Kikwete alikwepa tamko la maaskofu Tanzania

Katika hotuba ya jana ya tarehe 31/03/2013 ya Rais kikwete alipokuwa akizungumzia kuhusu suala la waislamu na wakristo nchini. Katika walaka wa tamko la maaskofu walidai kwamba serikali igawe mabucha yawepo ya wakristo na waislam, pia waliitaka serikali itamke kama imeshindwa kuwalinda wananchi wake pamoja na mali zao, na hii ilikuja kutokana na mauaji dhidi ya viongozi wa kikristo na vitisho dhidi ya wakristo vinavyoendeshwa na baadhi ya waislamu.

Raisi alikataa mambo hayo yote. alisema Serikali haijashindwa kuwalinda wananchi wake wala mali zao! pia suala la kugawa machinjio na mabucha kikwete alidai kuwa haiwezekani, maana italazimu kuweka majiko mawili mashuleni ya waislamu na ya wakrito, vivyo hivyo jeshini pia; suala ambalo yeye alisema haliwezekani, hivyo alisema kwamba tuvumiliane tu!

Mimi naweza kusema kwamba kikwete alisema hivyo kwa sababu yeye ni mwislamu! suala la kutuambia wakristo tuvumilie kula nyama walizochinja waislamu halitawezekana tena hata kidogo! hapo mwanzo tulikubali kula kwasababu tulikuwa hatujuwi kama waislamu kuchinja kwao ni ibada! lakini sasa kwa kuwa wametuambia hayo hatuwezi kula! Biblia imetuzuia kula nyamba zilizotolewa katika ibada za miungu!

Kwa hiyo kututaka tule nyama hizo ni kinyume cha imani yetu, jambo hili haliwezekani! sisi tunamwomba Rais atumie busara ya utawala, maana mzozo huu unasababisha vurugu na hata vifo! angalie madhara ya kugawa majiko mashuleni na jeshini. Kisha aangalie madhara ya kuendelea kuwepo kwa vurugu kama hizi! sio kwamba tunafurahia tunavyoona vurugu zinaendelea nchini, hatupendi hata kidogo, isipokuwa tunatafuta namna ya kuzikomosha hizi vurugu. Kikwete aangalie mbona makaburi tunatofautiana. bado tutaendelea kumwambia rais angalie upya juu ya hilo, japo wenzetu maaskofu wamedai kwamba watatafakari upya uhusiano wao na serikali, lakini mimi nawaomba maaskofu kabla hatujafikia huko hebu tujadili kwanza na serikali kwa mara nyingine tena! tuangalie athari za reaction zetu kwa jamii yetu!

Ninachowaomba wakristo kwa sasa kabla jambo hili halijatatuliwa, msiinue vurugu yoyote kaeni kimya msubiri muafaka wetu na serikali. Ninachowataka ni kwamba msile nyama iliyochinjwa na waislamu kwani ni kinyume cha maagizo ya Mungu wetu.

Bwana wasaidie sana!

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

9 Responses to Kikwete alikwepa tamko la maaskofu Tanzania

 1. shekeli says:

  Bwana Mungu wetu anasema
  “kiingiacho hakimtii mtu unajisi bali kitokacho…”
  kwa hiyo hakuna ubaya kula nyama iliyochinjwa na ndugu
  zetu waislam labda tuwe tunataka vurugu tu.
  “sisi si wa mwili bali ni wa roho”
  Hatuendi mbinguni kwa kula na kunywa bali kwa kujitia nira ya Bwana na mwokozi wa maisha yetu ambaye alikuwa mpole na mnyenyekevu
  HAYO TU!

  Like

 2. kivuyo says:

  Bwana Yesu asifiwe,
  kwa kweli tusifanye mambo yakawa ya ajabu ,kwa sababu kama Rais alivyosema tukifanya hivyo tutashindwa kukaa pamoja ,mimi nakubali kama mwenzangu alivyosema kiingiacho hakimtii mtu unajisi bali kitokacho na “sisi si wa mwili bali ni wa roho” basi tukae kimya, ikiwezekana tuwe kama Daniel kwamba kwa imani yetu hatuli nyama iliyochinjwa na ndugu huyo, basi na usile becoz hutapungukiwa chochote ,ila ukisema nitakiombee kwa imani basi fanya hivyo maana hata maaskofu hawakusema ule au usile
  jamani uamuzi ni wako

  Like

 3. mhina says:

  mimi nawaunga mkono wachangiaji walionitangulia,lakini pia ningependa kumletea mleta maada hii tafakri zifuatazo: Wakristo tunapokula mezani na familia zetu,huwa tunakuwa na utaratibu wa kukibariki,kukiombea na kukitakasa chakula pale mezani…sasa ndugu yangu wewe,je huwa hufanyi hivyo? Na kama unafanya….je huwa humuamini mwenyezi mungu kuwa amekwisha kitakasa chakula kile pamoja na finyango zote za nyama unazozipeleka mdomoni mwako?…Mimi ninavyoamini ni tofauti sana na mitazamo ya wakristo aina hii na pia nimeona kuwa elimu ya biblia na imani yake ikikukaa sana kwa kiwango chake…haiwezi kukuleta wala kukushauri kufanya au kuchukua hatua hizo za kimwili.Sasa kama ni kweli upendo ni utimilifu wa sheria zote za mungu tena ni sheria kuu ya sisi wakristo,hebu sasa tafakari wewe mwenyewe kutakuwa na upendo gani wa mungu wakati kaka bakari mtaani kwangu anauza nyama eti nipite na kwenda kununua mtaa mwingine kwa bwana john eti kwa kuwa yeye ni mkristo mwenzangu..hivi tutajenga jamii au tutabomoa jamii?…huoni kuwa hapo vitafuata na vitu vyengine kususiana na kubaguana eti kwa sababu ya dini zetu? Hivi tukifuata mawazo kama hayo ya jazba zisizo na tafakari sahihi tutakuwa kweli sisi ni wakwake kristo au wakristo? Tena naomba unipe jibu…hivi mababu zetu wote huko nyuma waliokula nyama zilizochinjwa na waislamu watakua wako jehanam kwa sababu ya nyama zile?SI KWELI KABISA HUYU NI IBILISI ANAETAKA KUARIBU KANISA LA MUNGU KWA KUJIFANYA MUELEVU NA MTETEZI WETU…Kwasababu neno la mungu liko wazi sana katika mambo yanayo husu mwili.Biblia inatufundisha kuwa mambo yote yanayohusu mwili na sheria zake mwisho wa mtu anayeyafuata na kushindana na hayo ni DHAMBI NA MAUTI!…Ndiyo maana huko juu nilionyesha na kuelezea hatua za ibilisi zinavyoingia kwa wakristo kwa uelevu wa uongo kwa kutumia maandiko ili KUTUPOTOSHA TUSIFIKE NCHI YA AHADI…Biblia yatuambia: ‘SASA BASI, HAKUNA HUKUMU YA ADHABU JUU YAO WALIO KATIKA KRISTO YESU KWA SABABU SHERIA YA ROHO WA UZIMA ULE ULIO KATIKA KRISTO YESU IMENIACHA HURU MBALI NA SHERIA YA DHAMBI NA MAUTI,Soma (warumi 8:1-3).Ndugu zangu wakristo ni kwamba mambo ya sheria na kudai haki fulani fulani za kimwili tayari yalikwisha isha pale msalabani na YESU KRISTO NDIYE HAKI YETU.Tusijaribu kushindana na watu wa mwili katika ulimwengu huu wa mwili kwa sababu sisi sasa tu wadeni wa Roho na wala si wa mambo ya mwili tena kama ni kweli tunataka tumtii bwana yesu.soma(warumi 8-12-16).Neno la mungu linafundisha hivi:MSISHINDWE NA UBAYA BALI MUUSHINDE UBAYA KWA WEMA…Sasa hebu fikiria,utakuwa mkristo gani wewe unaeshindana na ubaya pamoja na kuishi kwa maisha ya ubaguzi na hofu tele!!…ni kweli sikatai kwamba kunabaadhi ya mambo ambayo tunaweza kuyatetea lakini nauliza hivi ili la kuchinja limo katika katiba na sheria za nchi kwamba wachinje waisilamu tu? Na kama halipo kisheria yani liko huru…sasa tunachoilaumu serikali ni nini?kwanini sisi wakristo tusinge hangaikia kuunganisha mathehebu yetu tukawa nguvu moja katika yesu kristo badala ya kuminyana kwenye mabucha kugombania kuchinja kitoeo?…mwataka tufikie hali ya kukaribishana kwenye mialiko na kuuliziana, nyama hii kachinja padre, askofu au imamu,shekhe?…hakika hayo si mafundisho ya bwana yesu bali huko ni sehemu ya yule mpinga kristo anaeendelea mpaka ndani ya kanisa akiwanasa watu wa mungu kwa uerevu wake wa uongo kama alivyotumia maandiko kutaka kumnasa bwana yesu kwa kutumia maandiko hayo hayo ya mungu…lakini bwana yesu yeye alimtambua akamshinda kwa sababu alikua anaasili ya mungu na neno lake… yani MWANA WA MUNGU….Sasa wakristo wenzangu hebu jiulizeni,je na nyinyi ni watoto wa mungu na mnaasili ya mungu kama bwana yesu au bado hamjakomaa kwa mambo ya rohoni huku bado mkiwa mnapita ile njia pana badala ya nyembamba?TUTAFAKARINI WOTE HAYA NILIYOYAANDIKA MAANA ROHO NDIYE ALIYENITUMA!!.Mbarikiwe wote.

  Like

 4. DONALD S.L. says:

  mhina we mwisilamu unatumia vifungu vya Biblia pasipo inaonyesha unasoma huelewi HUWEZI KULA zilizotolewa sadaka kwa….

  Like

  • Lispa says:

   jamani ndugu DONALD,
   tuwe makini na manabii wa uwongo maana ishasemwa watawalaghai wengi kwa jina la Bwana;” HUWEZI KULA zilizotolewa sadaka kwa….” jamani hii ni agano la kale km kweli unampenda Kristu alitufia msalabani ili atukomboe na laana ya torati, sasa mbona mnataka kuturudisha kwenye mambo ya kimwili ya torati na hali tushakombolewa?
   TUTAFAKARI JAMANI TUACHE USHABIKI MAANA HATA RWANDA WALIANZA HIVIHIVI.

   Like

 5. DONALD S.L. says:

  mhina unashangaza huwezi kula nyama iliyotolewa sadaka kwa shetani hiyo niiliyosongolewa hata ungeomba umekula haramu

  Like

 6. mhina says:

  Kaka Donald…nakuomba uisome injili tena kwa umakini ili ujitambue ulipo na wajibu wako mbele za mungu.Unaonyesha imani yako bado ipo chini sana!!…unadiriki kusema kuwa hata mungu akikitakasa kitu haisaidii bado ni haramu tu!!…umeokoka kweli wewe au bado unashika mapokeo ya kanisa lako?….KWANINI NGUVU ZA SHETANI ZINAKUTAWALA KIASI HICHO KWENYE IMANI YAKO KULIKO NGUVU ZA MUNGU?…Sasa niseme na wewe kuwa Mungu tunaemuabudu sisi wakristo amejaa huruma na neema haoni hasira upesi tena ni mwingi wa fadhili.Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi kadiri ile rehema yake ni kuu kwa wamchao.Yeye amemfanya yesu kristo HEKIMA,HAKI , UTAKATIFU NA UKOMBOZI….Kusudi kama maandiko yanavyotufundisha yakituambia’YEYE AONAE FAHARI NA AONE FAHARI JUU YA MUNGU.Kwa hiyo ndugu donald mafundisho yote ya bwana yesu aliyotufundisha ni juu ya upendo kwa mungu na jirani zetu.Biblia inatufundisha wakristo wa kweli hivi:’BASI KWA KUWA MMEKUWA WATEULE WA MUNGU,WATAKATIFU WAPENDWAO JIVIKENI MOYO WA REHEMA,UTU WEMA,UNYENYEKEVU,UPOLE,UVUMILIVU MKICHUKULIANA NA KUSAMEHEANA,MTU AKIWA NA SABABU YA KUMLAUMU MWENZAKE KAMA BWANA ALIVYOWASAMEHE NINYI VIVYO NA NINYI ZAIDI YA HAYO YOTE JIVIKENI UPENDO NDIYO KIFUNGO CHA UKAMILIFU.Soma(wakolosai 3-12-14).Kwa hiyo ndugu donald hayo wakristo ndiyo tuliyoitiwa hapa duniani siyo chuki na vurugu!!..ukijenga chuki kwa jirani,uhasama na mashindano yoyote ya mambo ya mwili basi ujue kuwa huo siyo ukristo bali ni MAPOKEO YA DUNIA.Biblia inatusisitizia’ENENDENI KWA HEKIMA MBELE YAO WALIO NJE MKIUKOMBOA WAKATI MANENO YENU YAWE NA NEEMA SIKU ZOTE YAKIKOLEA MUNYU MPATE KUJUA JINSI IWAPASAVYO KUMJIBU KILA MTU.Sasa hapa ndugu donald kwa vyovyote vile utatambua kuwa msingi wa wakristo wote ni AMANI NA UPENDO…ndiyo maana ukaona nilijaribu kuondoa jazba za baadhi ya viongozi wa kanisa kwa kuwa hata wao ni wanadamu nao hujisahau wakati fulani.Mambo ya vyakula na unajisi wake tunawaachia watu wa mwili wasiyoijua kweli ya mungu mpaka leo kwa kuwa sisi ni wateule wa mungu,tupo katika njia halisi ya mungu tukishika sheria yake ndani ya mioyo yetu na wala siyo kushika mambo ya mwili na kuanza kujenga chuki,uhasama na ubaguzi…HAYO SIYO MAFUNDISHO YA BIBLIA…Tukifuata busara hii ndugu donald ndipo tutakapokuwa wakristo wa kweli wa agano jipya aliloliahidi mungu mwenyewe kupitia nabii yeremi tukiachana na mambo ya torati ile ya musa ya kimwili zaidi kuliko roho za watakatifu.soma(yeremia 31:31-34).

  Like

 7. joseph says:

  Jamani suala hili ni gumu hasa pale lilipoanza kugusa imani.mi nawaomba wote tuwe watulivu na tuombe kwani kwa nguvu zetu litatushinda.lakini tukilipeleka kwa Mungu litapata majibu.

  Like

 8. DONALD SL says:

  MUNGU alisema tusile iliyotolewa sadaka kwa shetani inatosha we unayetetea kwa kupindisha sikuelewi kabisa.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s