Mateso ya kanisa siku za wisho!

Karibuni tena katika kituo chetu cha kujifunza maneno ya Mungu wetu.

leo nimekuletea mada ya muhimu sana! mada ni ya siku nyingi sana lakini ni ya muhimu sana kuifahamamu.

Hapa nitakudokezea tu lakini niko katika mchakato wa kuandika kitabu kizima cha mada hii ambacho kitakuwa bure kwa kila mwenye kuhitaji, hivyo weka order yako mapema!

Ngoja twende kwenye mada husika: MATHAYO 24:5-37 Biblia imesema habari za mateso ya kanisa siku za mwisho, lakini pia imetaja dalili za mateso hayo kuanza, imesema watatokea makristo wa uongo, taifa litaondoka kupigana na taifa jingine, kutakuwako njaa na matetemeko ya nchi mahali mahali. Pia watatokea manabii wa Uongo.

Mpenzi katika Bwana kila kona ya dunia sasa hivi haya mambo yapo, ikumbukwe yalitabiriwa miaka 1980 iliyopita na sasa yanatokea katika kizazi hiki. Siku hizi kila anayeanzisha kanisa, utakuta anajiita nabii, sisemi kwamba kila anayejiita nabii ni wa uongo hapana, bali baadhi yao ni waongo, siku zote ukiona kundi kubwa la ndege wakiruka angani na popo wamo! kwenye msafara wa mamba hakosi kenge.

Biblia imesema upendo utaondoka ndugu watasalitiana wenyewe kwa wenyewe. siku hizi utaona baba amezaa mtoto zeruzeru anakwenda kmtafutia soko ili amwuze achinjwe kisha yeye apewe fedha, na hii inatokea maana Biblia inasema watu katika siku hizo watapenda fedha kuliko kuwapenda wa kwao.

Ngoja nikulete kwenye kizazi tulichonacho kwa sasa. tumekuwa tukishuhudia mauaji ya kidini yanayoendelea karibu duniani kote ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya vikosi vya kiislam dhidi ya nchi ambazo zinashukiwa kuwa zinamfumo wa utawala wa kikristo, pia mashambulizi dhidi ya watumishi wa Mungu pamoja na wakristo wa kawaida, wauaji hao hudai kuwa wanapigania dini yao, kwa maana nyingine huwaua wakristo wakidhani kuwa wanatekeleza sehemu ya maagizo ya Mungu.

Baadhi ya mashambulizi hayo ni kama lile la sep.11.2001 nchini marekani lililofanywa na kundi la kiislam la Al-qaida, lingine ni lile la juzi juzi nchini kenya katika shopping mall ya westgate lilofanywa na kundi la kiislam la Al-shabaab ambapo waislam wote waliruhusiwa kuondoka kisha wasiokuwa waislamu waliuawa. mengine ni boko haram nchini Nigeria katika majimbo la yobe na damaturu.

Suala hili la kuuawa kwa watu wa Mungu limekuwa tishio duniani pote, wakati jumuiya mbali mbali za kikristo zikijaribu kulipinga lisiendelee, lakini mara kwa mara jitihada hizo hugonga mwamba.

Hofu kuu imetanda juu ya wakrito katika nchi husika ikiwemo Tanzania, huku wengine wakilazimika kusilim ili kukwepa kuuawa, lakini Biblia inasema “Yeyote atakaye kuipoteza nafsi yake kwa sababu ya mwana wa Adam ataiona na awaye yote atakaye kuiokoa ataipoteza” hivyo usisilim kwa sababu ya kukwepa upanga bali simama na Bwana atakutetea.

Biblia inasema Yohana 16:2 “Saa yaja atakapodhan kila mtu awauaye kwamba anamtolea Mungu ibada”

Hivyo watu hawa wanaoendesha haya mauaji dhidi ya wakristo duniani wanadhani kwamba wanamfanyia Mungu ibada, na imani yao ndivyo ilivyo, ndio maana utaona wanaua kwa vitu vidogo tu, utakuta jambo kama la mtu kuchinja kitoweo wao wanachukia na kuanza kumtafuta wamwue eti kwa sababu aliyechinja si mwislam, wakati kila mtu anatambua wazi kabisa kwamba kila mtu anahaki ya kutayarisha kitoweo!

Kuna wakati hadi unashangazwa na mambo ambayo wanaweza kufanya, mfano ni yule mtoto aliyekojolea kitabu cha dini yao, wao badala watambue kuwa aliyetenda jambo hilo ni mtoto badala yake wakaanza kumtafuta wamwue. unaweza kufikiri na kutambua kwamba chanzo hakikuwa mtoto bali walikuwa na sababu zao wenyewe ambazo ni kutafuta kuwaua wakristo ili wamfanyie mungu wao Ibada, kwa hiyo suala la yule mtoto lilikuwa kama chanzo tu cha kuamsha matakwa yao.

Ndugu zangu kanisa linakwenda kuingia katika mateso makali kupita kiasi. wakati huo mpinga kristo atakuwa alishachukua nafasi sehemu yote duniani, kwa sasa anajipenyeza pole pole japo bado kunaupinzani katika baadhi ya sehemu, huku nchi kama marekani ikisimama kama pembe ya kutetea haki za wanadamu duniani, lakini itafika sehemu marekani ataungana na mpinga kristo na atakuwa mstari wa mbele kulivuruga kanisa. ikisha kuwa namna hiyo sasa watu watalazimishwa kutiwa chapa usoni au mkononi ili iwawezeshe kununua na kuuza!

Labda nikueleze kidogo juu ya hii chapa jinsi itakavyokuwa! Zamani tulisoma kuwa siku hizo mtu atakuwa anaongea na chuma na ile chuma inampatia pesa, tulidhani mdhaha na hatukuamini kabisa maana hatukujua jambo hili. lakini siku hizi wameleta hizi ATM mtu anapofika pale akiweka kadi yake ile mashine inamwambia weka namba ya siri, kisha inamuuliza unataka lugha gani, anasema lugha anayotaka, kisha inamuuliza kiasi gani unataka anaweka kiasi baada ya hapo inampa fedha na kisha inamwandikia risiti.

Lakini baada ya hizi mashine kuja, wakajiokeza watu wenye taaluma inaoitwa IT yaani Information technology, wakaanza kuziiba hizi ATM kupitia software za bluetooth na zinginezo kama ATM Harker software. ambapo huchomeka kile kifaa kwenye machine ya ATM na kisha wanakaa sehemu na computer au IPAD kisha mtu anapokuja kutoa fedha kile kifaa kinapeleka taarifa zote kwa wale wezi, na wezi wengine hufunga kamera kwenye hizo ATM mtu akija kutoa fedha ile kamera hurecodi PIN CODE zake kisha baada ya hapo wale wezi hutafuta kadi yake na kwenda kutoa hizo fedha.

Ili kukabiliana na jambo hili, Itafika hatua watu wa Benki watasema sasa ili kulinda account za wateja wetu, badala mtu apewe PIN CODE basi awekewe code hizo kwenye mfumo wake wa DNA ili anapoingia tu pale Benki ile mashine imtambua moja kwa moja kuwa ndiye mhusika. unaweza kuona kama jambo hili haliwezekani, lakini chukulia mfano mdogo tu, kuna ile milango ya umeme yenye sensor, ambayo kama kuna mtu anakuja mlango huhisi na anapoukaribia hujifungua wenyewe. hii milango ipo Blue peal Hotel na TRA Mwenge dar es salaam.

Hivyo mfumo huu ndio utakaotumika katika uundwaji wa password za benki.

kuwa macho mtu wa Mungu Bwana atakushindia, tutaendelea na mada hii siku nyingine tena ni mada ndefu sana.

karibu tena.

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

One Response to Mateso ya kanisa siku za wisho!

  1. godfrey40261 says:

    mungu atusaidie kwa kutumwagia roho wa ke ili tuyatazame mambo haya kiroho zaidi.Maana kwaanaye potea injili kwake ni upuuzi,bali kwetu ni uzima wa milele

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s