ya mkate haimanishi  hiyo siyo nyumba ya mkate tena.
 • Kutoziona Baraka za Mungu kwa kipindi Fulani haimaanishi Mungu si wa Baraka tena,Mungu Anabaki kuwa Mungu wa Baraka ,hata kama wakati huo hatuzioni Baraka.
 • Nyakati za “Njaa” au Majaribu kwa watu wa  Mungu ni ukweli usiopingika,kuna wakati tutapitia katika nyakati hizo pamoja na kwamba tupo “Bethelemu”.
 • Kupita katika nyakati ngumu,majaribu n.k. haina maana ya kwamba Mungu ametuacha,au hatujali na kutupenda tena,au anatuadhibu.
 1. 2.       KANUNI YA # 2: FAHAMU KWAMBA HATUWEZI KUFANIKIWA NJE YA MAPENZI YA MUNGU NA NJE YA UHUSIANO WETU NAYE: Ruthu  1:2-5
 • Pamoja na kukimbia Bethelemu kwasababu ya Njaa na Kwenda Moabu bado Naomi na familia yake hawakufanikiwa,Mume na watoto wakafa ndani ya miaka kumi,akabaki mjane na mwenye Uchungu. Naomi= “Utamu” ukwa Uchungu.
 • Ni heri kubaki katika mapenzi ya Mungu hata kama “hakuna Mkate” kuna njaa kwa muda,kuliko kutoka katika mapenzi ya Mungu na kuupata shibe ambayo itagharimiu maisha yako” ni heri kufa “Bethelmu kuliko kuishi Moabu”
 • Napaswa kuzingatia kuwa katika mapenzi ya Mungu na uhusiano wangu na Mungu hata kama sioni Baraka au Mafanikio kwa wakati huo.Baraka na mafanikio kwa watu wa Mungu ni matokeo ya uhusiano wetu na Mungu na kukaa kwetu katika Mapenzi yake.
 • Baraka na mafanikio yanapaswa kutufuata  kadiri tunavyo tii mapenzi ya Mungu na kudumu katika uhusiano naye (Kumbukumbu 28 :1-4)

Gharama ya kutoka nje ya mapenzi ya Mungu na uhusiano naye ni kubwa sana kuilipa(Ruth 1:19-21)ni vema basi ,mafanikio au baraka zozote zinazotutoa katika mapenzi ya Mungu na kutupeleka mbali na naye katika uhusiano wetu lazima zihojiwe.

 • Ukomavu wa kiroho ni pamoja na uwezo wa kugundua  mambo yaliyokuja kwa “sura”  ya Baraka au mafanikio na kumbe yapo kwa lengo la kututoa katika mapenzi ya Mungu na uhusiano naye.
 1. KANUNI YA 3#; FAHAMU YA KWAMBA   MUNGU HUWAJILIA NA KUWATOKEA WATU WAKE WALIODUMU KATIKA MAPENZI YAKE NA KATIKA HUSIANO NAYE( Ruth1: 6-8,19-21)
 • Naomi “alisikia”Bwana amewajalia watu wake na kuwapa chakula,Bethelemu ,nyumba ya mkate inatoa “makate” tena.watu wa Mungu waliobaki katika Mapenzi ya Mungu Bethelemu,Hatimaye Mungu aliwatokea,aliwatembelea na kuwabariki.
 • Majaribu,mapito,hali na mazingira mbalimbali yanayotukabili ni ya “muda” kuna wakati wa Mungu kututembelea na kumaliza hali hizo, somo hapa ni kwamba “tukivumilia na kudumu katika mapenzi na katika mahali petu, ‘Bethelemu yetu’,Mungu hututokea,na Mungu akitutokea ushuhuda huwa dhahiri kwa wote.”
 • Kumbuka “Nyakati ngumu huwa hazidumu,bali watu wagumu(majasiri,wenye kuvumilia,wasio kata tamaa na kuvunjika moyo)Hudumu.”

HITIMISHO:

Huenda upo katika kipindi kigumu cha kujaribiwa,unapitia hali na mazingira magumu,kumbuka Mungu huwajilia watu wake ambao wamedumu katika mapenzi yake bila kujali hali na mazingira wanayo pitia hivyo,usiondoke Bethelemu yako,Baraka zako ziko hapo.

Huenda upo katika mazingira ambayo yanakufanya kujaribiwa kuyaacha mapenzi Fulani ya Mungu yaliyo wazi kwako,na kutaka kutorokea “Moabu”kumbuka kamwe huwezi kufanikiwa nje ya mapenzi ya Mungu,kwa kitambo kidogo utaona kama umefanikiwa ukweli ni kwamba utalipia gharama kubwa zaidi ya kuwa nje ya mapenzi ya Mungu na uhusiano naye.

Neema ya Mungu na iwe juu yako sasa unaposubiri  kutokewa na kutembelewa na Bwana ukiwa Bethelemu yako.

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s