UFUGE ULIMI WAKO NA KUUTAWALA !

SOMO:KUUFUGA ULIMI NA KUUTAWALA

YAKOBO 3:1-12

NA: M.A.MTITU

UTANGULIZI                                                                                                                          Ulimi ni kiungo kidogo muhimu sana kinachotuwezesha kuongea,kutamka maneno,Utatumia 1/5 ya maisha yako kuzungumza tu.mazungumzo yako ya mwaka mzima yanaweza kujaa vitabu 66 vyenye kurasa 800.Idadi ya maneno yanayozungumzwa kwa siku na  wanaume ni kati ya17,000-20,000 na  kwa wanawake  ni kati ya maneno25,000-30,000 hii ni kutoka utafiti uliofanywa  na CNN Marekani.                                                                                                                                   MAANDIKO:

YAKOBO 1:19,26  MITHALI 21:23

YAKOBO 3:1-13 Dhambi ngumu kabisa ni kuufuga ulimi,ina hitaji ukomavu wa kiroho, “ukamilifu” Hapa haimaanishi kutokuwa na dhambi .Kiyunani lina maana ya “mature,health Person”-Ukomavu,kupevuka,Kuna Mambo sita ambayo ulimi umefananishwa nayo katika lugha ya picha  “ metaphor” ili kutupa kuuelewa Ulimi,kila mambo mawili yana beba somo moja kuhusu ulimi.mambo haya ni

1.      Usukani

2.      Lijamu

3.      Moto

4.      Mnyama mkali asiyefugika

5.      Chemichemi

6.      Mti wa matunda.

A.    KWANINI NAPASWA KUWA MAKINI NA ULIMI WANGU?

1.      ULIMI WANGU UNATAWALA NA KUONGOZA WAPI NIENDE:

Kielelezo cha usukani na lijamu.Ukitaka kujua utakuwa wapi au vipi miaka mitano ijayo akangalia nini unazungumza zaidi leo juu yako mwenyewe,maneno yetu yana tupa uelekeo wa kule tuendako.unaongea juu ya nini zaidi?.

“ulimi unatawala mwelekeo wa maisha yako.ulimi ni usukani wa maisha yako,ni mfumo wako wa uongozi wa maisha yako Ukitaka kumbadilisha mtu anvyoamini,mbadilishe vile anavyo zungumza,vile unavyozungumza mwisho wa siku nindivyo vile unavyoamini.”

yale unayo yazungumza sana,mara kwa mara mwisho wa siku ndivyo utakayo yaamini. wazo  Huiingia katika ufahamu,kasha katika MOYO,MANENO hutoka moyoni na kasha MATENDO  huzaliwa.(MITHALI 18:20)

Nukuu: Martin LUTHER-“huwezi kuzui ndege wasiruke juu ya kichwa chako,lakini unaweza kuzuia wasijenge kiota na kuhamia hapo

2.      ULIMI WANGU UNAWEZA KULETA UHARIBIFU NA MADHARA KWANGU NA KWA WENGINE

Kielelezo cha moto na mnyama mkali asiyefugika.Mithali 21:23 18:21 Madhara makubwa sana yameletwa na ulimi,ndoa zimevunjika, urafiki,mahusiano,makanisa ,ndugu,wamekosana  n.k ulimi unasabisha magovi,chuki n.k ULIMI unadhuru unaitwa mishale…una dhuru hata mbali.Neno moja liweza kusababisha “chain reaction”unaweza kuzungumza kitu ambacho hudhamiria kilete madhara lakini matokeo yake makubwa yasiyozuilika.

3.      ULIMI WANGU UNA NIDHIHIRISHA  VILE MIMI NILIVYO

Kielelezo cha chemchemi namti wa matundaYAKOBO 3:9-12Watu wengi wanafikiri labda kukaa kimya pekee yake kunasaidi,cha muhimu zaidi ni ndani yako kukukojeMfano wa kisima/chemichemi  na mfano wa mti na matunda-Kile kilichopo katika kisima ndicho kitakacho toka na kuwepo katika maji,kadharika kilichopo katika mti kitajidhihirisha kwa njia ya matunda.

Kanuni:                                                                                                                                    Kinachotoka katika kisima ndicho kilichomo ndani yake,kina chozaliwa  na mti ndichi kilichopo ndani ya mti. Maneno yangu ni matokeo ya hali ya moyo wangu.nina weza kujificha na kuwapubaza watu kwa muda  hatimaye maneno yangu hunisaliti na kunitambulisha mimi ni niko vipi.

maneno yanafunua kilichomo ndani yetu,kukaa kimya bila kupona ndani haisaidii   MATHAYO 12:34

Kama una tatizo na ulimi ujue unatatizo kubwa moyoni kuliko unavyofikiria.

·         Mtu mwenye maneno makali ana moyo wenye hasira.

·         Mtu mwenye maneno hasi ana moyo wa woga na hofu.

·         Mtu mwenye ulimi /maneno ya kulipuka ana moyo ambao haujatulia.

·         Mtu mwenye maneno ya kujivuna na kujisifia ana moyo usiojiaamini,hana usalama wa moyoni.

·         Mtu mwenye maneno ya kutukana ana moyo usio safi

·         Mtu ambaye wakati wote ni mkosoaji na wa kulaumu ana moyo wa uchungu

. lakini upande wa pili,mtu mwenye kutia moyo siku zote ana moyo wa furaha.mtu anazungumza kwa upole ana moyo wa upendo,anayezungumza ukweli ana moyo wa uaminifu.

 

 

 

B.     JINSI YA KUKUFANYA ILI NIWEZE KUUTAWALA NA KUUCHUNGA ULIMI WANGU:

1.      PATA MOYO MPYA  Ezekeli 18:31, zaburi 51

2.      OMBA MSAADA WA MUNGU KILA SIKU                                                                    Zaburi 141:3 huwezi kwa nguvu zako unahitaji msaada wa Mungu

JIFUNZA NIDHAMU YA KUSIKILIZA.

Ufikiri kabla ya kusema-jifunze nidhamu ya kusikiliza  Yakobo1:19 ,Kusikiliza kutakufanya kuwa na maneno machache.Ukiwa mwepesi kusikiliza hautakuwa mwepesi kusema, kusukiliza ni sanaa,ni jambo la kujifunza ni kazi sana, mfano katika maongezi ya simu,kuiingilia kati mwingine anapozungumza,kumkata kauri mtu mwingine,kutaka kutawala mazungumzo pekee yako,n.k.

Kusikiliza listening ni tofauti na kusikia hearing,unaweza kuwa unasikia lakini husikilizi,

kusikiliza ni ngazi ya juu ya mawasiliano inayo husisha, macho, masikio,mwitikio wamwili,lugha ya mwili,hisia za mwili-ni katika kusikiliza unaweza kumjua mtu zaidi,na kuusoma moyo wake,ana uchungu kiasi gani,ameumia kiasi gani,n.k.

 

Tunauweza wa kusikiliza maneno 600 kwa dakika,wakati tunauwezo wa kusema maneno 150 tu kwa dakika,tofauti ya maneno 500,tunafikiria haraka kabla ya mtu hajamaliza kusema tayari tunamaliza naye sentence,Inahitaji Nidhamu.

“Maneno yetu yana nafasi kidogo sana katika mawasiliano na kufikisha ujumbe,mawasiliano ni zaidi ya kuzungumza maneno.utafit wa Kodak uligundua hili –Nusu ya mawasiliano yetu ni ujumbe usio wa maneno yeyote,kutazama ,lugha ya mwili kunachukua 58% ya kuwakilisha ujumbe,sauti yetu na namna tunavyo sema 35%,maneno yenyewe hasa ni7% ya ujumbe wote.hii ni kusema maneno au kuzungumza hakuna nafasi kubwa katika mawaasiliano tofauti na tunavyofikiria na kuamini.”

 

 

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

One Response to UFUGE ULIMI WAKO NA KUUTAWALA !

  1. Jackson lukala says:

    Nimependa somo nilikua sijapata ufunuo kama huo kuhusu ulimi.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s