Mateso yanayokwenda kulikumba kanisa katika nyakati hizi za mwisho!

Ndugu wapendwa nisingependa mkose kuijua siri hii! ya kwamba hizi ni nyakati za mwisho Bilblia inasema kanisa litaingia katika mateso makali!

Itakuwa hapo mateso yatakapoanza kulikumba kanisa, hayawezi kuja tu kutokea kusikojulikana lazima kuwepo na chanzo cha hayo mateso. Ili nchi iyumbe lazima uchumi wake uwe mmbaya! na maisha ya mtu ili yayumbe lazima uchumi wake uwe mmbaya! nchi haiwezi kuyumba kama uchumi wake uko vizuri! Marekani alipokuwa na uchumi mzuri aliweza kuendesha operation za kijeshi katika nchi nyingi sana, lakini baada ya uchumi kuharibika Rais Barack Obama ameanza kuondoa vikosi vyake katika baadhi ya field!

Na haya mateso ya Kanisa ili yafike ni lazima uchumi wa dunia uyumbe! sera ambayo shetani anaitumia kuvuruga uchumi wa Dunia ni mikopo. Wale watu walikaa wakaona kwamba ili tuweze kuwavuruga ngoja tuwapelekee mikopo! watu wanakuja kwako mikono nyuma wakiwa wapole wakikushauri kukopa katika taasisi zao! wanakupa na mchanganuo wa biashara kiasi kwamba utajiona mwenyewe kuwa umekwisha tajirika tayari!

Ukishachukua mkopo huo wanakugeuka ghafla wakija hawawi wapole tena kama zamani, watakuja wakiwa wakali hawataki suluhu wala kusikiliza matatizo yako, watachukua nyumba yako na vitu vyako kisha wataondoka wakikuacha bila kitu kuliko hata walivyokukuta!

Hivyo badala ya kuleta maendeleo unajikuta kwamba wanasababisha umasikini mkubwa katika maisha yako! watu wengi sana wanalia na hii mikopo!

Biblia katika kitabu cha Ufunuo 13:16-17 inasema..

16  Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;

17  tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake

Sasa hapa soma kwa makini uone jinsi gani watu watatiwa hii chapa! Zamani tulikuwa tunasoma imeandika siku za mwisho watu watakuwa wanazungumza na chuma na inawapatia fedha! tulianza kubisha na kusema huu ni uongo, chuma itaongea namna gani? na itanipatia fedha namna gani?

Ukiangalia hivi sasa wameleta hizi ATM machine. Ukifika katika hizi mashine unaweka kadi yako kisha mashine inakwambia “Weka namba ya siri” inakuuliza “Lugha gani” Unabonyeza lugha unayotaka, kisha inakuuliza “unataka pesa kiasi gani” unaweka kiasi kisha inakupa pesa inakuandikia na risiti!

Sasa kitakachofanyika hapa ni kwamba, kutokana na wezi wa kimtandao wanaojulikana kama ‘ATM hacker’ ambao mtu anatumia bluetooth kutafuta namba yako ya siri. Itafika hatua watu wa mabenki watasema ili kukwepa wizi wa namna hii inabidi mtu awekewe namba yake ya siri kwa njia ya DNA au aweke kifaa kimoja kinaitwa micro cheap ndani ya ngozi yake kwenye paji la uso au mkononi ili mtu akifika tu kwenye ATM machine, hatahitaji tena kuweka namba ya siri bali atagusisha mkono au uso wake tu kwenye sensor na ile ATM machine itamsoma moja kwa moja! hivyo ndivyo itakavyokuwa katika zoezi la kutiwa chapa ya mnyama. jihadhari mtu wangu Shetani asikudanganye!

Tutaendelea tena week ijayo…..

Bwana akubariki sana!

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s