KUISHIWA NGUVU/UCHOVU KATIKA HUDUMA

 

INTERNATIONAL CHRISTIAN MINISTRIES (ICM)-TANZANIA

SOMO: JINSI YA KUISHINDA HALI YA KUISHIWA NGUVU/UCHOVU KATIKA HUDUMA

(HOW TO OVERCOME BURN-OUT IN MINISTRY)

Imetayarishwa na Pastor Meinrald A. Mtitu

1.      MAANA YA UCHOVU/KUISHIWA NGUVU(Burn-out)

·         Burn-out- Ni Kuungua mapaka kuteketea Kabisa,Kutumia nguvu mpaka zinakwisha kabisa.Burn-out  ni kuchoka sana kwaajili ya jitihada za muda mrefu.

 • Ni aina ya mfadhaiko na uchovu wa kihisia, kuchanganyikiwa  na kuishiwa nguvu  kunakotokea wakati mfululizo wa matukio katika mahusiano,huduma,kazi, na mtindo wa maisha  unaposhindwa kuzalisha/kuleta matokeo tuliyoyatarajia.
 • ·         Ni hali ya kuchoka kabisa kimwili, akili, kiroho ,na kihisia kunakosababishwa na kiwango cha juu na endelevu cha mafadhaiko,kunakopelekea mwili kuzalisha kupita kiasi kemikali za adrenali.hali hii hupelekea mtu kujihoji juu ya uwezo wake na uthamani wa kazi anayoifanya.

2.      MATOKEO YA “BURN-OUT” YA UCHOVU/KUISHIWA NGUVU;

Kuishiwa nguvu,au uchovu huathiri maeneo makuu manne,mwili,akili,Roho,Hisia.

KUTOKA 18:14-26

 • KUCHOKA KI-MWILI :                                                           Mwili wako unauweza wa kikomo wa kukabiliana na mfadhaiko mzuri au mbaya kimeng’enya aina adrenali inafanya kazi ya kutoa nguvu za ziada.lakini inaposukumwa mara kwa mara mwilini inafanya mwili uchoke,badala ya kuupa nguvu ya ziada,hupingana na mwili na kuufanya uchoke
 •  KUCHOKA KI-AKILI                                                                  Ni hali ya Akili kuchoka kabisa.Wachungaji kwa maadili ya wito wao,wanapaswa kutumia akili pengine zaidi ya kazi nyingine zote.kuandaa mahubiri kunahitaji kufikiri kwa kina, kufanya maamuzi, kushauri,kuandaa ibada, kuandika na kutangaza maono kunahitaji akili na mara zote kunatumia akili ya mtu.Kufidia mahitaji yaliyopelekwa katika ubongo,mwili huzalisha kimeng’enya ya aina yake ya caffeinated coffee-Adrenaline-hii huwezesha akili  kuweka mkazo zaidi katika kazi iliyopo wakati huo iwe ni kushauri, kuhubiri, Lakini Akili inapokosa kupumizishwa adrenali aina hii hufanya kazi kinyume cha Ubongo na kuzalisha uchovu
 • KUCHOKA KIROHO:                                                                      Uchovu ni hali ya kuchoka kabisa kiroho.huduma ya uchungaji inatumia na kunyonya nguvu zako za kiroho.Mchungaji wakati wote anatoa.Imenenwa kwamba Huduma ya kuchungaji ni mahali  pazuri kwa mtu kupoteza hali yake ya kiroho. Hii ni kwasabu ya kanuni ya uhitaji na ugavi.watu wanahitaji zaidi ya vile mchungaji anavyo weza kugawa.anagawa haraka  kuliko vile yeye anavyo pokea.Hatimaye hali hii inamlema na maisha yake ya kiroho yanatumika mpaka kukaribia kumalizika kabisa.Kuna hatari kubwa ya kugeuka nchi kavu,au Jangwa ambalo halizalishi tena,kila kitu kimetumika.kuchoka Kiroho ni kama kuwa Bahari mfu,bahari ambayo haina uhai,inapokea tu bila kutoa.,Ukikoma kupokea,utakoma kutoa,ukitao utatoa lakini si VITU  venye uhai,wachungaji wengi wako katika hali hii.
 • KUCHOKA KIHISIA                                                                        Ni hali ya kuchoka kabisa Kihisia/Mhemko- furaha,huzuni,huruma,hasira,Wasiwasi,mashaka,hatia ,kushindwa ni mihemko ambayo mara kwa mara wachungaji /viongozi huwanayo.tatizo huja pale ambapo hisia hizi zinapo ambatana mara kwa mara kupita kiasi, husababisha tatizo la kihisia.Hisia hizi zinapoenda kwa mfululizo bila kupumzika ,huulazimisha mwili kutengeneza Adrenali ili kuufanya uendelee.Hisia/Mihemko inapokuwa inaendeshwa kwa adrenali kwa kipindi Fulani,nyufa za kihisia  ni hakika zitatokea. Hasira,hisia za kujiona umeshindwa/umefeli,hujafanikiwa,kujihukumu, kujiona na hatia,kudanganyika kimawazo na,kuchanganyikiwa ni  tabia za kawaida za kuchoka kihisia Kazi ya uchungaji/uongozi ina husisha sana hisia,hivyo ni rahisi sana kuchoka kihisia ukiwa kiongozi na Mchungaji, Matukio yanayohusisha hisia,Harusi,Misiba,migogoro,ushauri,maombezi,kunenwa vibaya,.

 

3.      SABABU ZA UCHOVU (KUTEKETEA KWA NGUVU)KATIKA HUDUMA

A.    Sababu za kuchoka/kuteketea kwa nguvu kimwili:

·         Kukosa  usingizi wakutosha na muda wa kutosha wa kupumzika,wastani wa masaa 8-6

·         Kufanya mazoezi ya mwili/viungo kidogo au kutofanya kabisa

·         Kuongezeka uzito au kupungua kupita kiwango kinachohitajika kwa mwili wako

·         Upungufu wa vitamin na madini mwilini.kutokukula mlo kamili

·         Ugonjwa-ni vizuri kuwa na utaratibu wa kucheck afya, matatizo ya kifya yanapogunduliwa mapema ni rahisi kuyatibu bila kuhatarisha maisha.

·         Kufunga mifungo ya muda mrefu mara kwa mara bila utaratibu mzuri wa jinsi gani ya kurudisha afya baada ya mfungo mrefu.

·         Kukosa muda wa kupumzika,kupumzika si lazima kulala usingizi,unaweza pumzika kwa kufanya jambo tofauti nay ale amabayo huyafanya kila siku,kucheza michezo,kujiburudisha, kufanya mambo ambayo huwa yanakuvutia,”hobby”

B.     Sababu za kuchoka Ki-hisia

o   Kuwa na wasiwasi kupita kiasi-katika hali ya kawaida tunatarajia wachungaji wasiwe na wasiwasi sana ukilinganisha na watu wengine,lakini sivyo ilivyo.kwanini unaomba kama unaweza kuwa na wasiwasi?Wachungaji wengi wanawasiwasi uliojificha juu ingawa nje wanaoneka wa kiroho lakini ndani kuna wasiwasi mkubwa juu ya familia zao,kodi ya nyumba,kusomesha watoto,kipato kidogo, afya,fedha,huduma,Kanisa halikui, mahali pa kuabudi,migogoro na uongozi wa kanisa na mambo mengine,haya yote yana leta mchoko wa kihisia

o   Kuvunjika moyo- Watumishi wengi wanaacha huduma baada ya miaka michache ya huduma kwasababu tu mambo hayakwenda vile walivyotarajia.mambo kwenda kinyume na vile ulivyotarajia katika huduma.Matarajio ambayao hayakutimizwa hutoa udongo wenye rutuba  kwa mbegu za uchungu kuchipua na kusababisha mtu apate Mkandamizo wa Hisia wa Hali ya juu .

o   Kujihurumia/kujisikitikia-kuona Mungu hajakufanikisha kama wengine,Huna Jengo kubwa, huna nyumba,huna gari zuri,huna washirika wengi,kumbuka Mungu anavutiwa zaidi na uaminifu  zaidi ya  idadi kubwa.n.k

 • Kuumizwa kuhisia-kuwawepesi kushambulia kuna haribu hali ya hisia zetu.ni rahisi kuumia tunapojua kuna watu hawapendi kiletunachofanya,au hawapendezwi nasi,kumubuka kamwe hatuwezi kuwapendeza watu wote,hakuna mtu aliyeweza kuwapendeza watu wote,Hata mtu mkamilifu Yesu Kristo,alikuwa na watu wakumkashifu.Tatuta kumpenda Kristo.Kadiri Mchungaji anavyotafuta kumpendeza Kristo,Mchungaji huyo atawapenda wengine pia ambao wanatafuta kumpendeza Kristo.
 • Kubeba sana matatizo ya watu: Huwezi kamwe kumsaidia kila mtu na kumpendeza kila mtu katika huduma.

C.    Sababu za kuchoka kiroho

o   Kiburi:-Hata mafanikio katika huduma bado yanaweza kumpelekea Mchungaji kuwa katika hali ya uchovu wa kihuduma kama ataamini kwamba maendeleo na mafanikio ya kanisa ni kwasababu yake na juhudi zake na siyo ni Baraka ya Mugu.(Daniel 4:30)-mfano wa Nebukadezar.

o   Kutimiza andiko na siyo roho:-kusoma biblia kuwanaweza kuwa kazi ngumu ya kuchocha,kuomba kukawa kazi ngumu,kujifunza kukawa ni mzigo mzito,na kuhubiri kukawa ni utaratibu wa usio na kina ,ni juu juu tu.Kuna vipindi vya kujiona mkavu kiroho wakati mazoezi ya kiroho yanapopungua,lakini inapogeuka na kuwa desturi,Mchungaji hapo anaelekea kwenye uchovu wa Kiroho.

o   Kushindwa kimaadili-kwa kila mchungaji anayeshindwa kimafundisho,pengine wapo kadhaaa wanaoshindwa kimaadili.taama za mwili zinaposhukua nafasi ya  kuendenda katika roho.ushirika na Mungu unapotea,matokeo ni kuchoka kiroho

TAKWIMU KUHUSU WACHUNGAJI NA UCHOVU KATIKA HUDUMA:

 • 33% ya Wachungaji  walijihisi wako katika hali ya kuchoka kihuduma katika miaka yao mitano ya kwanza ya huduma
 • 25% ya wake za wachungaji  wanaona ratiba za huduma /kazi za waume zao ni chanzo za migogoro nyumabani/ugomvi
 • 40% ya wachungaji na 47% ya wenzi wao wanateseka na uchovu,mapangilio wa kazi wa kukasirisha na kutokana na matarajio yasiyo na uhalisia
 • 45% ya wake za wachungaji wanasema hatari kubwa zaidi kwao  na kwa familia zao ni Uchovu wa kimwili,kiakili,kihisia na kiroho.
 • 45% ya wachungaji wanasema  wamekuwa na hali ya mkandamizo au Uchovu kwa kiasi ya kwamba  wanahitaji kuchukua likizo na kutokuwepo katika huduma.
 • 56% ya wake za wachungaji wanasema  hawa marafiki wa karibu
 • 57% ya wachungaji walisema wangeacha  uchungaji kama wangekuwa na kitu kingine cha kufanya au mahali pengine pa kwenda.
 • 80% ya wachungaji walisema hawana muda wa kutosha na wenzi wao.
 • 25% Ya Wachungaji na wake zao wana ana amini kwamba kuwa katika huduma ya uchungaji ni hatari kwa hali nzuri za familia zao na afya zao.
 • Wachungaji 15000 wana acha huduma zao kila mwezi kutokana na uchovu,migogoro au kushindwa kimaadili
 • 75% Ya wachungaji wanatumia chini ya Jioni moja kwa mwezi kwa muda wa kijamii tu na wake zao na watoto wao.
 • 70% wanafanya kazi zaidi ya masaa 60 kwa wiki
 • 85% wanatumia masaa 2 au chini ya hapo kwa wiki nyumbani.

5.      DALILI/ALAMA ZA KUCHOKA KATIKA HUDUMA

Kuna aina mbili za dalili za kuchoka –dalili za ndani na dalili za nje

A.    DALILI ZA NJE NI  PAMOJA NA MAMBO YA FUATAYO

·         Kuongezeka kwa shughuli lakini uzalishaji/ufanisi unabaki uleule, ambao unaitwa uwendawazimu  insanity-kufanya jambo lilelile kwa muda mrefu na kupata matokeo yale yale. Kuwa na shughuli nyingi si Kiroho.Kimsingi unapaswa kutumia nguvu kidogo tu na kuwa na matokeo makubwa-maarifa ni ya muhimu zaidi ya nguvu na bidii nyingi.

·         Kuchoka kimwili,kuishiwa nguvu-kuchoka mfululizo ni dalili ya Burn-out,kujiona hupendi kufanya jambo lolote lile.Kupenda kulala tu,kuona kero kuamka hasa alfajiri.

·         Kutokuwa tayari kujihatarisha au kuthubutu-kukwepa  changamoto katika huduma,kukwepa watu na marafiki,kupoteza imani juu yako mwenyewe na kupoteza uwezo wa kukamilisha mambo.

·         Kukwazika kirahisi/kukasirishwa na mambo na watu ,hata Mungu mwenyewe kirahisi- Musa na Yeremia ni mfano mzuri –Hesabu 11:11 Yeremiah 20:7,

·         Kukosa usingizi ,kupoteza hamu ya kula,Kuwa na mawazo mengi,kupenda kuwa pekee yako , “kujificha katika upweke”

·         Kupooza /stroke,shinikizo la moyo,kipanda uso,kichwa kuuma mara kwa mara

·         Matatizo ya kuyeyusha chakula,matatizo katika utumbo mkubwa (coronary problem),vidonda ya tumbo/ulcers.

B.     DALILI ZA NDANI NI PAMOJA NA MAMBO YAFUATAYO:

·         Kupoteza ujasiri

·         Kupoteza kujiamini na uthamani wako binafsi

·         Kuwa na mtazamo hasi

·         Kupoteza  makusudi- kumwona Mungu ni chanzo cha kushindwa kwako,kujikasirikia mwenyewe kwa kushindwa kufikia malengo

·         Kuchoka kihisia,depression,mkandamizo

·         Hatia ya kujiona hufanyi vya kutosha,huna matokeo ya kutosha, na kufikiri pengine ukiongeza bidii nyingi ndipo utaona matokeo,kwa wengine hupelekea kufunga sana mfululizo kuomba sana,kukesha sana,wakifikiri kwa kufanya hivyo kutakuwa na matokeo kinyume chake,hupelekea uchovu zaidi na hakuna matokeo.

·          Martha complex-kuwa na shughuli nyingi sana na kukosa muda binafsi wa Mungu kukuhudumia

C.    ALAMA KUMI NAMOJA ZA KUJIPIMA KUCHOKA KIHUDUMA:

1.      Kuanza kuwadharau watu ulioitwa kuwapenda na kuwahudumia

2.      Unaanza kurushu mawazo yako kuchukuliwa na mambo mengine ambayo ungeweza kuyafanya zaidi yakufanya huduma .

3.      Unajihisi ni kama “mashine ya huduma”  hivyo unafanya yale ufanyayo ukiwa na hatia ya kwamba ni Lazima  uyafanye badala ya kutenda kwako  kutokane na kutembea kwako karibu na Mungu(Mahusiano),kazi ya Bwana Vs Bwana wa Kazi.Juhudi vs Ufanisi.

4.      Unaanza kufanya maaumzi kulingana na nini ni rahisi kuliko vile unavyojua ndivyo Mungu anakutaka ufanye.

5.      Unazidi kuwa mkosoaji na kupita kiasi juu ya makanisa,watu,na huduma za watu wengine ambazo unafikiri Mungu anazibariki kuliko  huduma yako na wewe

6.      Hukumbuki lini mara ya mwisho ulifungua Biblia kwaajili kwaajili ya ushirika wako binafsi na Mungu,bali ni kwaajili ya kutafuta Mahubiri na Masomo ya kufundisha Biblia

7.      Unaanza kuwaona watendakazi wanaotumika pamoja na wewe  kama watumishi wako badala  yakuwaona kama ni watumishi wa Mungu.

8.      Unatumia kugawa majukumu kama udhuru ya kuwa mvivu,una kwepa majukumu kwa kuwagawia wengine wafanye.

9.      Hukumbuki mara ya mwisho ni lini ulikuwa na mazungumzo na mke wako ambayo haya husiani na mambo ya kanisa

10.  Hukumbuki mara ya mwisho ni lini ulitumia muda na watoto wako na mkafurahia pamoja.

11.  Unaanza kutilia mashaka nguvu za Mungu ndani yako na ndani ya maisha ya watu wengine.

HALI KUCHOKA KATIKA HUDUMA YA ELIJA:

A.    Chanzocha uchovu wa Elija:

Matarajio yake kutotimizwa,Matarajio yake juu ya Yezebel hayakutimia na akakabiliana na upinzani ambao hakuutarajia-1 Wafalme 19:

Tunapotarajia mafanikio kwasababu ya nguvu zetu wenyewe na ndani ya muda wetu tuliojiwekea wakati matarajio haya hayatimii,yawe niyale tuliyopewa  na Mungu au mengineyo,kinachofuata ni kuanza kumtegemea Mungu Kidogo na kujitegemea wenyewe zaidi,Hapo Kuchoka Hakupo mbali,lazima Tutachoka.

Je,tuwe na matarajio makubwa?tutarajiw miujiza? Ndio ,lakini katika njia yake siyo na siyo katika njia yetu (ISAYA 55:8-9)

Jua ukomo wako,mpaka wako,mwisho wa uwezo wako na usinie makuu(WARUMI 12:3)

Kuchoka au kuchakaa –Kuna husisha matarajio ambayo hayajatimia,Kile alichofikiria mtu kitatimia au kitatokea katika huduma ambacho kingempa furaha ,kutambulika,utoshelevu,usalama na kujihisi vizuri ,matokeo yake hakitimii.

  Dalili za kuchoka kwa Elija:

              YAKOBO 5:17; I WAFALME 19:1-4,10

1.      Ubinafsi/kujisifu/kujiona-Ubinafsi wa Elija uliambatana na hisia za kuwa pekee.Mungu alimkubusha kwamba hayuko pekee yake aliyebakia,walikuwako wengine wasio muabudu baali.

2.      Hisia za uchungu na chuki-alikuwa na uchungu kwamba wengine wamemwacha Mungu.na hali hiyo ikawa inamnyonya nguvu zake za muhimu za kihisia.

3.      Hisia za kuona anaonewa kila wakati (paranoia)- Eliya  na sasa wanataka kuniua na mimi pia.ni kama vile amelikuza tishio moja la yeye kuta kuuawa kuwa ni mkakati wa kitaifa wa kivita wa kutaka kumuua

4.      Hisia za kujihurumia- Maneno yake yame jaaa “mimi”

5.      Hisia za uchungu na hasira dhidi ya Mungu-Mungu hakuwa anahitaji kukumbushwa jinsi gani Eliya Amekuwa na bidii yake na jina lake.kumwambia Mungu amuue( v4)ukilinganisha na malalamiko yake ya “wanataka kuniua”(v.10) yanaonyesha kutoridhika kwake na kukosa kumtumaini Mungu kuhusu nguvu zake na uwezo wake wa kutawala kila kitu kuhusu maisha yake.

Hisia hizi ni zina weza kumtokea mtu yeyote anayepitia kipindi cha kuchoka.Elija alikuwa mwanadamu kama sisi.

C.    TIBA YA MUNGU KWA UCHOVU KWA ELIJA

Tunaona vile Mungu alivyoshughulika na kumponya Elija katika hali ya uchovu,na tunajifunza kanuni kadhaa za kutusaidia katika hali kama hiyo:

1.      Mungu alishughulika kwanza na hitaji la kimwili-kupumzika na kumlisha

2.      Mungu aliruhusu Elija  aone kwamba yeye Mungu bado anatawala Mazingira na kwamba bado ana husika na maisha ya Elija.(9-17)mazungumzo marefu baina yao yanaonyesha vile Mungu anavyoendelea kumjali Eliya.

3.      Mungu anakupitia mzungumzo na Eliya ana msaidia kuondoa Hisia zote hasi,na nakuzitoa,ni muhimu kutozizika,lakini kuzidhihirisha hisia(ingawa si kwa namna ya kuwa umiza wengine)Ni pale tunapoweka wazi hisia zetu kwa wengine ndipo tunaanzakuona kwa uhalisia…zipo vipi na ndipo tunapoweza kuziondoa.

Mungu  kwa uvumilivu anamfanya Elija afunue wazi hisia zake na aeleze vile anajisikia(v4,10,14)

4.      Mungu anampa kazi mpya Elija iliyo nyepesi baada ya kuwa amedhihirisha hisa zake.(v.15-16),watu ambao wamatoka kupitia kipindi cha kuchoka wasirudhishe maramoja kwenye hali ambazo zitahusihsa mfadhaiko mkubwa,kuanzia kwenye  majukumu mepesi kutawafanya kujenga hali ya kujiamini iliypotea kwa urahisi.

5.      Mungu anampa Eliya jambo ambalo kila mtu ambaye ni mathirika wa UCHOVU anahitaji.Rafiki Mwaminifu.kuanzia wakati huo Elisha anakuwa rafiki wa Elija,Mtendakazi pamoja naye,na mwanafunzi wake.(v.18-21) .Ile hali ya Kuwa pekee yake hailuwa picha halisi,walikuwepo wengine7000,Elija ndiye aliyekuwa mpwekee,lakini hakuwa pekee yake.

D.    MAMBO  MAKUU ELIYA ALIYOHITAJI  KUTOKA KATIKA HALI YA KUCHOKA

·         Elija alihitaji kupumzika na kulishwa- Kuna wakati Mungu kwa neema yake huingilia kati na kutupumzisha wa lazima,Mfano wa Pastor Sammy Pity aliye pata tatizo la sauti ,na pastor mwingine aliye vunjika mguu,na Mungu alitumia fursa hizo kuwa pumzisha toka katika shughuli nyingi za huduma walizokuwa nazo.

·         Elija alihitaji ushirika wa karibu na Mungu-Mungu alisemanaye kwa utulivu sana(v.12)

·         Elija alihitaji Mtazmo sahihi juu yakw mwenyewe-Mungu alimpa jukumu ambalo angelimudu

·         Elija alihitaji mahusiano ya karibu na wengine-Mungu alimpa rafiki na mtumishi ,Elisha.

 MADHARA YA BURN-OUT

Burn-out –Kuungua mpaka kuteketea,ni kuchoka kunakotokana na kupoteza nguvu zote,kutumia nguvu zote za kimwili,kihisia,kiakili na kiroho.

1.      Inapelelea kupotea kusudi la Maisha

2.      Inapelekea kuharibiwa matazamo Binafsi wa Mtu

3.      Inapelekea Mtu kujiona mpweke, Zaburi 55:6-8

4.      Inapelekewa kujawaa na uchungu na Hasira ya Ndani Hesabu 11:11-12,Yeremeia 20:7

5.      Inapelekea kuona na kuhisi hauna matumaini yoyote tena.

6.      Inapelekea kifo cha mapema

7.      Inapelekea kuacha huduma au kubaki katika huduma lakini bila matokeo yoyote ,na huduma inabakia kama sehemu ya kuponea katika maisha.

8.      Inapelekea kwenye tabia za dhambi na vifungo,kama uzinzi,kuangalia T.v. masaa mengi,kuangalia sinema muda mwingi,kucheza game kupita kiasi,kuangalia picha za ngono,yote hii huanza kama njia ya kupunguza burnout lakini ni njia hatararishi na siyo sahihi.

TIBA ZA BURN OUT

1.      Badilisha Eneo,toka nje ya eneo na mazingira yako ya huduma

2.      Badilisha shughuli-pumzika

3.      Badilisha Muda

4.      Badilisha Vipaumbele vyako

·         Wewe  na Mungu-maisha yako binafsi ya Kiroho

·         Wewe na Mke wako-maisha yako ya ndoa,hakuna ndoa ,hakuna huduma yako.

·         Wewe na  watoto wako-familia –Kanisa huanza nyumbani

·         Wewe na Huduma.

·         Wewe na watu wengine

 MUHUTASARI KUHUSU (BURN-OUT) UCHOVU:

UCHOVU:

         Ni kuchoka sana kwa jitihada za muda mrefu ,kuishiwa nguvu,kimwili,kihisia na kiakili.

         Kunatofauti kati ya msongo (stress) na kuchoka(kuteketea nguvu)

                                        SABABU ZA UCHOVU

STRESS/MSONGO

BURNOUT/UCHOVU

Unatabia zifuatazo

1.      Kujihusisha kupita kiasi na shughuli

Unatabia zifuatazo

         Kutojihusisha katika shughuli

2.      Hisia zilizopitiliza

         Hisia zilizopotea

3.      Dharura na shughuli zilizopitiliza

         Kutokuwa na matumaini na kutojiweza.

4.      Kupoteza nguvu

         Kupoteza msukumo

 

      5.  inaleta wasiwasi mwingi

         Ina pelekea mkandamizo

     6.  Uharibifu wake huwa zaidi katika mwili.

         Uharibifu wake wa huwa zaidi katika hisia/mhemko 

Dalili /Alama za Burn-out

 1.      1. kupoteza hamasa  na motisha

2.   kuhusi kutothaminika

3.      kukosa sababu sahihi ya kukwenda ofiini  kanisa. (Search for an alternative)

4.      Kupoteza hamu ya kula kunakopelekea mwili kuwa na kinga dhaifu(kuwa na maabukiza kama mafua,homa,kifua)

5.      Kuchoka kwa mwili kunakofanya mwili kuwa katika hali ya kuchoka kwa muda wote.24/7

6.      Matatizo ya kiafya kama vile Shinikizo la damu,kisukari,vidonda vya tumbo etc.

7.      Hayo maradhi yanakuwa sugu na kupelekea kuwa na hasira za haraka.

8.      Kutokuwa na matumaini na kukosa msaada-una hisia ulipofika hakuna sana kinachoweza kubadilika.

9.      Unajitenga na mwenyewe kutoka kwa wengine-

10.  Uchoshi unaofanya akili kuumia-unapoteza shauku na ujuzi wako,kazi yako,taaluma yako.

11.   Kuahirisha mambo kunatokea. Kuahirisha mambo ya muhimu na matukio na kuyapeleka  siku za usoni.

12.   Udhaifu katika kutawala muda. –chochote unachofanya sio kwa wakati na kwa usahihi .

13.  Kusahau kunatokea.unapokuwa umechoka sana hatimaye mambo yote yanakuwa jinamizi.

SABABU YA KUCHOKA SANA:

Zifuatazo ni dalili za kuchoka sana

1.      Kazi nyingi kupita kiasi

2.      Kuwa mtu wa kukubaliana kila kitu na mkuu wako au bosi wako.

3.      Kuhisi umekwama katika ujuzi wako/taaluma yako.

4.      Kuwa mlevi wa kazi

5.      Kulazimishwa katika mazingira yanayokukandamiza. Kuona una majukumu kupita kiasi

6.      Kufanya kazi  na wateja ambao hawana mwitikio na ushirikiano. Matatizo ya kifamila kama fedha.

7.      Mafanikio ya  uponyaji.

 

TIBA YA UCHOVU

1.      Jifunze kuweka mipaka.

         Jifunze kuwa na hisia za uchechi-uwe rahisi na unaye weza kukalibiwa  kirahisi. Tengeneza  mtandao  usiwe mpweke, gawa majukumu kwa wegine. Unapokuwa peke yako kimbia kwa kasi lakini kwa muda mfupi.mnapokuwa wengi kimbia taratibu  lakini kwa muda mrefu..

2.      Uwe na shughuli nyingine mbali na shughuli za kanisa,kama vile michezo,matembezi.

3.      Wakati wote tunza akilini mwako lengo yako.

4.      Jifunze kuthamini kudhihirisha hisia hasi zako.

5.      Hudhuria semina mahali kwingine,katika makanisa mengine na maeneo mengine.

6.      Tengeneza tabia ya kupumzika –chukua siku moja kupumzika katika wiki na chukua likizo ndefu.

7.      Chukua tabia ya afya njema:kula vizuri,fanya mazoezi,lala vizuri.

JINSI YA KUZIMA HALI YA KUCHOKA 

1.      Shughulikia mfadhaiko wako kwa kufanya  mazoezi ya viungo

         Tumia mazoezi  rahisi.

         Andiko maneno  rahisi hewani kama vile Jina lako n.k. kwa kutumia mwili waka au mwenendo wa kichwa.

         Chukua siku moja ya kupumzika.

2.      Tawala muda wako.-usihairishe mambo,uwe na orodha ya mambo ya kufanya.

3.       Gawa majukumu,epuka kujitegemea mwenyewe.

4.      Pata uwajibikaji-mthibitishe mtu unayemwamini.

5.      Fanyaia kazi nidhamu za kiroho kama vile Maombi,Kusoma Biblia,kufunga,n.k..

 

 

 

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s