Leo tunataka tukushirikishe msingi wa SITA ambao ukiufuata katika maisha yako, utakusaidia uweze kuwa na uchumi mzuri sana.
Msingi huu wa SITA ni huu: Kadri unavyoijua tabia ya fedha,ndiyo unavyoweza ukashirikiana nayo vizuri zaidi, katika kuinua uchumi wako, vile vile bila kukuangusha kiroho!
Tabia ya 1: Fedha ya mtu na moyo wake vinakaa mahali pamoja, kwa kuwa fedha ina nguvu kuliko moyo wake. Hii kufuatana na Mathayo 6:21
Tabia ya 2: Fedha inamfuata yule anayejua kuitumia, na kuizungusha vizuri ili iongezeke; na fedha inamkimbia mtu yule asiyejua kuitumia na kuizungusha vizuri ikaongezeka. Hii ni kufuatana na Luka 19:12-22
Tabia ya 3: Fedha inampa mamlaka ya kiuchumi, ya kisiasa, nay a kiroho juu ya mji, mtu yule ambaye anawekeza kwa faida zaidi kuliko wengine katika mji huo huo. Hi ni kufuatana na Luka 19:15-26
Tabia ya 4: Fedha ina tabia ya kuwageuza wawe watumwa wake, wale wote wanaofanya kazi kwa ajili yake. Kwa hiyo usiitumikie fedha, ila fedha ikutumikie wewe. Hii ni kufuatana na Mathayo 6:24
Tabia ya 5: Ingawa Fedha ni chanzo cha ulinzi, lakini inaweza pia ikawa chanzo cha maovu. Hii ni kufuatana na Mhubiri 7:12 na 1 Timotheo 6:10.
Tabia ya 6: Fedha inataka iwe jibu ya maswali yote ya mtu, kwa hiyo jihadhari katika kuitumia usije ukamshukuru Mungu wako. Hii ni kufuatana na Mhubiri 10:19 na kumbukumbu ya Torati 8:12,13,18.
MUNGU AKUBARIKI.

Christopher Mwakasege – Mana Ministry
http://www.mwakasege.org

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s