Kanisa lashambuliwa kwa Bomu Arusha! baadhi wauawa wengi wajeruhiwa!

majeruhi 2

MAJERUHI (4)Bomu limelipuka majira ya saa 5 leo asubuhi katika uzinduzi wa Parokia mpya ya Olasiti, Jijini Arusha wakati Askofu Mkuu Josephat Louis Lebulu na Balozi wa Baba Mtakatifu nchini, Askofu Mkuu Francisco Montecillo Padilla wakiwa wamejiandaa kuanza maadhimisho ya misa ya kutabaruku kanisa hilo kwa kuwabariki waumini hao tayari kwa ibada.

Taarifa za awali zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas zinasema kuna majeruhi zaidi ya 30, lakini wanne walikuwa na majeraha makubwa, na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kuweza kuwabaini waliorusha na/au kutega bomu kwenye eneo hilo la Ibada.

Akiahirisha Ibada hiyo Vicar General wa Jimbo Katoliki la Arusha Padre Simon Tengesi aliwataka wakristo wote kuondoka eneo hilo na uzinduzi huo umeahirishwa hadi pale itakapotangazwa tena, na watu wameondoka eneo hilo ili kuruhusu vyomvyo vya ulinzi na usalama viweze kuanza uchunguzi.

Chanzo chetu cha habari kinasema eneo lilipolipuka bomu kuna damu nyingi na watu wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s