ITAFUTE PENUELI YA MAISHA YAKO

PENUELI- “MAHALI PA KUKUTANA NA KUGUSWA NA MUNGU WAKO

NA PASTOR -TEACHER M.A.MTITU 

UTANGULIZI:                                                                             Je,kuna wakati katika maisha yako umefikia mahali pa kuona umefika mwisho,huna nguvu tena,huna matumaini tena na una hofu juu ya Hali ngumu inayokukabili? Yakobo Kabla hajafika mahali ambapo hatimaye alipaita Penueli alikuwa amefika mwisho, mwisho wa uwezo wake wa kulaghai, mwisho wa kudanganya, alikuwa anakabiliwa na kukutana uso kwa uso na Adui wa Maisha yake kwa miaka yapata 20 aliyeapa kumuua huyu ni Esau nduguyake(MWANZO 27:41) .

Yakobo alikuwa ameishiwa mbinu,hakuwa na mahali pa kumkimbilia isipokuwa kwa Mungu tu,na ndipo alipokutana na Penueli yake. Huu ulikuwa ni wakati muhimu wa maisha yake ,hakukubali kumwacha Mungu aende mpaka “amebarikiwa”.Katika Maisha yetu kunawakati tunafika mwisho na tunahitaji Kutokewa na kuguswa na Mungu tu. “Kuna mahali tunafika katika kutembea kwetu na Mungu ambapo Mafanikio yetu,fedha yetu,maarifa yetu,umaarufu wetu,utajiri wetu haviwezi kutusaidia tena,tunahitaji Kukutana na Mungu uso kwa uso na atuguse maisha yetu”

ANDIKO LA MSINGI: MWANZO 32:24-31

Kupata mguso wa Mungu katika maishayetu kuna gharama lakini una matokeo makubwa katika maisha yetu,Yakobo alilipa gharama ya kukaa pekee yake, kukesha usiku kucha,kutenguliwa mguu,na kuchechemea maisha yake yote. Hakuna mtu ambaye atakutana na uso wa Mungu na kuguswa naye akabaki vile alivyo,lazima kutakuwa na tofauti dhahiri itakayo onekana katika maisha yake.mambo yafuatayo yatakuwa dhahiri katika maisha yetu tukiipata Penuel yetu:

1. MGUSO WA MUNGU WA PANUELI HUTUPA NGUVU YA KUMKABILI ESAU WA MAISHA YETU:

MWANZO 33:1-15, Kabla ya Kuguswa na Mungu pale Penueli,Yakobo alikuwa na hofu kuu juu ya Esau,hakuwa na ujasiri wa kumkabili ,ni baada ya kutoka Penueli ndipo alipomkabili Esau,ambaye alimkimbia kwa miaka 20! Mguso wa Mungu katika moyo wetu unatuwezesha kumkabili “Esau” wa maisha yetu.mambo yanayotupa hofu na kututisha ndani yetu tunaweza kuyakabili tu baada ya kutoka Penueli tukiwa tumeguswa na Mungu. Adui zetu hawawi adui zetu tena wanakuwa rasilimali zetu bila sisi kuhitaji kufanya hila au ujanja,tuliowatafsiri na kuwaona kama maadui wanakuwa marafiki. haijalishi ukubwa wa tatizo lako au muda wa tatizo lako,limekutisha na kukupa hofu kiasi gani,ukitoka kuguswa na Mungu tatizo hilo litayeyuka kirahisi sana mbele yako!

2. MGUSO WA MUNGU WA PANUELI HUBADILISHA HISTORIA MBAYA YA MAISHA YETU: MWANZO 32:27-28) Jina la “YAKOBO” lilibeba historia ya zamani ya maisha yake,historia ya maisha yake ilijaa udanganyifu,kama jina lake lilivyo maanisha,jina lake liendana na tabia yake,alimdanganya na Kumrubuni Esau haki ya uzaliwa wa Kwanza,Alimdanganya Baba yake Isaka na kupora Baraka za ndugu yake,alimdanganya Labani na kutoroka bila kuaga.maisha yake yalijaa ubabe na kutumia nguvu zake kutimiza matakwa yake,Baada ya kuguswa pale Penueli tunamwona Yakobo aliyebadilika katika maisha yake yaliyo fuata, Tunapokutana na Mungu kuna mabadiliko katika Historia YETU,mwenendo na Tabia zetu Hubadilika,Historia yetu hubadilika.haijalishi historia yetu ni mbaya kiasi gani,bado haiwezi kuzuia hatima na kusudi la Mungu Maishani mwetu,Mungu akitugusa mambo hubadilika.

3. MGUSO WA MUNGU WA PANUELI HUTUPONDA NA KUTUNYENYEKEZA NA KUTUFUNDISHA KUMTUMAINI MUNGU PEKEE.                                       (MWANZO 32:31-32)Alama kubwa ya kuguswa na Mungu ni kuacha kutegemea nguvu zetu na uwezo wetu,Kukutuna na kuguswa na Mungu kunatunyenyekeza ,kutufanya Kuchechemea na kuacha kutumia nguvu zetu,akili zetu ,maarifa yetu n.k.Yakobo kutenguliwa Paja ilikuwa ni alama ya kumfanya asalimu amri,baada ya hapo hakuweza kuendelea kushindana tena,Mungu hataki tushindane naye,tutumie nguvu zetu na uwezo wetu,Tusipo salimua amri kwa hiari Mungu atatufanya tusalimu amri kwa nguvu. Ujuzi wa Penueli unatunyenyekeza na una vunja kujitumaini kwetu na kiburi chetu ,Baada ya Yakobo kuvujwa na kunyenyekezwa na Mungu,Mungu aliingilia kati kesi yake na Yakobo,alipoacha kutegemea mipango yake mwenyewe,Mpango wake na NJIA yake ya kumkabili Esau ilikuwa na GHARAMA kubwa sana ,alianda zawadi za gharama ya kubwa sana(Mwanzo 32:13-21),Tukijisalimiasha na kupondeka ,Mungu hutenda kwa njia yake rahisi sana.hatutalipa gharama yeyote ile!

4. MGUSO WA MUNGU WA PANUELI HUANZISHA MABADILIKO MAPYA YA KIROHO KATIKA MAISHA YETU. (MWANZO 33: 18-20)Baada ya mguso wa Penueli,Yakobo alijenga madhabahu baada ya miaka 20! Kukutana kwake na kuguswa na Mungu kulianzisha na kuamsha mabadiliko ya kiroho katika maisha yake tena. Alianza na Shekemu kujenga Madhabahu,na hatimaye Hali mpya ya kiroho ilimpelekea kwenda Betheli mahali pa juu zaidi katika mahusiano na Mungu. Kukutana na Mungu na kuguswa naye katika Penueli yetu hutupeleka kwenye mabadiliko ya Kiroho,Tukiguswa na Mungu kunahatua mpya ya kiroho huanzishwa tena ndani yetu,shauku ya kimungu iliyopotea huanzishwa tena,Ibada huanza tena ndani ya mioyo yetu.

 5. MGUSO WA MUNGU WA PANUELI HUTUAANDAA KWAAJILI YA KULITIMIZA KUSUDU LA MUNGU KATIKA MAISHA YETU:                                                                            (MWANZO 32: 28)Yakobo hatima yake iliwekwa wazi na Mungu baada ya tukio la Penueli,Kubadilishwa jina kulimaanisha pia Hatima yake,na kusudi lake ki-Mungu sasa linawekwa wazi kwake ,na kupitia yeye taifa la ISRAEL likajengwa na kuzaliwa.Kukutana na ,Mungu na kuguswa naye hupelekea kulijua kusudi la Mungu katika Maisha Yetu.`Tukiguswa na Mungu tunaandaliwa kwaajili ya huduma,kazi maalumu,au kusudi la Ki-Mungu katika maisha yetu,Jina Jipya liliwakilisha ,Kazi mpya,Nafsi yake mpya,Mamlaka yake Mpya.

6. MGUSO WA MUNGU WA PANUELI HUTUPA NGUVU WA KUYAKABILI MAJARIBU YATAKAYO KUJA MBELENI. Yakobo alipata nguvu kutoka Penueli iliyompelekea kuya kabili majaribu na mambo magumu aliyokutana nayo mbeleni alipo ingia katika nchi ngeni ya SHEKEMU.(MWANZO 34:1-27),kama sio mguso wa Mungu uliokuwa juu yake toka Penueli,maisha yake yalikuwa hatarini na familia yake yote,Mguso wa Mungu kutoka Penueli hutupa neema ya kukabili majaribu yatayotokea mbeleni na kutufanya tupite salama na kushinda.

Hitimisho;                                                                                              Pengine umefika mwisho wa akili zako,mwisho wa nguvu zako,unahitaji kuitafuta Penueli ya maisha yako itakayobadilisha hali yako? Pengine umeendelea kutumia nguvu zako za mwili,umeendelea kushindana na Mungu kubali kusalimu amri kwake, akuguse akuponde na uone nguvu zake.

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

3 Responses to ITAFUTE PENUELI YA MAISHA YAKO

 1. bintu says:

  Mungu apewe sifa , ninajuwa kama dunia inamambo mengi sana lakini tutaishida siku moja , hii ndiyo mwisho wake . kweli nimekubali yesu kama mwokozi wangu katika maisha yangu . mimi nampenda yesu sana ,na ninapenda watu saana ,ila shetani ndiye adui mkubwa kwetu . mimi ninataka kutoka hapa lakini sina uwezo wowote . kwani sijwi niende wapi . ninapoamuwa kutoka nashindwa , kwa kuwa sijaona kwenye mungu alisema na mtu ili anichukuwe hii ni dunia kubwa sana watu wana kufa ovyo saana . sitaki kwenda kufa na mtoto . mimi sipendi tena kubakia hapa kwa kweli . niliisha choka na hii mgine wa maneno maneno . sina kwenye nitaenda . sina ndugu . basi nina sema asante sana kwa kunijulisha na kunishaulisha . MUNGU AKUPE UZIMA .

  Like

 2. Meinrald says:

  Asante,Mungu akubariki.

  Like

 3. servant sigsmund paschal says:

  nafurahi kuuona ujumbe niliouhitaji. ujumbe huu niliupata jumapili katika ibada ya jioni, na Mungu kwa kipekee akanigusa moyoni. kweli ukikutana na Mungu unabadilishwa jina na kuokolewa. ni baraka kuu sana kukutana na Bwana hasa tunapokuwa faragha kwa maombi. mungu ambariki mtumishi huyu kwa kuuandika ujumbe huu.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s