Mgomo wa Madaktari nchini Tanzania warejea tena, Waziri mkuu asema waziri wa afya na naibu wake hawang’olewi!

Wakati mambo ya madaktari yalipokuwa yakionekana kupata muafaka, hali imekuwa tete tena Nchini Tanzania, Mgomo umeanza upya tena huku madaktari wakisema hawako tayari kuendelea na huduma mpaka waziri wa Afya na Naibu wake wang’olewe madarakani. Wakati hayo yakiendelea, waziri mkuu upande wa serikali Mh. Mizengo kayanza Peter Pinda amefumbua kinywa juu ya hilo. Waziri mkuu ameonyesha uwazi wake kwamba mawaziri hawa hawataondolewa madarakani. Pinda alisema Serikali haioni sababu ya kuwawajibisha mawaziri hao kwa sasa na kueleza kushangazwa kwake na hatua ya madaktari hao kugeuza suala hilo kuwa dai namba moja hivi sasa.

“Hivi kweli mnataka nifike mahali nimwaambie Rais (Jakaya Kikwete) tunakupa saa 72 uwafukuze kazi viongozi hao? Hapana… hapana… hapana. kwa lipi hasa? Siwezi kumwambia atekeleze hayo. Ingekuwa hatujafanya chochote sawa, hata angekuwa mtu yeyote hawezi kukubalina na hayo vinginevyo wenzetu madaktari watuambie wana hoja nyingine.

Ni jambo la kushangaza sana kama serikali haioni umuhimu wa wananchi wake. mimi sidhani kama kweli mawaziri hawa hawana makosa, yamkini yapo makosa yao, serikali inatakiwa iwaulize madaktari kwanini wanawataka hawa viongozi waondolewe. serikali kwa mara nyingi imekuwa ikitumia mabavu katika kuendesha shughuli za kijamii, wakati huo ikitumia siasa kufunika maovu ya viongozi. Jamani Serikali hebu sikieni vilio vya wananchi, hata kama hawa viongozi hawana makosa basi waondoeni, maana madhara ya kuondolewa kwao si makubwa kama madhara yatakayojitokeza baada ya kuwaacha waendelee kukaa madarakani. maana wananchi watakufa, taifa litapoteza nguvu kazi. mimi naomba hawa viongozi muwaondoe ili kumaliza mzozo.

Zaidi sana watu wa Mungu nawaomba tuungane pamoja kuliombea tena jambo hili, pia kuiombea Tanzania. Tanzania ni taifa lisilomjua Mungu, maana serikali yake haikubaliani na mambo ya Mungu, kwa hiyo hii nchi hapo chini ya uangalizi wa Mungu na ndio maana utaona mambo kama haya yakijitokeza. serikali imekuwa na viongozi vipofu wa kiroho, hivyo tunaomba tuwaombee viongozi wa nchi yetu. Pia tumwombe Mungu ili aikumbuke nchi hii.

Bwana aisaddie Tanzania katika Jina la yesu. Amina

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

One Response to Mgomo wa Madaktari nchini Tanzania warejea tena, Waziri mkuu asema waziri wa afya na naibu wake hawang’olewi!

 1. Frederick Marandu says:

  BWANA YESU ASIFIWE!Kwa kweli nchi inahitaji maombi sana sana! Ukiangalia nchi nyingi zilizo anza na migomo mfululizo mwishowe waliishia kwenye kuwatoa maraisi wao na vita mauaji mengi yalifwatia dalili ya mvua ni mawingu!hizi ni dalili mbaya ktk ulimwengu wa Roho hakuko salama!Hii sasa ni Roho ya migomo inatafuta mahala itende kazi kama hii inafwatiwa na Roho ya mauti iko kinywa wazi kumeza idadikubwa ya watu kupitia miundo mbinu ya migomo,Tulikatazwa tusiuwe lakini bila kujua watu tunauwana kupitia vitu kama hivi serekali + kutolipa mahitaji ya madakari+migimo ya madaktari = kuuwa watu je ktk hukumu siku ikifika hawatakuwepo watu watakao takiwa kujibu(kutoa hesabu juu ya hili kweli?!)Nina hakika wapo ktk madactari ambao ni watumishi wa mungu na washetani lazima wapo na pia ktk serikali najua lazima wapo watumishi wa MUNGU na wa shetani sasa isije ikawa hapa panatumika pia ili watu wafe (kafara itimie) kwa manufaa ya shetani!na nivizuri hata serikali na Raisi wake wasiwe wakuchukua mda mrefusana kutoa jibu la mabo kama vile samaki wa magufuli walivyochukua muda mrefu hadi mhusika amehamia eneolingine na meli ya wezi wa samaki imechoka ndio kesi imekwisha hebu viongozi jengeni namana ya kupenda kupata ushauri kwa watumishi wa MUNGU mtapata muongozo wa MUNGU lakini bila hivyo mtatumiwa na shetani ktk uongozi wenu mtaongoza kwa idadi kubwa ya vifo vya watu bila hatia,Kumbe mmekosa hekima ktk kuongoza na hekima sahihi hutoka kwa MUNGU tu!Sio mkapige ramli na mkaulize kwa wanajimu wa shetani!matokeo yake ndio haya!
  Mbarikiwe mtakapo anza kupata ushauri wa watumishi wa MUNGU aliye hai.
  AMEN!
  frederick Marandu

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s