Safari yetu Rwanda tumerudi jana

Safari yetu Rwanda tumerudi Jana, tumefurahi sana kuwepo Rwanda tulipokelewa kwa shangwe na wenyeji wa mji wa kigali usiku wa tarehe 06/12/2012. Pia wametuaga kwa furaha huku wengine wakitutaka tuendelee kukaa huko. Bwana awabariki watu wote walioshughulika kutuhudumia tulipokuwa Kigali.

Tulitembelea sehemu za historia ya Mauaji za Genocide ambapo tulijionea mafuvu ya watu waliouawa pia tuliona miili ya watu ikiendelea kukusanywa hadi hivi leo. Tuliona mifupa ya watu. tuliona siraha zilizotumika kutekeleza mauaji hayo yakiwemo mapanga, marungu na Bunduki. pia tuliona makaburi matatu ambayo ndani yake walizikwa watu 259,000 wakati kaburi la tatu bado halijajaa kwa hiyo bado wanaendelea kuweka maiti za watu, litakapojaa litafunikwa. Kaburi hilo bado liko wazi na ukiangalia ndani utaona maiti nyingi zimelazwa humo. ni jambo la kusikitisha sana. Ila Bwana atawarehemu waliofanya hayo!

Photo-0073

Waimbaji wa Kwaya ya kanisa la Kilutheri makao makuu Mjini Kigali wakimwimbia Bwana siku ya Tarehe, 9/12/2012.

Wahubiri wa Mkutano huo walikuwa Ev.Moses Mayila na Ev.Danford Kidosi, Kidosi alishusha mvua ya Baraka siku ya Mwisho ya mkutano katika Ibada ndani ya Kanisa la Kilutheri makao makuu nchini humo, ambapo Injili ilimgusa kila mtu.

Wakati huo huo jioni kwenye mkutano Moses aliwasha moto wa Injili hadi speaker zikashindwa kuhimili sauti kuu ya mwanaume huyo, Moses ni mhubiri anayetumia nguvu nyingi sana awapo jukwaani lakini hata hivyo sauti yake huwa haigomi, Askofu mkuu msaidizi wa kanisa la Kilutheri nchini Rwanda alimuuliza Moses kesho yake mara baada ya kuhubiri siku ya Kwanza “Vipi Sauti?” Moses alimjibu “Iko swa”. lakini kwa haya yote lishukuriwe jina la Bwana Mungu wa Majeshi. Amina

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s