MAUTI NA KUZIMU… Na Mch. Kiongozi Josephat Gwajima..

Na Mch. Kiongozi : Josephat Gwajima. 15/4/2012
Ujumbe : MAUTI NA KUZIMU

Kila jambo lina nguzo linazozitegemea, na kila utawala una nguzo unaotegemea.. vilevile utawala washetani umejengwa juu ya nguzo ziitwazo MAUTI na KUZIMU.. Ayubu 38:18 na nguzo hizi mbili ndizo ambazo zinashikilia utawala wa shetani na ndio maana maeneo mengi ambayo kuzimu inatajwa basin a mauti ipo pia.. mfano katika kitabu cha zaburi 116 :3 .. HAPA UTAONA kila mahali ambapo mauti imetajwa basi kuna mahusiano na kuzimu ..

MAANA YA MAUTI NA KUZIMU :

MAUTI ni roho ambayo kazi yake ni kuuondoa uhai ulio ndani ya mtu. Na KUZIMU ni roho ambayo kazi yake ni kuwahifazi wale waliokufa.. ufunuo 6: 9, Isaya 28 :15 ..

Mauti ni roho yenye akili na yenye kupanga.. ndio maana wanafunzi wa Yesu , walipomuona Yesu yuko juu ya maji, biblia inasema wanafunzi wa Yesu wakadhani wameona roho.. kumbe roho ina personality ina akili kili, inaweza kupanga na kutekeleza na pia yaweza kumpagaa mtu. Kwahiyo mauti ni roho yenye personslity hapo tunaweza sema mauti ni mtu.. Tunaweza sema mauti ni mtu ina “personality” ufunuo 20 : 13.. mauti inaweza kumeza watu..

ufunuo 20 : 14 kila mahali inapotajwa mauti kuzimu inafuata pale, hii inaonyesha kuwa mauti inaanza alafu kuzimu inafuata.. katika hiki kitabu cha ufunuo 20 : 14 tunaona kuwa “ mauti na kuzimu vikatupwa kwenye jehanamu” kumbe mauti unaweza uka ikamata kabisa na kuitupa mahali.. kama mauti na kuzimu vingekuwa ni matukio basi visingeweza kushikwa na kutupwa kwenye moto. Ndio maana Yesu alipokufa alishinda mauti na kuzimu. ( yohana 20 :3)

tuangalie hili andiko mwanzo 37:25 katika agano la kale kuzimu lilikuwa linatumika kama mahali wafu walipokuwa wanakwenda, na palikuwa panaitwa “sheol” kwa lugha ya kingereza na huko wako wafu wote waliotenda haki na walitenda maovu walikuwa wanakwenda kule.. lakini palikuwa wamepagawa mahali pa watenda haki na mahali pa watenda maovu.. na mahali walipokuwa wanaenda watenda palikuwa panaitwa Kifuani pa Ibrahimu, ( yaani wale walioamua kuungana na imani ya Ibrahim) na sasa kunaitwa paradiso..

TOFAUTI YA JEHANAMU NA KUZIMU:

Jehanamu ni shimo la rohoni la moto watakapo angamizwa watu watendao dhambi, kwasasa jehanamu hakuna mtu ndani maana hukumu bado haijatolewa lakini watu wanaokufa kwa sasa wanaenda kuzimu (bottomless pit) hii ni roho iliyojifunua kama shimo. Isaya 14:11,15 . tunaona shetani alipoasi akatupwa kwenye hilo shimo ndio maana ya maneno yaliyo katika kitabu cha ufunuo 12:7-9 kumbe kuzimu ipo hapa katika nchi, hapaonekani kwa kuwa lipo katika ulimwengu wa roho. Ufunuo 9:15 , KUZIMU ndio kwenye makao makuu ya shetani , wanakofanyia kazi zao.. (operation centre) ufunuo 17:8 .. kwa hiyo ni muhimu kujua kuzimo ipo angani, baharini na hata kwenye nchi.. ndio maana biblia inataja mara nyingu neon hili wakuu wa anga’

KAZI ZA KUZIMU NA MAUTI.

Kuzimu ndio inayo achilia uovu duniani, inaachilia magonjwa, tabu, dhambi, mateso, balaa,mikosi, ukimwi, kuchanganyikiwa, kuchukiwa na watu, inadhoofisha, inatesa na inaleta uhalibifu.. kwahiyo kuzimu inaleta roho ya uzinzi na uasherati, uovu na dhambi na hizi zote zinamfanya mtu kudhoofika na kuishiwa nguvu. Hapo sasa mauti ndo inakuja pale mtu anapokuwa kwenye comma. KWAHIYO kuzimu kazi yake ni kudhoofisha kwanza.. na ndio maana unaweza muona mtu anaumwa hadi kudhoofika sana lakini huyo mtu hafi.. hii ni kwasababu mashetani ya mauti hayajaanza kufanya kazi..

Hapo mgonjwa anapokuwa dhaifu ndipo sasa mauti inakuja na kufanya kazi yake, ya kumuua . na mauti ikifanikiwa kuutoa uhai basi sasa mauti inatuma mapepo wa kuja kumchukua Yule mtu kama alikuwa mtenda dhambi.. na ndio maana utaona kuwa mtu anapotaka kufa waliowengi utawasikia wanasema maneno kama ‘naona giza’ au msinichukue’ basi ujue wakati huo.

Kuzimu inaleta duniani hata mitindo ya kuvaa.. ili kuingiza tamaa za uzinzi na uasherati.. na unapoona tamaa ya dhambi inaongezeka basi jua unakaribia kufa.. kama ulipangiwa kuishi miaka 80 utajikuta unaishi miaka 40.. kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.
Marko 16 :19-22.. Mtu anapokata roho anachukuliwa na malaika kwenda mbinguni au anachukuliwa na malaika kwenda kuzimu..

NGUZO MBILI ZA KIPINDI CHA SAMSON

SAMSON alikuwa mnadhiri alikuwa na jukumu la kuangamiza wafilisti, lakini wafilisti walimnasa baada ya kudanganywa na mkewe, ILI kutoa siri ya nguvu zake, baada ya kujua wafilisti wakmnyoa nywele , wakamtoboa macho na kumweka asage ngano, mfano huu wa Samson unaonyesha hali ya kanisa ya sasa baada ya kanisa kukosa nguvu, na kudharauriwa Mungu ameanza kulipa nguvu kanisa kama nywele za samason zilipoanza kuota.. Samson alipopata nguvu akajitegemeza kwenye nguzo mbili ambazo jingo linazitegemea. Na akazitikisa hadi jingo lote likaanguka kabisa. Ndivyo kanisa linavyotakiwa kuwaangamiza nguzo za mauti na kuzimu.. ili liweze kurudi kwenye uweza wake na ndio maana ushindi wa Yesu msalabani kimsingi ni ushindi dhidi ya mauti…

MAUTI NA KUZIMU HAZINA NGUVU JUU YETU.. Mch. Josephat Gwajima ni mchungaji kiongozi wa kanisa la Glory of Christ T Church.. maarufu kama nyumba ya ufufuo na uzima.. Kawe Dar es Salaam.

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

19 Responses to MAUTI NA KUZIMU… Na Mch. Kiongozi Josephat Gwajima..

 1. enock says:

  nimesoma hapo juu,je mtu akifa huenda kuzimu huko ambako ni chanzo cha mateso mbalimbali? au anaenda sehemu nyingine tofauti na kuzimu.

  Like

  • makiria says:

   MP.MARY BONIPHACE MAKIRIA
   Inategemea mtu akifa anakwenda kuzimu au laa. Mtu kama ameishi maisha ya dhambi akifa atakwenda kuzimu (maana yake motoni) lakini kama mtu akiwa ameishi maisha ya kumtumikia mungu atakwenda mbinguni, kama neno la mungu linavyo sema kwamba kila atakayenitumikia nitamweshimu.
   Mtu akifa inategemea mahusiano yake na mungu ndiyo yatakayo mfanya aende kuzimu au aende mbinguni. mtafute mungu upate kuishi maisha mema. pastor ufufuo na uzima.

   Like

 2. stella says:

  maisha aliyoishi mwanadamu duniani kabla ya kufa ndo yanayoonyesha mtu akifa ataenda wapi, kama maisha yake yalikuwa ya kutenda dhambi na kuhatamia dhambi mtu wa namna hiyo akifa ni kuzimu moja kwa moja, na kama alihishi maisha ya uhaminifu yaani mcha Mungu, mtu huyo akifa anaenda mbinguni.

  Like

 3. makiria says:

  MP. MAKIRIA
  Namshukuru mungu kwa ajili ya Baba yangu Kiongozi Josephat Gwajima kwa mafundisho yake mazuri na yanayotupa mwelekeo wa kusonga mbele tunapokutana na majaribu yanayo tukatisha tamaa, tunapata nguvu tunaposikiliza mahubiri yake kwa sababu anagusa sehemu ambazo ndizo zimeshikilia maisha ya watu walio wengi katika mateso yanayo wapata siku hadi siku.

  Na tunapata nguvu ya kuyashinda kwa sababu anatupa maarifa na mbinu za kuweza kukabiliana na adui wa maisha yetu. kama neno la mungu linanyo sema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Ni kweli watu wengi wanashindwa kuomba kwa sababu hawajui waombe vipi, kwa maana hawaelewi chanzo cha tatizo ni nini. na je? waombeje? unatakiwa kujua tatizo lako ni nini? na hapa Baba ametufundisha namna ya kuomba na ukifuata maombi haya mungu atakubariki. Mungu akubariki wewe utakaye elewa na kuchukuwa hatua ya kuomba. Na zaidi zaidi Mungu ambariki Baba yangu Josephati Gwajima ampe miaka mingi na heri duniani na kumpa mafunuo mengi ili aweze kuponya roho zilizoibiwa na shetani na ambazo zimekata tamaa. Mungu akubariki pamoja na familia yako Baba. pastor ufufuo na uzima

  Like

 4. Milinga. says:

  Ubarikiwe Mtumishi?

  Mafundisho haya mimi naona kama hayako sahihi kwani yameacha maswali mengi bila majibu. Aidha, naona kama yameenda nje ya maana ya maandiko (out of text context).

  Hebu soma ufafanuzi huu hapa kuhusu KUZIMU NA MAUTI ili kuona ukweli zaidi tofauti na maelezo ya Mtumishi ili kujenga mwili wa Kristo zaidi:

  KUZIMU NI WAPI?

  Wazo la kuzimu kwa watu wengi ni mahala pa adhabu kwa’roho zisizopatwa na kifo’ za wabaya moja kwa moja baada ya kufa, au mahala pa kuteswa wale ambao watakataliwa. Ni tendo letu la kusadikisha kwamba Biblia inafundisha kuwa kuzimu ni kaburi, mahali watu wote wanakwenda wakifa.

  Ni neno lisilotumika sana katika misemo ya watu, awali katika Kiebrania neno’Sheol’ limetafsiriwa’hell’ kwa kiingereza. kwa hiyo Biblia ya kiswahili ilipoandikwa tafsiri toka kiingereza neno liliandikwa’Kuzimu’ likiwa na maana’mahala pa kuzika wafu’ Leo watu wametoa habari zinazotofautiana na Biblia inavyoelezea kuhusu neno kuzimu. Biblia yetu ya kiswahili hapa Afrika Mashariki ni U.V ikiwa na maana kuwa ni tafsiri tofauti -tofauti toka Biblia mbali mbali za kiingereza ambazo ni K.J.V, R.S.V, R V n.k sasa hivi Biblia zilizopo kwa kiswahili ni U.V na Biblia habari njema kiswahili cha kisasa kwa kifupi (B.H.N) mifano michache ambayo katika Biblia hili neno’Kuzimu’ limetafsiriwa’kaburi’ linafanya wazo la watu wengi kutofaa kuhusu kuzimu kuwa ni mahala pa ziwa la moto na kuteswa wabaya ni: –

  “E e BWANA, …….. wasio haki wanyamaze kuzimu” (Zab. 31:17).

  “Bali BWANA ataikomboa nafsi yangu, atanitoa mikononi mwa kuzimu – Kaburi (Zab. 49:15) yaani nafsi ya Daudi au mwili atafufuliwa toka kaburini, au kuzimu’.

  Imani ya kuwa kuzimu ni sehemu ya kuadhibiwa wabaya mahala ambapo hawawezi kuepuka haiwezi kupatana na hii; mtu mwenye haki anaweza kwenda kuzimu (Kaburini) na kutoka tena. Hosea 13:14 anathibitisha hivi: “Nitawakomboa (watu wa Mungu) na nguvu za kaburi (kuzimu); nitawaokoa na mauti” mstari huu umenukuliwa katika 1 Kor. 15: 55 unahusu ufufuo Kristo akirudi. vivyo hivyo katika maono ya ufufuo wa pili (ona somo la 5. 5) “mauti na kuzimu zikawatoa wafu waliokuwemo ndani yake” (Uf. 20:13). Tazama mfano kati ya mauti yaani, Kaburi, na kuzimu (pia ona zaburi 6:5).Maneno ya hana katika 1 Sam. 2:6 yapo wazi kabisa: “BWANA huua naye hufanya kuwa hai (Kwa njia ya ufufuo): hushusha hata kuzimuni (kaburini), tena huleta juu”.Kwa kuwa’kuzimu’ ni kaburi itegemewe kwamba wenye haki wataokolewa kutoka hilo kwa njia ya kufufuliwa kwao kupata uzima wa milele. Hivi inawezekana kabisa kuingia’Kuzimu’ au kaburini, na baadae kuliacha kwa njia ya ufufuo. Mfano mkubwa ni huo wa Yesu, ambaye roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukupata kuoza’ (mdo. 2:31).wa sababu alifufuliwa. Angalia usambamba kati ya’roho’ ya Kristo na’mwili’ wake. kama mwili wake “haukuachwa kuzimu” ni kudokezwa kuwa alikuwako huko kwa kipindi, yaani, siku tatu ambazo mwili wake ulikuwamo kaburini. Kama Kristo alikwenda’kuzimu’ uwe ushahidi wa kutosha kwamba sio sehemu wanako kwenda wabaya.

  Watu wote wabaya na wazuri wanakwenda’Kuzimu’ yaani kaburini. Hivyo Yesu “Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya” (Isa. 53:9) kwa kufuatana na mstari huu, ipo mifano mingine mingi ya watu wenye haki kwenda kuzimu, yaani kaburini. Yakobo alisema ya kwamba “nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu (kaburini) …. Akamlilia” Yusufu (Mwa. 37:35).

  Ni moja ya mambo ya awali ya Mungu ya kuwa adhabu kwa ajili ya dhambi ni mauti (Rum 6:23;8:13;Yakobo 1:15). Hapa kwanza tumeonyesha mauti ni hali ya kutokuwa na fahamu kabisa. Dhambi husababisha kuangamia kabisa, sio kuteswa milele (math. 21:41;22:7; Marko. 12:9; Yakobo 4:12), hakika kama watu walivyoangamia kwa gharika (Luk. 17: 27, 29), Kama waisraeli walivyokufa jangwani (1 Kor. 10:10). katika sehemu zote hizi watenda dhambi walikufa kuliko waliteswa milele. Basi haiwezekani kwamba wabaya wanaadhibiwa wakiwa na fahamu kwa mateso na kuona.

  Vile vile tumeona kuwa Mungu hahesabu dhambi – au kutuweka katika taarifa ikiwa hatujui neno lake (Rum 5:13). Walio katika nafasi hii watasalia wakiwa wafu. Walio kwisha jua matwaka ya Mungu watafufuliwa na kuhukumiwa Kristo akirudi. Ikiwa wabaya adhabu wanayopata itakuwa ni kifo, kwa sababu hii ni hukumu kwa ajili ya dhambi. Kwa sababu hii baada ya kuja mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, wataadhibiwa na kisha kufa tena, kubaki katika kifo milele. Hii itakuwa ni’Mauti ya pili’ iliyosemwa katika ufu. 2:11; 20:6. Watu hawa walikuwa wamekufa mara ya kwanza, kifo cha kutokuwa na ufahamu kabisa. Watafufuliwa na kuhukumiwa Kristo akirudi, na kisha kuadhibiwa na mauti ya pili, ambayo, kama mauti yao ya kwanza, hawatakuwa na ufahamu kabisa. Hii itadumu milele.

  Ni katika maana hii ya kuwa adhabu kwa ajili ya dhambi ni ya’milele’, katika hiyo haitakuwa na mwisho mauti yao. Kubaki wafu milele ni adhabu isiyo na mwisho. Mfano wa Biblia kutumia aina hii ya maelezo yanapatikana katika K/Torati 11:4. Huu unaeleza Mungu akiwaangamiza mara moja Jeshi la Farao katika Bahari ya shamu milele, maangamizi yanayoendelea ni kama hasa jeshi hili halikurudia tena kuwasumbua Israeli, “alivyowafunikiza na maji ya Bahari ya Shamu …….. alivyowaangamiza BWANA hata hivi leo”.

  Hata katika nyakati za awali za Agano la Kale waamini walielewa kwamba kutakuwa na ufufuo siku ya mwisho, ambapo waovu wanaowajibika watarudi kaburini. Ayu. 21:30,32 yupo wazi sana: “Kwamba mwovu …… na kuongozwa nje (Yaani kufufuliwa) katika siku ya Adhabu ….. pamoja na hayo atachukuliwa (kwenda) kaburini”. Moja ya mifano ya mahubiri kuhusu kurudi kwa Kristo na hukumu inazungumzia wabaya’Kuchinjwa’ mbele yake (Luk. 19: 27). Mfano huu ni shida kufaa katika wazo la wabaya wanaishi milele katika hali ya kuwa na fahamu daima wakipokea mateso. Kwa vyovyote hii itakuwa ni adhabu isiyo na maana – mateso ya milele kwa matendo ya miaka 70. Mungu haoni raha kuwaadhibu watu wabaya; basi inategemewa kuwa hatawapa adhabu isiyo na mwisho. (Ezek. 18:23, 32; 33:11; 2 Pet. 3:9).

  Ufalme wa Kikristo ulioiacha imani mara nyingi unajumuisha’kuzimu’ na wazo la moto na mateso. wazo hili hutofautiana vikali na mafunzo ya Biblia kuhusu kuzimu (kaburi). “Kama kondooo wamewekwa kwenda kuzimu (kaburini); na mauti itawachunga” (Zab. 49:14) inadokeza ya kuwa kaburi ni mahala pa usahaulifu kwenye utulivu. Mbali ya roho ya Kristo, au mwili kuwa kuzimu kwa siku tatu, haukuachwa uoze (Mdo. 2:31) isingewezekana kama kuzimu ni mahala pa moto.

  Ezek. 32: 26- 30 inatoa picha ya mashujaa wa vita wa mataifa yaliyowazunguka, wanalala kwa amani katika makaburi yao: “Mashujaa wao ….. walioanguka (katika vita) walioshuka kuzimu pamoja na silaha zao za vita: ambazo wameweka panga chini ya vichwa vyao ….. wamelala ….. pamoja nao washukao shimoni”Hapa tunatajiwa desturi za mashujaa kuzikwa na silaha zao na kukilaza kichwa cha maiti juu ya upanga wake. Lakini haya ni kueleza’Kuzimu’ – kaburi. Hawa watu mashujaa bado wanalala kuzimu (yaani, kaburini) ni shida kusaidia wazo la kuwa kuzimu ni sehemu ya moto.

  Vitu vya mwili (kwa mfano, mapanga) kwenda sehemu moja “kuzimu” kama watu, ikionyesha kwamba kuzimu sio uwanja wa mateso ya kiroho. Hivyo Petro alimwambia mtu mwovu, “Fedha yako na ipotele mbali pamoja nawe (mdo. 8:20) Taarifa ya yaliyompata Yona yanapinga hili. Akiisha mezwa hai na samaki mkubwa, “Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki akisema, Nalimlilia Bwana …. Katika tumbo la kuzimu naliomba” (Yona. 2:1,2).’Tumbo la kuzimu’ hili ni sambamba na hilo la nyangumi. Tumbo la nyangumi kweli palikuwa ni’mahala pa uficho’ ambayo ndiyo maana ya neno msingi’Kuzimu’ lililotafsiriwa’kaburi’ Ni wazi haikuwa ni sehemu ya moto, Yona alitoka nje ya “tumbo la kuzimu” hapo nyangumi alipomtapika. Jambo hili lililenga mbele kwenye ufufuo wa Kristo toka’kuzimu’ (kaburini) – ona Mathayo 12:40.

  Natumaini kwamba tutazidi kujifunza zaidi.

  Like

 5. Agnes Ndalahwa says:

  Utukufu..
  Mimi namshukuru sana Mungu na sina cha kujieleza juu ya mafundisho ya baba yangu wa kiroho Josephat Gwajima , kweli ninampenda sana sana sana na Mungu akujaze mabaraka na uzidi kutufunulia na kutufundisha yaliyo mema. Nimejifunza mambo mengi sana kupitia kwa baba huyu wa kiroho , namna ya kushindana na adui , namna ya kuomba , maana halisi ya sadaka na mafunzo mengi mengi ambayo ameniweka karibu sana na Mungu na hata nisiweze kukubali kupoteza hata kipindi kimoja cha ibada kanisani. Utukufu uwe kwa Mungu na atukuzwe daima , asante sana baba , nakuombea maisha mema na marefu baba , asante sana mimi ndio naweza jua umuhimu wangu kuwepo hapo kwenye bonde la kukata maneno. baba asante kwa mafundisho yako . najiona kabisa mimi ni mtu wa tofauti kutoka pointi moja kwenda nyingine.

  Like

 6. Abas minga says:

  Mi niko Ileje mbeya lakini ninafwatiliasana mafundisho ya mchungajihuyu na yamenibadilisha kwa kiasi cha ajabu,hivyo namshukulu Mungu na Munguazidikumbaliki na kumpa mafunuomengine mengi kwani mimi namuonamungu kupitiavitabu na mafundisho yake natamanisanaibada zake Munguambaliki aishi milele

  Like

 7. filbert orio says:

  mm naitwa filbert orio ningependa kukutana na mchungaji gwajima nasali hapo ufufuo na uzima namba yanguya cm ni 0654086913

  Like

 8. shangwe says:

  utakatifu ndio kigezo kikubwa cha kuingia gates za mbinguni – na utakatifu huu ni kwa njia ya kuoshwa kwa DAMU YA YESU

  Like

 9. Shepherd. Joshua mahundi says:

  Mimi ni shepherd joshua mtumish wa bwana naendelea muomba mungu kwa ajili ya baba yangu gwajima kwani kwa kupitia yeye nimepata mambo mengi ambayo hayawez semekana mungu awe pamoja naye sasa na hata milele maadui zake wawe maadui wa yesu kristo

  Like

 10. erick says:

  tubuni kwa maana ufalme wa mungu u karibu

  Like

 11. ARNOLD PETER says:

  BABA naendelea kubarikiwa na mafundisho yako na hasa ili la MAUTI NA KUZIMU limenipa upana wa maarifa wa kumfahamu shetani kiundani na kazi zake, na kuweza kumfahamu YESU kiundani zaidi, MUNGU akubariki sana maana ninabarikiwa

  Like

 12. Peter j says:

  May i have personal contact email from PST GWAJIMA?I am from Njombe

  Like

 13. baraka charles says:

  namshukuru yesu aliye niokoa toka dhambini.dugu zangu napenda mjuekwamba neno la mungu ni roho hai kabisa,hivyoinatakiwa ufunuo wake kulijua,mfano agano la kale limetaja kuzimu kama sehemu ambayo watuwote walikwenda baada ya kufa walio haki na waovu ingawakulikuwa na utengano kidogo,nikweli,lakini siokwamba hadi leo iko ivo,hapana,ilikuwa vile kwasababu dhambi zao zilikuwa hazijaondolewa kabisa ila zilifunikwa tu,utaona baada ya kuja yesu aondoaye dhambi zote kwa damu yake,alipo kufamsalabani ilemiili ya watakatifu ilitoka makabulini kuzimu na kuingia peponi,utaona kweli kuwa hadi sasa mauti na kuzimu hazina nguvu kwa mtakatifu.pia kuzimu siokwamba ndo jehunum la nitofauti na piakuzimu hakuna moto ila nisehemu ya mangojeo ya waovu kwa hukumu yamwisho lakini simahala salama nitaabu kuu.hebu tumwache roho mt.atuongoze tusitumie akili zetu zadunia hii kumjua yesu haiwezekani,pia watu wanataka kujuakuzimu ikowapi wakati hatakumjua mungu na kutangaza neno ambalo ni agizo wameshindwa,tangaza neno.amen

  Like

 14. Imani Swillah says:

  Please send me any updates from Pastor Gwajima. Be fully blessed.

  Like

 15. Jejacs says:

  Naomba contact za Pastor Gwajima nina kiu ya Kuwa na kitabu chake cha Maombi ya Kushindana

  Like

 16. Landelinus says:

  Ubarikiwe kwa kuhubiri ukweli huo . Mungu wa Amani na ukufunulie ukweli mwingine kama vile utunzaji wa sabato,meza ya bwana na mengine (Yakobo2:10)

  Like

 17. Yasin Ibrahim says:

  Safi xana pastor

  Like

 18. Musa lameck says:

  Ubarikiwe mchungaji

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s