New Hope Ministry (NHM) tutakuwa na mkutano Mwanza Feb.2014

SAM_0148Mwezi wa pili mwaka kesho (feb.2014) tarehe bado haijajulikana, unatarajiwa kuwa mwezi wa tofauti kwa wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake! kwani kikosi kizima cha NHM kutoka tanzania, kenya, Japan na Rwanda kitakutana pamoja ili kumlipua Ibilisi! watu waliofanywa mawindo, shetani amewafanya mateka lazima wataachiwa kwa jina la Yesu!

Kutakuwa na mkutano mkubwa wa kihistoria ambao utakumbukwa kila mwaka katika kumbukumbu za huduma hii. Nguvu ya Mungu itakwenda kuuatamia mji wa Mwanza kwa muda siku 40, mkutano utakuwa wiki nzima siku 7. Watu wengi wataponywa magonjwa sugu na ambayo si sugu! watu walioteswa na mapepo watafunguliwa, wako watu katika mji huo wamefungwa na wachawi, waganga na washirikina Bwana atawafungua katika hivyo vifungo kwa kishindo kikubwa!

Watu waliofungwa uchumi wao, kazi zao zimefungwa, na kuna watu wamewafungia wasipate kazi, wasifanikiwe, wasiweze kuzaa watoto, wasiolewe wala kuoa, na wengine wamefungwa akili zao. Bwana atawafungua kwa jina la Yesu!

Wako watu katika mji huu naweza kuwaona katika ulimwengu wa roho, wameolewa na majini, kila mara usiku wa manane hujisikia kana kwamba wanashiriki tendo la ndoa na hali hii huwapata mara nyingi wanapokuwa katika usingizi, na huwa inatokea mara nyingi wakiamka hujikuta na hali halisi kama kweli wamefanya tendo la ndoa. hilo ni jini huja kufanya ndoa na nao.

Pia naweza kuona kuna watu wasiokuwa majini ambao ni washirikina huwaingilia wanawake na mabinti usiku wa manane wanapokuwa wamelala! Hawa nao Bwana atawakomesha kabisa!

Watu wote wenye matatizo kama Haya Bwana anakwenda kuwafungua kwa Jina lipitalo majina yote (Yesu). huduma zote zitatolewa Bure katika viwanja vya furahisha barabara ya kutoka mjini kwenda uwanja wa ndege kabla ya kufika kona ya Bwiru. maandalizi yatakapokuwa tayari tutawajulisha tarehe ya kuanza.

Kama ukiguswa kushiriki Baraka za kuandaa mkutano huu, unaweza kuchangia chochote na Mungu atakubariki sana, maana Mungu humheshimu yeye apelekaye injili na pia humheshimu mtoaji! na kila atoaye ni lazima atabarikiwa maana amewekeza kwa Bwana. mkutano utagharimu Sh.milioni 8. Bwana akuguse kwa chochote ili tuweze kufanikisha kazi hii.

unaweza kuchangia kupitia bank:-

EXIM BANK (T) LTD
P.O.BOX 1431
DAR ES SALAAM
TANZANIA.

Account name: MOSES KAPAYA MAYILA
Account number: 5460997775
Swift code: EXTNTZTZ

M-pesa 0755 961 270

Tigo pesa 0715 961 270

Airtel money 0787 589 475

Ubarikiwe sana kwa Jina la yesu.

Mwanza sema Yesuuuuuuuuu!

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s