Ev.Moses Kapaya anena juu ya watumishi Feki

Wakati fukuto la kuvuma kwa watumishi Feki, Mwinjilisti Moses Kapaya Mayila naye afungua kinywa. Alipoulizwa na mwandisi wa blog hii kuhusu watumishi feki Moses alisema “Unajua watu wengi watajikuta Jehanamu kwa Dhambi ambazo hazikuwastahili! Nimekuwa nikisikia watu wakisema Mchungaji flani ni freemason, mtumishi flani anatumia nguvu za giza. Nimeona watu wengi wakihangaika sana na hali hii.
Biblia iko wazi imesema mtawatambua kwa matunda yao, Matunda ni mazalia yatokanayo na uhalisia wa mtu. kwa maana nyingine ni kwamba mtawatambua kwa mafundisho yao. lakini suala la mtu kumtambua kwa mafundisho yake linahitaji msaada wa Mungu na pia uzoefu mkubwa katika neno la Mungu, maana Biblia inasema Malaika wa Shetani nao pia hujigeuza kuwa kama malaika wa Nuru (Mungu).

Sasa ili nikusaidie usichanganywe na mambo haya, wewe usipoteze muda wako kumkagua mtumishi wa Mungu kwamba huyu ni mtumishi wa Mungu kweli au anafanya janja janja. Suala la kumchunguza mtumishi si kazi yako ni kazi ya Mungu mwenyewe. hivyo wewe unatakiwa kumwamini kila mtu asemaye kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu! kama anadanganya basi siku hiyo ya mwisho utamuuliza pale mlango (Ndugu wewe si tulikuwa pamoja kumbe wewe mwenzetu ulikuwa ukituzunguka?)

Nakuambia kweli mtu wa Mungu usijichumie dhambi isiyokustahili. Yesu alikuwa akitoa mapepo kwa Nguvu za Roho Mtakatifu watu wakasema anatumia Baalzebuli mkuu wa mapepo. Yesu alisema Dhambi zote watasamehewa wanadamu lakini dhambi ya kumkufuru Roho wa Mungu hawatasamehewa, inamaana kwamba wale watu walikufuru kwa kusema kwamba Yesu anatumia Nguvu za Shetani kutoa mapepo. Hivyo dhambi zao hazitasamehewa, sasa nakuonya na wewe usije sema mtumishi flani anatumia nguvu za shetani hali yakuwa kumbe mtumishi huyo anatumia nguvu za Roho Mtakatifu! wewe mwamini tu asilimia zote siku hiyo atajulikana wala haitakudhulu wewe.”

Mimi naweza kusema kuwa Moses ameongea Point sana kiasi kwamba kila mtu mwenye busara zake atakubaliana naye.

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s