Siri za kufanikiwa kupitia kwa Bwana!

Haleluya!

karibuni tena katika kituo chetu cha neno la Mungu ili tujifunze pamoja, jina langu ni Moses Mayila.

Leo tutajifunza kuhusu somo tajwa, ‘SIRI ZA KUFANIKIWA’ Unajuwa kula kitu kina siri zake, na kila utawala unasiri zake, waliokuwa askri wanaweza kunielewa vizuri. kama ikitokea askari akatekwa vitani cha kwanza atakachoulizwa ni siri za jeshi la nchi yake. maana siri ndo kitovu cha mafanikio. vivyo hivyo Mungu naye katika ufalme wake kunasiri ambazo ameziweka ili mtu akizijua ni lazima atafanikiwa. Moja ya siri kuu kabisa katika zote ni UTII MBELE ZA MUNGU, yapili ni KUSAMEHE WALIOKUKOEA, ya tatu ni UTOAJI, na yanne ni MAOMBI.

Leo tutaanza na hii ya UTII MBELE ZA MUNGU, nadhani wengi wetu tunafahamu wazi kabisa kwamba Mungu huwapa neema wanyenyekevu na pia huwapinga wenye kiburi! (1petro:55) hivyo kama ukimtii Mungu utakuwa na nafasi kubwa ya kupokea neema ambayo ni kwajili ya wanyenyekevu wake!

hebu tuangalie vifungu hivi. Luka:5-8

4  Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki. 5  Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. 6  Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika; 7  wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama. 8  Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini pa Yesu, akisema, Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana. 

Hapa tunaona kuwa Simon alifanya kazi usiku kucha lakini hakupata kitu, na tukiangalia saikolojia ya kauli aliyoitumia kumjibu Yesu inaonyesha wazi kuwa Simon alijua kuwa hata kama akizamisha zile nyavu hadi kilindini lakini hataambulia kitu.

Ila kwa kumtii Yesu alilazimika kutweka nyavu vilindini, lakini dhamira ya Simon haikuwa kupata samaki ila ilikuwa kumtii Yesu. maana anasema “Tumekesha usiku kucha hatukuambulia kitu, ila kwa neno lako nitatweka” hii ni kauli iliyokwisha kata tamaa.

Yawezekana na wewe umekuwa kama Simon, umejaribu sana kutafuta mlango wa kuyakomboa maisha yako lakini haijawezekana, umefika hatua umechoka kama alivyokuwa amechoka simon kwa kazi ya usiku kucha na asipate kitu. pengine umetafuta sana kupata mtoto, kazi, mtaji, au elimu. Lakini mambo yanakwenda kinyume na ulivyotarajia! umefika hatua umekata tamaa kama Simon.

Usikate tamaa bado unayo nafasi ya kupata kile unachokihitaji, Yesu anataka kuona utii wako, kisha ukishamtii utaona matokeo ya ajabu. Simon kama angelikataa kutweka nyavu, asingepata kitu, lakini alipokubali alipata samaki wengi ambao alishindwa kuwabeba peke yake, hata mtumbwi wake ulishindwa kubeba akalazimika kuomba msaada kwa majirani ili wamsaidie kubeba samaki wake!

Hebu tii kile ambacho Mungu anakuambia kufanya, unajua kunawakati Mungu huongea na wewe akikutaka ufanye kitu ili mlango wa mambo yako ufunguliwe, lakini bahati mbaya sana huwa hujuwi kama Mungu anaongea na wewe. na siku zote kama Mungu akikusemesha halafu usijue kama ndiye anenaye nawe huwa ananyamaza kimya hatendi jambo lolote. angalia (1Sam. 3:1-8) utaona Mungu alikuwa akimwita Samwel ili azungumze naye lakini samwel alidhani kuwa alikuwa akiitwa na Eli babaye. Mungu alikaa kimya mara tatu, hadi pale Samwel alipotambua kuwa amwitaye siye Eli bali ni Mungu ndipo Mungu akasema naye!

Na Mungu anapokwambia jambo si lazima lifanane na jambo lingine ambalo limewahi kutokea kwenye biblia, maana Mungu husema na maisha ya mtu yeye kama yeye. hata kama ukiangalia kwenye biblia kila mtu aliagizwa kufanya mambo yake ambayo haya kufanana na ya wengine. Isaya aliambiwa avue nguo atembee uchi kama ishara ya kwamba Israel watakuwa uchi, Hosea aliambiwa akaoe kahaba tena kinyume cha sheria ili iwe ishara ya kwamba hao si watu wa Mungu na wala Bwana hawapendi.

Unajua Mungu huwa ananjia nyingi sana za kusema na watu wake, anaweza akasema kwa upole sana, anaweza akasema kwa sauti inayokuja ndani ya moyo wako kama mawazo walakini sio mawazo ila yanakuwa na msisitizo, anaweza akasema kwa ukali sana, anaweza akasema kwa utisho sana, anaweza akasema kwa ndoto. na nilichogundua ni kwamba Mungu anaongea na watu wengi sana katika kizazi hiki kwa njia ya mawazo na ndoto, lakini wenyewe hawamtambui! ningekuwa nafundisha somo la jinsi ya kumsikia Mungu tungeangalia kwa kina katika hili! kwa hiyo Mungu husema karibu na kila mtu amtafutaye! ndo maana utakuta uliota ndoto miaka titatu iliyopita lakini bado ile ndoto haijatoka kichwani. ndoto mpya zinakuja na kuzisahau mara baada ya siku moja tu, lakini ile bado ipo kichwani hadi leo, ifuatilie inaujumbe wa muhimu sana ndani yake.

Kama tulivyoona tabia za Mungu kuwa husema na mtu kwa namna tofauti. Kwa hivyo wewe usianze kuutafakari ujumbe wa Mungu uliokuja ndani yako ukidhani kuwa haujatoka kwa Mugu, eti kwa sababu hauendani na biblia, Mungu atanyamaza kimya hatasema tena na wewe mpaka pale utakapotambua kuwa yeye ndiye anayesema na wewe.

Hivyo Mungu akikwambia fanya usiwe mbishi, bali fanya kama Simon, hata kama kile anachokwambia kufanya ndicho hichohicho ambacho ulifanya na hukufanikiwa fanya tena maana kina nguvu ya Mungu ndani yake, ulipokuwa ukifanya wewe hakikuwa na nguvu ya Mungu lakini sasa kimekuwa na nguvu ya Mungu ndani yake maana Bwana anasema fanya! unaweza kuwa unasikia msukumo kutoa sadaka kwa mtumishi flani, au kwa mtu flani asiyekuwa mtumishi, pengine anaweza kuwa hata si mcha Mungu. usianze kushindana na huo msukumo, chukua hatua upesi, maana muda huo Mungu anakuwa ameshilikia ufunguo kuachilia Baraka za ajabu juu yako!

Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa Simon, alikesha usiku kucha akitafuta samaki lakini hakupata, yesu alipokuja kwake akamwambia kufanya tendo lile lile alilokesha akilifanya, simon hakuanza kubisha wala kujihoji ndani yake bali alifanya moja kwa moja, pamoja na kwamba alikuwa amechoka sana lakini alijikaza, na mara akapata samaki wengi sana.

Jifunze kumtii Mungu ili upate mafanikio yako upesi.

Bwana akushike mkono.

Ev.Moses mayil: NHM-Senior

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

2 Responses to Siri za kufanikiwa kupitia kwa Bwana!

  1. Yusha says:

    Amina,nimebarikiwa na somo.

    Like

  2. annajoyce nolasco kagombora says:

    vipengele vingine vya siri ya mafanikio bado hujavielezea tunatamani kujifunza yote

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s