TOKA NA UISHINDE HALI NGUMU INAYOKUKABILI:

JINSI YA KUISHINDA NA KUTOKA KATIKA HALI NGUMU INAYOKUKABILI:

2 Wafalme 7:3-10

By Pastor Mtitu M.A.jr

Tunajifunza kuhusuWakoma Wanne na jinsi walivyoweza kutoka katika hali ngumu iliyokuwa inawakabili,habari hii ni mafano wa maisha yetu ya kila siku tuna hali ngumu zinzaotukabili,kwa wakoma  wanne wao hali ngumu iliyokuwa inawakabili ilikuwa ni Njaa,kukosa chakula.Wewe hali ngumu inayokukabili inaweza kuwa ni ya kifedha,labda hali ngumu ya kibiashara,hali ngumu ya kifamilia,hali ngumu ya kimasomo,hali ngumu ya kiroho,hali ngumu ya kiafya,hali ngumu ya kimahusiano,hali ngumu ya kihuduma,au kwa mwingine ni hali ngumu ya ndoa,n.k.katika hali yoyote ngumu tunayopitia sasa Mungu anayo njia ya kututoa katika hali hiyo,wakomaa walitoka katika hali hiyo ikabaki historia,nasi tukijua kanuni za kimungu za kuzitumia katika hali yetu ngumu inatukabili,mambo yatabadilika na kubaki historia.

Kila mkristo anaweza kushinda na kutoka katika Hali ngumu inayomkabili kwa kufuata kanuni hizi:

·         KATAA  KUKATA TAMAA NA KUKUBALIANA NA HALI NGUMU UNAYO KABILIANA

Wakoma wanne Walikataa kukubaliana na hali mbaya iliyokuwa inawakabili,walikataa kukata tamaa.waliendelea kuhoji na kwa kujiuliza maswali juu ya hali yao.”kutafakari” (mst 3-4)

Kamwe,Usikubali kuridhika au kukata tamaa na hali inayokukabili hatakama inaonekana ni ngumu kiasi gani,uwe na mtazamo wa kwamba Kwa Mungu bado kuna ufumbuzi, bado kuna jibu,Uwe na mtazamo mzuri,mtazamo chanya juu ya hali ngumu unayokabiliana nayo.

·          TAFUTA NA KUANGALIA FURSA ZINAZOWEZA KUKUSAIDIA KUSHINDA NA KUTOKA KATIKA HALI HIYO NGUMU INAYOKUKABILI:

Wakomaa wanne Walitafuta na kuangalia wapi kuna fursa,nafsi,mlango wa  kuwasaidia kutoka katika hali ngumu iliyokuwa wanaikabili.(mst 4)

Tafuta wapi kuna fursa ya kukusaidia kutoka katika hali ngumu na mbaya inayokukabili,badala ya kukaa chini ,kulia,kulaumu,na kulalamika juu ya hali yako ngumu,tatizo au shida inayokukabili tafuta fursa ya kusaidia kupata ufumbuzi juu ya hali yako ngumu.

Wakoma wane waliangalia fursa ipo wapi katika maeneo matatu na iliwapasa kufanya uchaguzi sahihi,Hekima ni uwezo wa kufanya maamuzi na uchaguzi sahihi katika hali inayokukabili.

Usikae bila kufanya maamuzi,kufanikiwa au kushindwa kwetu kupo katika maamuzi na uchaguzi tunaoufanya na kuuchukua.uchaguzi wako na maamuzi yako ya leo ni ya muhimu sana kwa kwa hatimaya yako,kwa siku zako za mbele.

Wakati mwingine ilikuweza kutatua tatizo husika linalokukabili,itakulazima kufanya maamuzi magumu ya kujihatarisha,ndivyo walivyo fanya wenye ukomaa wane,maamuzi yao magumu yalikuwa ni kuchagua kwamba ni bora waende kwenye kambi ya adui maana ndiko mahali pekee ambako tumaini lilionekana,kwenye kambi ya adui walikuwa na fursa ya kufa au kupona,wakati pale walipokuwa nje ya lango la mji kulikuwa ni kufa tu ,hakukuwa na tumaini,kwenda mjini  pia ilikuwa ni kufa tu.

·         UWE TAYARI KUJIHATARISHA KUZICHUKUA FURSA ZA KIMUNGU AMBAZO NDANI YAKE UNAO KUNA MATUMAINI YA HALI NGUMU KUPATA UFUMBUZI

Wakomaa wanne Walikuwa tayari kujihatarisha  katika fursa iliyokuwa ina matumaini ndani yake.Katika kupata ufumbuzi wa hali ngumu zinazotukabili  ni lazima tuwe tayari kujihatarisha katika fursa zenye matumaini ndani yake. “wakati mwingine fursa zinazoonekana zinaweza kutusaidia  kutoka na kufanikiwa zina hatari ndani yake,lakini ndipo jibu letu lilipo.tukikwepa kujihatarisha tutapoteza fursa zenye matumaini ya kututoa katika hali zetu nguumu tunazopitia.”

       Katika kujihatarisha tunapaswa kujihatarisha kimahesabu,”calculated risk” siyo kujihatrisha “kichwa kichwa”,.wakomaa walipiga mahesabu na kuona kuna fursa ya kupona kwenye kambi ya washami,kule nafasi,na uwezekano wa kupona ulikuwa ni nusu kwa nusu,wakati uwezekano wa kupona pale walipo na mjini ulikuwa ni sifuri kabisa.Tunajifunza kwamba kabla ya kuchukua maamuzi makubwa yenye kujihatarisha ni lazima tuzingatie kufanya mahesabu kwanza,tusikurupuke,tuangalie faida na hasara tutazozipata kwa maamuzi yetu ni kwa ukubwa gani.tuangalie yatatufaidisha nini na kutugharimu nini,tujiulize maswali kabla magumu kabla ya kuchukua maamuzi, Pia tunahitaji macho ya kiroho kuzitambua fursa za kimungu zinazojitokeza. wakomaa wanne walijiuliza maswali magumu na kujijibu wenyewe,Pia tunajifunza kufanya maamuzi wenyewe,usitegemee mtu mwingine atakufanyia maamuzi ya maisha yako,pia ni muhimu kufanya maamuzi katika wakati muafaka,wakati mwingine tunafanya maamuzi tukiwa tumechelewa sana,na hali imezidi kuwa ngumu.kuna fursa hutokea mara moja na kashi hutoweka,tukichelewa na kuhairisha maamuzi fursa hazitusubiri sisi.

Tusipofanya maamuzi na uchaguzi wenyewe wa nini tufanye juu ya hali yetu,basi mazingira na watu wengine watatufanyia maamuzi,usisubili mazingira na hali inayokukabili ikufanyie maamuzi ya hatima yako,fanya maamuzi mwenyewe kabla mambo hayajaharibika kabisa.usikae hapo kwenye hali yako ngumu bila kufanya maamuzi kwa muda mrefu,muda haukusubiri,hali na mazingira havikusubiri,fursa hazikusubiri.ni vizuri kufanya maamuzi mara baada ya kufanya utafiti na kujiuliza maswali magumu kama wakoma walivyo fanya,baada ya kuchanganua fursa hizo tatu mara walifanya uamuzi.

Watu wengi tunahairisha kufanya maamuzi,hata baada ya kuona fursa zote na majibu tunayo kwa hofu ya kujihatarisha.uzoefu unaonyesha watu wengi ni waoga wakufanya maamuzi magumu ambayo ndani yake yana faida iliyochanganyika na hatari. Angalia faida usiangalie hatari,wakomaa wanne pamoja na hatari iliyokuwepo walichagua kuwa na mtazamo chanya  wa kuangalia faida. Uwe na mtazamo  tofauti ,wako watu ambao  katika miiba wao wanaona maua,wakati kuna watu katika maua wanaoona miiba.wengi katika fursa wanaona ugumu tu,na wengine katika ugumu wanaona fursa.wengine wanasema jambo hili  linawezekana lakini ni gumu,na wako wanao sema jambo hili ni gumu lakini linawezekana.

Wengine katika msitu wanaona jangwa na wako ambao katika jangwa wanaona msitu.hawa ukiwapa jangwa watageuza kuwa msitu na wale ukiwapa msitu watageuza kuwa jangwa.

Mtazamo wako juu ya ufumbuzi wa matatizo yako ni wa muhimu sana kuliko tatizo lenyewe.

Wakomaa walioona fursa katika kambi ya adui,na wakachangamkia kwenda huko,mtazamo wao kwanza ulikuwa ni kwamba watahifadhiwa na kuishi,kufa halikuwa jambo la kwanza waliloliona katika kambi ya adui,waliona kuishi na kuhifadhiwa .kile unachokiona katika fursa yako ya kutatua hali ngumu inayokukabili ni muhimu sana,unaona matumaini gani,?katika ugonjwa unaona uzima au mauti?katika biashara yako unaona nini hasara au faida?katika huduma yako unaona nini?katika familia yako unaona nini,mtazamo wako ni wa muhimu.

·         PIGA HATUA YA KWANZA YA IMANI YA KUIKABILI HALI YAKO NGUMU

Wakomaa wanne walitenda mara yale waliyo yaamua.wakomaa wanne hawakuhairisha utekelezaji wa maamuzi.mara baada ya kufanya maaumuzi ,ni vema kuyatekeleza mara hii ni siri ya kututoa katika hali ngumu.wakomaa waliamkaa mapema asubuhi kwenda kwenye kambi ya washami kama walivyo panga na kuamua.Hili lilikuwa ni tendo la Imani,Imani bila matendo imekufa.ni baada ya kuondoka kwa imani na kuanza kuelekea kwenye kambi ya washami ndipo na Mungu alipoingilia kati.Mungu alitenda muujiza .Mara nyingi Mungu anakuwa amesha andaa mazingira ya kutatua tatizo letu,ni sisi kuchukua hatua ya Kutoka kwa Imani .Siku zote hatua ya kwanza ni yetu sisi hutua zinazofuata ni za Bwana mwenyewe.

·         TARAJIA UINGILIAJI KATI WA KIMUNGU KATIKA HALI YAKO NGUMU

Njia za Mungu za kutatua hali yetu ngumu ni za muujiza,haielezeke,wala kuchunguzika ziko juu sana akili zetu haziwe kupambanua,kwa wakomaa wanne Mungu alitenda muujiza washami wakakimbia kwa kusikizishwa kishindo cha magari ya farasi,Tunajifunza Mungu ni Mungu mwenye uwezo wote,anaweza kutumia mtu yeyote Yule kuleta ufumbuzi wa tatizo letu,anaweza kutumia mazingira tusiyoyatarajia, jambo la muhimu ni kuamini kwamba Mungu anaweza kutenda muujizi katikati ya hali yetu ngumu,lakini,ni lazima tufanye sehemu yetu,wakoma walifanya sehemu yao,.Tukifanya sehemu yetu,Mungu atafanya sehemu yake,naye hufanya zaidi yavile tunavyoweza kuomba,kuwaza,au kufikiri.

·         UWE NA MOYO NA DHAMIRA YA KUWA BARIKI WENGI UTAPO ISHINDA NA KUTOKA KATIKA HALI YAKO NGUMU

Wakoma wanne hawakuwa wabinafsi,ingawa wao walikuwa wanatengwa na kukataliwa kutokana na hali yao ya ugonjwa na kukaa nje ya lango la mji,lakini walipopata Baraka walikuwa radhi kuwashirikisha wengine.walijua kuwa ikiwa watajibariki wenyewe tu,madhara yatawakuta. ,Mungu huangalia mioyo yetu maana anatujua ndani nje,kama ni watu wabinafsi wenye kujijali wenyewe na kujipenda ni vigumu kutubariki,maana anataka akitubariki  nasi tufanyike Baraka kwa wengine,wakomaa wanne walipofanikiwa kutoka katika hali yao ngumu walishirikisha Baraka kwa wengine.wako watu leo wakibarikiwa au kufanikiwa kutoka katika hali ngumu walizokuwa nao wanawasahu wengine walio katika hali ngumu kama walizokuwa nazo,wana sahau walikotoka,Mungu hapendi hali hiyo.wako watu wakibarikiwa kidogo leo au kufanikiwa katika mambo yao wanageuka kuwa karaha na kero na makwazo kwa wengine, wanajisifu,wanajigamba na wana kosa unyenyekevu,wanasahau kuwa ni Mungu amewafikisha hapo walipo na sio uwezo wao au nguvu zao,wanawadharau wengine wasio  na Baraka zile walizonazo wao,

Tukifanikiwa kutoka katika hali zetu ngumu tukumbuke kuwabariki wengi walio katika hali ngumu ,Mungu akiuona moyo huu na nia hii ndani yetu atahusika kutupa mpenyo wa kutoka katika hali ngumu tuliyonayo maana anajua tutafanyika Baraka kwa wengine,

Hitimisho

·         Je,ni hali gani ngumu unayopitia na kukabiliana nayo sasa?Je,umeamua kukubaliana nayo?je,umekataa tama na kuona basi hakuna la kufanya?kumbuka wakomaa wanne hawakukatatamaa na walikataa kukubaliana na hali yao ngumu,Hebu kamwe usikubaliane na hali hiyo,wala mawazo yanaokuambia kwamba Hali yako haina ufumbuzi,kwa Mungu Haijarishi tatizo ni kubwa kiasi gani,hali ni ngumu kiasi gani,kwake yote yanawezekana na yana majibu.

·         Zipo fursa za kutoka katika hali hiyo ngumu inayokukabili,kwanini usimwombe Mungu akuonyeshe fursa,mlango ,namna ya kutoka,?omba akupe ufunuo,wazo la ufumbuzi wa tatizo lako,wazo moja tu la kimungu linaweza kubadili hali yako na ikabaki historia.

·         Pengine unahitaji kufanya maamuzi na uchaguzi sahihi ambao utakutoa katika hali yako hiyo,Pengine unahitaji kufanya maamuzi magumu ya maisha yako,usiogope,uwetayari kujihatarisha,maamuzi yako na uchaguzi wako wa leo vimebeba hatima ya maisha yako,vimebeba ufumbuzi wa hali yako.

·         Pengine unahitaji kufanya maamuzi ya kumpokea Kristo kama Bwana na Mwokozi wa  Maisha yako,huu ni uamuzi utakao athiri hatimaya yako ya milele,ni uamuzi mkubwa kuliko wote uliowahi kufanya na utakao kuja kufanya katika maisha yako,Hali yako ngumu ya Kiroho itabadilika na utaanza maisha mapya .

·         Pengine unashindana na kutekeleza maamuzi ambayo umesha yachukua,hebu chukua hatua ya Imani leo,Mungu anasubiri ufanye sehemu yako naye amalizie sehemu yake.pasipo matendo Imani imekufa,huwezi kumpemdeza Mungu,ni wapi unahitaji kuchukua hatua ya Imani?Kwanini usifanye hivyo sasa?

·         Tarajia Muujiza wa Mungu katika Hali yako ngumu,hakuna gumu la kumshinda,haijalishi nini unapitia,kwa wala kwa muda gani umekuwa katika hali hii,ukitarajia Muujiza wa Mungu,yeye aweza kubadilisha hali hiyo,aweza kumtumia mtu yeyote,aweza kukutumia malaika,aweza kukuponya kwa muujiza,aweza kutumia mazingira yeyote!

·         Kumbuka Mungu anaangalia moyo wako,tena anakujua ndani nje,Je,Moyo wako ukoje,nia yako iko je,Mungu anatafuta mtu ambaye atapo mtoa katika hali ngumu atawakumbuka wengine,atapo barikiwa atawabariki wengine,atapoinuiliwa .atawainua wengine,Mungu Anatufuta mtu asiye na ubinafsi,asiyejipenda na kujijali yeye tu ,mtu ambaye atakuwa mnyenyekevu atapo barikiwa na kufanikiwa,Mungu anaunagalia moyo wa jinsi hiyo na yupo tayari kuinigilia kati sasa katika hali yako ngumu kama atauona moyo huu kwako.

Muombe Mungu akusaidie katika haya yote,Amen

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

3 Responses to TOKA NA UISHINDE HALI NGUMU INAYOKUKABILI:

 1. Anthony Mwenda says:

  Asante sana inabariki sana

  Like

 2. pastormtitu says:

  Asante,ubarikiwe .

  Like

 3. Peter says:

  Ndugu wapendwa katika Bwana,
  Napenda kuwajurisha kuwa usiku wa juma mosi kaka yetu marehem GREGORY PROTACE alimtokea mdogo wake DEOGRATIAS PROTACE na
  Kumuuliza kwanini walimuua? Huyu DEOGRATIS ndiye mwenye mke anayesadikiwa kumuua kaka yetu GREGORY.Tafadhari sana ninawaomba mzidi kuomba ili kumkomboa kaka yetu mpendwa.Ahadi yangu baada ya kumkomboa kaka kutoka mikononi mwa shetani ni kuokoka mimi na familia yangu yote na familia ya kaka yetu. Ninawaomba mnisaidie.

  Ishengoma.

  —–Original Message—–
  From: Ishengoma, Peter [ICG-GTS NE]
  Sent: Friday, March 02, 2012 3:35 PM
  To: ‘prayer@ufufuonauzimaministries.org’
  Subject: THE DEATH OF MY ELDER BROTHER GREGORY PROTACE

  Dear Ufufuo na Uzima Ministries (GCTC) or (Majeshi ya Ufufuo)

  It is with much feeling that I received a bad news of my sad loss, My Elder brother GREGORY PROTACE NIWAGIRA he has passed away on Friday January 13,2011 at Rubya Hospital Muleba Kagera Region after short sickness .

  The burial of our beloved elder brother was taken place on Sunday January 15, 2012. at Buyera village.
  It is truly an irreparable loss. I feel the blank so much. I can yet hardly believe it is true. I have indeed been comforted by the knowledge that all was done for the best by the Divine wisdom . I know that God will relief my pain for is the Merciful One.
  Kindly assist to return him alive so that he may live a victorious life. Glory be to God. I desire to see the Holy Spirit’s miracle-working power.

  Thanks and Best Regards

  Ishengoma.

  Regards
  Peter Ishengoma.
  Cell. 0717 658610 / 0788 658610 / 0757 315899

  —–Original Message—–
  From: Ishengoma, Peter [ICG-GTS NE]
  Sent: Monday, February 27, 2012 3:04 PM
  To: ‘info@ufufuonauzimaministries.org’
  Subject: KIFO CHA KAKA YANGU GREGORY PROTACE

  Mchungaji Joseph Gwajima,

  Ninakuomba sana utumie uwezo na karama ulizopewa na mwenyezi Mungu umurudishe kaka yangu GREGORY PROTACE aliyefariki
  Tarehe 13/01/2012 katika Hospital ya Rubya Muleba Kagera na kuzikwa kataka kitongoji cha Buyera mnamo tarehe 15/01/2012.
  Kifo chake ni cha utata mtupu hadi kusababisha nyumba tatu za watu wanaosadikiwa kuwa wachawi kuchomwa moto na mmoja wapo
  Kufariki.

  Ninakuomba sana utusaidie.

  Peter.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s