Ili mambo yako yafanikiwe ni lazima ukae ndani ya Yesu!

Yesu alisema “Kaeni ndani yangu nami ndani yenu, kama tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, maana nyinyi bila mimi hamwezi jambo lolote.”

Haleluya. Haya ni maneno mazito sana kama ukiyatafakari katika hali ya ndani zaidi. lakini ukiyatafakari katika hali ya juu juu tu, utayaona kuwa ni maneno ya kawaida tu! Hebu tuangalie pale aliposema “Maana ninyi bila mimi hamwezi jambo lolote” Kumbe katika kukaa na yesu ndipo tunawezeshwa na yeye kuyatenda mambo yote, hata umasikini huu kumbe tusipokaa na Yesu hatutaweza kuuondoa, na ndiyo maana mtu mmoja kwenye Biblia anajivuna akisema “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu!” Huyu jamaa aligundua siri ya uwezo wake ya kuwa yuko amwezeshaye!

Magonjwa uliyonayo usipokaa na yesu hutaweza kuponywa maana wewe bila Yesu kumbe huwezi jambo lolote! halafu anasema “Kama tawi lisivyoweza kuzaa peke yake” Unajuwa Tawi bila shina haliwezi kusimama, kwa hiyo mafanikio ya tawi yanategemea shina. vivyo hiyvyo kristo naye ametufananisha sisi na tawi wakati yeye akijifananisha na shina, kwa maana nyingine sisi (Matawi) bila Kristo (Shina) hatuwezi kufanikiwa wala kusimama!

Mkabidhi Bwana njia zako zote leo ili akuwezeshe katika mambo yako yote, Biblia inasema “Mkabidhi Bwana njia zako naye atakupa yale ambayo moyo wako unayatamani.”

Bwana Akubariki mtu wa Mungu.

Ev.Moses Mayila

New Hope world wide ministry

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

2 Responses to Ili mambo yako yafanikiwe ni lazima ukae ndani ya Yesu!

  1. kone sailepu says:

    kweli kabisa bwana mosse neno lako limenigusa mungu akubariki sana mtumishi

    Like

  2. sarah kayange says:

    mungu akubariki sana

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s