Ujumbe : MADHABAHU Na. Mch. Josephat Gwajima.. Tar. 8 April, 2012 ..

Na Mch. Kiongozi : Josephat Gwajima

Leo tunaendelea na somo la madhabahu, kwa ufupi tulisema kuwa tunapozungumzia madhabahu kimsingi tunazungumzia vitu vitano.. yaani kuhani wa madhabahu , Mungu wa madhabahu , Nguvu ya madhabahu ( moto wa madhabahu) , kafara ya madhabahu na madhabahu yenyewe .. na kwa leo tujikite zaidi kwenye neno hili kafara ya madhabahu

KAFARA YA MADHABAHU

Nini maana ya kafara?

Kwa akili zawatu zilivyo wakisikia neon kafala wanakimbilia kwenye waganga wa kienyeji.. lakini neno hili kafara kwenye biblia ndio linaitwa dhabihu kwenye biblia.. kuna maadiko kadhaa yanayo taja kafara kwenye biblia kama ifuatavyo :- mambo ya walawi 2 :2, 9, 16; mambo ya walawi 10 : 13, 14.. maandiko haya yanataja neon kafara kwenye biblia .. na limeonekana mara nyingi.. hii ni kukuonyesha kuwa neno kafala lipo kwenye biblia na lina maana sahihi.. kwahiyo Kafara ni sadaka inayotolewa kwa ajili ya kupokea jambo fulani kutoka ulimwengu wa roho aidha kwa Mungu au kwa shetani..

Ni Muhimu kujua matatizo mengi ya watu yanasababishwa na kafara zinazotolewa.. .. na shetani amewafunga watu wasijue vyanzo vya matatizo yao na kufungwa huku ndio biblia anaita “mafumbo ya kishetani” Ufunuo 2: 24-25 na kwa namna hii shetani amewapofusha watu wasijue siri hii ndio maana hata baadhi ya wakristo wamefungwa wasijue siri hii..

Kwa desturi watu hupanda ngazi kwenye maisha kulingana na sifa zao na haki, lakini watu wengine kwa kutumia njia ya mkato wanatoa kafara ili kuwa funika wengine na kuchukua nafasi zao.. Yeremia 32 :35 1wafalme 16 : 34 tunaona hapa kwenye hili andiko, maana Joshua alipoubomoa ukuta wa Yeriko akaweka kanuni nya kuwa yeyote atakaye taka kujenga atafiwa na mwanaye pale atakapo anza na atakapo fika katikati atafiwa na motto mwingine … lakini tunaona Hieli mbethel akaamua kumtoa kafara mwanaye kwa kuweka misingi na tena akamtoa kafara mwanaye mwingine..

Tunaona hapa kuwa kafara na kutoa kafara hayakuanza leo bali yalianza tangu kipindi cha cha zamani kwenye biblia.. 2 wafalme 3:24-27 hapa tunaona wayahudi wakavamia Moabu na wakakaribia kuteka mji wa Moabu na hapa ndio maandiko yaasema ndipo alipomtoa mwanaye ambaye angekuwa ni mtawala badala yake kwenye ukuta ili wayahudi wasiweze kuwavamia..

Ndio maana ni rahisi kumkuta mtu anasikitika kuhusu matatizo yake., lakini ni Muhimu kujua watu wa duniani hutoa kafala ili apate ushindi katika maisha na kwa njia hii hufunika wengine.. ndio maana kuna aina ya mashetani yanaitwa mizimu hawa sio roho za watu waliokufa bali ni mashetani waliokaa muda wa kutosha nafamilia hadi wakajua tabia zenu na pale mtu anapoenda kutoa kafara anakuwa anayaalika yale mapepo nyumbani au kwenye ukoo husika.. na ndio maana ni rahisi kukuta ukoo mmoja kuwa na matatizo yanayo fanana..

Kimsingi waganga wa kienyeji hutumia kafala kuwafunga watu, na ndio maana ukienda kwa mganga atakutaka ulete kafara aidha ya kuku au ya mbuzi kwa maana kwa mganga wa kienyeji ni madhabahuni pa shetani… na wachawi pale ile damu inapomwagika mashetani anamiminika pale na kufanya vile kafara inavyowataka wafanye.

Ndugu zangu kuna watu hata hawapendi kukuona unakula vizuri, au unapika vizuri au unasomesha.. na akiona huo wivu anaamua kwenda kukufanyizia kwa mganga wa kienyeji..ambapo ataambiwa atoe kafara kwa ajili ya kukuangamiza wewe..

21wakorintho 10:20 .. zaburi 126:38 kumbe kuna uwezekano wa watu kutoa kafara kwa mashetani. Na biblia inalikubali hili kupitia maandiko hayo tuliyoyaona hapo.. unaweza kuwekewa pepo la udhaifu kupitia kafara.. Luka 13:10 Pepo wa udhaifu.. mtu anaweza kukutolea kafara ili ufe kifo cha Ghafla..

Kwetu tuliookoka..

Unapomkubali Yesu unakuwa umejiunganisha na mauti ya Yesu hivyo hakuna haja ya kutoa kafara tena.. maana Yesu alifanyika kafara kwa ajili yetu na damu ya Yesu ilimwagika ili kutufungua wote na Yesu alipigwa na kufa ili sisi kutookoa kama kafara kwaajili yetu.. watu wa dunia wanaweza kwenda kwa waganga na kutoa kafara lakini sisi tuna Damu ya Yesu ambayo ni nguvu ya madhabahu yetu..

Hivyo sasa kwa kutumia damu ya Yesu unaweza sasa kuharibu kafara na madhabahu zao zote,, ukishughulikia madhabahu na kafara unakuwa umeiangamiza nguvu ya madhabahu nza kishetani na tatizo ulilonalo litakwisha .. kwahiyo ni muhimu kuharibu makuhani wa madhabahu yaani wachawi na waganga, madhabahu yenyewe yaani wanapokusanyikia, inatubidi kubomoa kafara yao, nguvu yao na pia Mungu wa madhabahu zao ambazo ni shatani.. na hapo utapata ushindi mkamilifu..

Mathayo 17:14 utajiuliza inakuaje, Yesu anaamua kumtoa pepo wakati tatizo lake lilitajwa ni kifafa, hapo utagundua kuwa matatizo ya watu wengi yanatoka na mapepo au majini yanayo tumwa na kumfanya awe vile alivyo.. lakini unatakiwa ushughulikie madhabahu na mambo yanayofuatana nayo…

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

7 Responses to Ujumbe : MADHABAHU Na. Mch. Josephat Gwajima.. Tar. 8 April, 2012 ..

  1. hosea hezron says:

    ujumbe mzuri, juhudi zako ni kubwa. Ubarikiwr

    Like

  2. hosea hezron says:

    nice

    Like

  3. Your message is enormous.
    May God Be With You

    Like

  4. Meshack yusuph says:

    lazima kazi zao ziharibike,kwa Madhabahu zote kuvunjwa kwa damu ya Yesu:maana tumepewa kushinda mno

    Like

  5. joely maira says:

    Nimebarikiwa sana na somo Baba,unatisha kama nini duniani.!!!!

    Like

  6. Pst. Livingston Mbaru says:

    Great work Man of God. God bless you abundantly.

    Like

  7. John Kifaru says:

    Somo zuri sana mungu aku bariki.

    Like

Leave a comment