Tanzania tutafakari uhusiano wetu na Rwanda!

Tanzania-RwandaUhusiano kati ya Rwanda na Tanzania unazidi kuwa mmbaya kila kukicha, huku vyombo vya habari vya pande zote mbili vikizungumza kwa kauli kali zinazochochea kuwepo vita!

kauli za Rais kagame zimekuwa sio nzuri sana kwa Rais Jakaya kikwete, nadhani hii ilikuja mara baada ya Kikwete kumshauri Kagame kuwa afanye mazungumzo ya amani na waasi.

Kumekuwepo na taarifa nyingi zenye kauli kali kupitia vyombo vya habari vya nchi hizi mbili. Huku kila upande ukijipiga kifua kwamba unajiweza kivita dhidi ya upande wa pili!

Lakini ndugu zangu hebu tufikirie kama watu wenye busara! Madhara ya vita yalivyo mabaya! Hebu sisi tulioko Rwanda tufikiri na tukumbuke jinsi mauji ya 1994 yalivyokuwa! na sisi tulioko Tanzania hebu tufikiri hofu iliyotanda wakati wa Idd Amin! Hebu tuwaangalie watoto wetu, Je! vita vikianza watapona? Viongozi tunaweza kukimbia nje ya nchi zetu, lakini je! ndugu zetu watakimbilia wapi?

Tukumbuke Kwamba hakuna vita visivyo na athari! na kama tukilifahamu hilo, kwa nini tupigane? sisi ni majirani, pia sisi tulipendana sana hapo mwanzo. Tanzania ilifanya jitihada nyingi kurejesha Amani Rwanda, lakini leo kama tukigana na Rwanda, Jitihada zetu zote zitakuwa bure! jamani hebu tukumbukeni tulivyopendana! Nawaomba upendo wetu usiondoke!

Nakumbuka mwezi december mwaka jana nilikuwa Kigali kwajili ya Injili, tulipokelewa kwa shangwe na watu wa Rwanda, na hata tulipokuwa tukipita mitaani wananchi walisimama na kutupungia mikono tukiwa katika gari letu! hii inaonyesha upendo wa hali ya juu sana. lakini leo iweje upendo huu uondoke tuanze kupigana risasi bila huruma tena?

Nawaomba viongozi hawa (Rais kagame na Rais Kikwete) waombane radhi juu ya haya mambo, wao ni wanadamu hakuna aliye kamili walitambue hilo kisha wasameheane. Na kwa niaba ya Rais Kikwete namuomba msamaha Rais Kagame kwa kila jambo ambalo lilimkwaza kutoka kwetu! naomba turudishe uhusiano wetu tena kama zamani!

Mungu ibariki tanzania, Mungu ibariki Rwanda, Mungu Dumisha Amani kati yetu!

 

Ev.Moses MayilaNew hope ministry

newhopeministrytanzania@gmail.com

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s