WITO WA KURUDI BETHELI YAKO

NA PASTOR-TEACHER M.A.MTITU JR.

BETHEL- “MAHALI PA  KURUDISHA UHUSIANO WA KARIBU NA MUNGU WAKO:”

UTANGULIZI:

Je,kuna wakati katika maisha yako ulio kuwa karibu a Mungu kuliko ilivyo sasa?Kama watu tulio mwamini Kristo tunapaswa kila mmoja kuwa na mahusiano binafsi na Mungu,Hili ni Jambo tofauti kabisa na kuwa washirika wa kanisa,au kufanya majukumu ya kikanisa au kuwa na ushirika wa pamoja na wakristo wengine.

Tunaweza husika katika kanisa kijumla katika huduma,ibada,na majukumu mengine na bado tusiwe na ushirika wa karibu wa kibinafsi na Yesu Kristo.Kunatofauti ya  “kutenda”  na  “kuwa”.Huduma za kanisa na shughuli zote za kikanisa kamwe hazipaswi kuchukua nafasi ya mahusiano yetu ya Binafsi na Mungu. Pia ni sahihi na sawa ya kwamba tunapokuwa na ushiano wa karibu na Mungu,tunakuwa tumeunganishwa na Nyumaba ya Ibada,Kanisa lake.

ANDIKO LA MSINGI:

MWANZO 35:1-15  NA MWANZO 28:20-22 –Betheli ni mahali ambapo Mungu alimtokea Yakobo mara ya kwanza wakati anamkimbia Esau kwenda kwa Mjomba wake Labani.Ni mahali Alipo weka Agano na Mungu wake,ni mahali alipoona uwepo wa kipekee wa Mungu. Ni mahali alipokuwa amejitoa na kujiweka wakfu wa Mungu.

Wakati anatoka kwa Labani baada ya miaka yapata 20,inashangaza kwanini Yakobo hakuja moja kwa moja  BETHEL,Mahali ambapo moyo wake ulikuwa tangu mwanzo.Badala yake alienda kukaa SHEKEMU.Uhusiano  wake na Mungu Haukuwa wa karibu tena kama ilikuwa miaka 20  iliyopita,alikuwa amejichanganya na mambo mengi.Kukaa kwake SHEKEMU badala ya kuwa BETHEL Kulimgharimu,kuna mambo yaliyompata ambayo yasingempata kama angekuwa Bethel,

Shekemu palimfanya anonekane vibaya,anuke,asiwe na ushuhuda kwa mataifa walio mzunguka na zaidi palimfanya maisha yake yawe hatarini.Shekemu ni mahali ambapo uhusiano wetu na Mungu ni wa Mbali sana,sio wa Karibu. Neno Bethel –maaan ayake Nyumba ya Mungu,Kwa Abrahamu na Yakobo,Bethel palikuwa mahali maalumu katika ramani  ya nchi ya Kaanani.Mahali halisi kijiografia. Ilikuwa ni Maili 30 Kusini mwa Mji wa Shekemu,na Palikuwa Mile 5 Kaskazini mwa Yerusalemu.Bethel ilikuwa mahali pa juu kwenye mwinuko n kama futi 1010 Kuliko Shekemu, na Betheli ilikuwa ni njia ya kwenda Yerusalem,Bethelem  na Hebron.

Tukiwa nje ya BETHEL,Tunatafuta matatizo.Pamoja na kujenga Madhabahu hapo shekemu,bado hakukuwa na mpenyo wa kiroho maana alijenga madhabahu mahali pasipo sahihi,ni kama kuabudu lakini siyo katika roho na kweli,hakuwezi kuwa na matokeo.

Kwetu sisi leo ,Bethel inawakilisha na inamaanisha Mahusiano sahihi na ya karibu na Mungu.Ilikuw ahivyo kwa Abraham,na ilikuwa hivyo kwa maisha ya Yakobo na ndivyo ilivyo katika Maisha yetu.

Betheli Yetu ipo katika mioyo yetu,Hii inamaanisha tunaweza kuondoka Betheli bila kubadilisha eneo tulilopo kijiografia,unaweza kuwa hapo hapo lakini ukwa umeondoka Betheli yako.Tunapomtazama Yakobo akirudi Bethel,na kuwa na mahusiano sahihi na Mungu wa Betheli tunajifunza mambo yafuatayo ya kuyaangalia katika Maisha yetu.Mambo NANE muhimu ya kujifunza.

1.      SAFARI YA BETHELI  INAANZA NA KUSIKIA NA KUTII SAUTI YA MUNGU:

Kurudisha mahusiano sahihi na ukaribu wetu na Mungu kunaanza na kuisikia sauti ya Mungu na Kuitii,(Mwanzo 35:1),katika MWANZO 31:3 –Mungu alisema naye kitambo lakini hakutii alichukuliwa  na mambo mengine,alipoteza mwasiliano mahali Fulani akawa hasiki tena sauti ya Mungu.Matatizo Yaliyompata SHEKEMU  yalimfanya masikio yake kufunguka  na kumsikia Mungu tena.Je,unaisikia sauti ya Mungu inayokutaka urudi BETHELI?Je,utaendeleea kuipuuza mpaka ujikute kwenye matatizo? Usisubili matatizo ndipo uanze kuondoka kwenda Bethel anza safari sasa,safari ya kurudisha mahusiano sahihi na ya karibu na Mungu.

2.      SAFARI YA BETHELI INAANZA KWA KUTUBU  DHAMBI ZETU, NA KUTAKASA MIOYO YETU NA MAISHA YETU:

MWANZO 35:2-4- Yakobo alianza kwa kufanya matengenezo ya Kiroho, kuondoa Miungu ya kigeni,vinyago yote,na mambo yote yaliyohusiana na ibada za miungu,uchawi  na ushirikina katika familia yake, mavazi yalifuliwa.Hii ilikuwa ni TOBA na KUJITAKASA. Toba na kujitoa upya  kwa BWANA hadharini ni Muhimu kwa ukumbusho.YAKOBO 4:8 Toba na kujitakasa, kunatufanya tuwe  karibu na Mungu,kuna vuta tena uwepo wa Mungu katika Maisha Yetu. Dhambi isiyotubiwa inanyonya uwepo wa Mungu katika maisha yetu.

3.      SAFARI YA KURUDI BETHEL INATUHAKIKISHIA  UWEPO NA ULINZI WA MUNGU

     (MWANZO 35:5)-Mataifa waliomzunguka Yakobo walishikwa na hofu ya Mungu alipoanza safari ya kwenda Betheli,Tunaposhughulika kurujesha uhusiano sahihi na wa karibu na Mungu tuna hakikishiwa ulinzi na uwepo wake Mungu kuwa pamoja nasi. Uwepo wa Mungu unavutwa na Toba na KUJITAKASA kwetu, maadui waliokuwa tishio kwa Yakobo,baada ya yeye kutafuta kurejesha uhusiano wa karibu na Mungu wao ndio walianza kumwogopa,Tukimhofu Mungu na kumcha ,watu wata  tuhofu sisi.

4.      SAFARI YA KURUDI  BETHEL  INAFUNGUA MLANGO  YA BARAKA NA AHADI  ZA MUNGU KWETU ZAIDI:

MWANZO 35:11-12.  Yakobo anathibitishiwa  tena Baraka na ahadi ambazo Mungu alimwapia, Baraka kimsingi ni matokeo ya uhusiano wetu na ukaribu wetu  na Mungu,Baraka za jinsi hii hazi myumbishi MTU,wakati Mwingine Mungu anachelewa kutubariki akisubiri mahusiano yetu naye yawe mazuri,ili Baraka zisitupotezee.Tukiwa  na mahusiano mazuri kwanza na Mungu ,Baraka huwa ni matokeo tu,Baraka zinapaswa kutufuata siyo sisi kuzitafuta,maana zenyewe ni matokeo ya mahusiano yetu na Mungu wa Baraka

5.      SAFARI YA KURUDI BETHELI INATUUNGANISHA NA KUSUDI LA MUNGU JUU YA MAISHA YETU:

MWANZO 35: 9-13 –Yakobo alipoanza safari ya kwenda Bethel na kurudisha uhusiano wake wa karibu na Mungu,kusudi la Maisha yake liliunganishwa na kuthibitishwa na Mungu,Hatima yake na future yake iliwekwa wazi na Mungu,Mpango wa Mungu juu ya Maisha yake uliwekwa wazi tena na kuthibitishwa na Mungu.Mungu aliweka wazi nini amekusudia kufanya katika maisha yake.Tunapokuwa na maisha ya ukaribu na Mungu tena Mungu ataweka wazi nini amekusudia kufanya katika maisha yetu,Future yetu Huwa dhahiri.

 SAFARI  YA KURUDI  BETHEL INA WAVUTA NA KUWAHAMASISHA WENGINE KUMFUATA MUNGU WA BETHEL

MWANZO 35:6,Yakobo alipoanza safari ya kwenda Betheli kurudisha uhusianao wake na Mungu na kujenga tena Madhabahu, Watu wengine alikokuwa nao walihamasishwa na kuvutwa kumfuata katika safari ya kwenda Betheli,

Tunapoamua kumfuata Mungu wa Betheli wako watu ambao nao watavutwa kupitia sisi,ukaribu wetu na Mungu katika Maisha yetu unawezakuwavuta watu wengine kutaka kumtafuta Mungu pia,Watu walio karibu yetu wanao

tuzunguka,majirani zetu,wafanyakazi wenzetu,waamini wenzetu,watumishi wenzetu n.k wanaweza kuvutwa na kuhamasishwa pia  kutufuata Betheli.

7.      SAFARI YA  KURUDI BETHEL INALETA UPATANISHO NA WATU WA MUNGU:

MWANZO: 35:8,Safari ya Yakobo kwenda Betheli iliwaunganisha tena familia ya Isaka,na kuleta upatanisha,tunaona Debora mlezi wa Rebeka Mama yake Yakobo anatajwa,hapa,Debora alikuwa ni kama Mama yake Yakobo baada ya Rebeka Kufariki,tunaona familia ikipatanishwa na kuunganishwa tena bethel.

Bethel ni kurudi tena katika familia na ushirika wa watu wa Mungu, Bethel mahusiano yanatengenezwa upya. Ukaribu wetu na Mungu unatengeneza mahusiano yetu na watu wengine.

8.      SAFARI YA KURUDI BETHELI INALETA UAMUSHO NA MAREJESHO

MWANZO 35:7, 9,14-15

Yakobo  anatokewa tena Mungu,Mungu anaendelea kusema naye,ukaribu wake na Mungu umerudi kwa nguvu ,anajenga madhabahu upya ile aliyoijenga miaka 20 iliyopita,anatoa sadaka,anaabudu huu ni uamusho katika maisha yake,na marejesho.Kurejesha uhusiano wa Karibu na Mungu kunaleta tena Uamusho na Marejesho,Moto wa Roho unawake tena ndani yetu,Nadhari zinafanywa upya,viapo vinafanywa upya,UTII wa Amri za Mungu unarudi tena, kunakuwa na kujitoa upya  tena na kujiweka wakfu upya kwaajili ya Mungu,Sauti ya Mungu tunaisikia na kuielewa kwa urahisi.

 Hitimisho:                                                                                     Pengine umekaa shekemu maili 30 toka Betheli,Mungu anakutaka usonge mbele ufike Betheli, lipa  gharama ya kwenda mbele zaidi kiroho,lipa gharama ya kuongeza viwango vyako vya kirioho.ni kweli unaabudu,unamahusiano na Mungu lakini,ukiwa SHEKEMU,Mahusiano yako na Mungu si ya kina,ni ya mbali sana ,una madhabahu, lakini umeijenga Shekemu na siyo Betheli,Mungu anataka uanze safari ya kwenda Betheli leo,Mahali ambapo utatengeneza mahusiano yako na Mungu upya,utakuwa karibu naye tena, utapoona uwepo wake tena, utapoona utisho wake tena,Mahali`utapojitoa wakfu upya,mahali amabapo utafanya maagano naye upya na kumwabudi katika madhabahu iliyo mahali sahihi.Betheli itabadilisha maisha yako hautabaki vile ulivyo tena.

Mungu akubariki unaporudi Bethel yako!

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

3 Responses to WITO WA KURUDI BETHELI YAKO

  1. Anthony Mwenda says:

    uBARIKIWE SANA mCHUNGAJI MTITU. AMENI NIMEPITIA HARAKAHARAKA NITARUDIA TENA SOMO ZURI SANA LINASAIDIA SANA.

    Like

  2. Elias says:

    Mungu wa amani nyingi akubariki kwa kazi njema! Kwani somo limegusana maisha yangu hakika Bwana azidi kuikuza kazi hii na kukuinua zaidi katika utumishi ulioitiwa./

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s