Mwambie Mungu atatue chanzo cha tatizo lako!

Biblia inasema “Ndipo watu mji ule wakamwendea Elisha, wakamwambia; angalia twakusihi mji huu ni mzuri kama Bwana wangu aonavyo; lakini mji huu huzaa mapooza na maji yake ni machungu. Ndipo elisha akawaambia nileteeni chombo kipya mkatie na chumvi ndani yake, wakamletea akachukua kile chombo na le chumvi kisha akaenda kuimwaga kwenye chemchemi za maji, kisha akasema; Bwana asema hivi; hapakuwa tena na kuzaa mapooza wala maji machungu.”

Hapa tunajifunza jinsi Mungu alivyo uponya ule mji; yamkini na wewe biashara zako zinazaa mapooza yaani hakupati faida katika hizo biashara! yamkini ndoa yako inazaa mapooza, yamkini tumbo lako linazaa mapooza, kila ukichukua mimba inaharibika! yamkini watoto wako wamekuwa mapooza, hawakusikilizi, hawapati kazi.

Mwambie Mungu nahitaji unifanyie chombo kipya kama na chumvi. kisha wambie aiweke hiyo chumvi kwenye chanzo cha tatizo lako, maana Elisha aliweka chumvi ile kwenye chanzo cha maji, kwa hiyo Elisha kama angeweka ile chumvi kwenye maji; maji yangeponywa yale tu yaliyowekewa chumvi lakini yale ambayo yangekuja baadae baad ya hayo yenye chumvi kuisha yasinge faa kitu. ndiyo maana Elisha akaweka chumvi kwenye chanzo cha maji ili kutibu mfumo mzima wa maji. na wewe ili kutibu tatizo zima usiombee tatizo liishe tu bali taka sana kitatuliwe kile chanzo cha tatizo. ni sawa na mgonjwa wa ukimwi leo akiugua homa atakwenda hospitali atapewa dawa atapona. lakini kwasababu hakuponywa ukimwi kesho tena atapatwa na homa nyinge! Bwana akusaidie mtu wa Mungu.

Ubarikiwe sana!

Ev.moses Mayila
newhopeministrytanzania@gmail.com

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

2 Responses to Mwambie Mungu atatue chanzo cha tatizo lako!

  1. Ikaya Moses says:

    NAshukuru sana kwa mafundisho, Mungu awabariki.

    Like

  2. Messo says:

    Nabarikiwa na mafundisho yako,,endelea

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s