Umeokoka; lakini kwanini bado matatizo yanakuandama?

mawazohaleluya watu wa Mungu.

Leo nimekuletea somo zuri sana, somo ni la muhimu sana.  Tafadhali fuatana nami! Kichwa cha somo letu ni:  Umeokoka; lakini kwanini matatizo bado yanakuandama?

Naweza kusema 100% ya watu waliookoka maisha yao huwa na furaha kwa muda na pia huwa na shida sana kwa muda, na mara zile shia huisha maisha yamakuwa na furaha kisha huja shida ama matatizo ya namna nyingine tena. na kwa bahati mbaya sana wengi huwa hawajuwi ni kwanini matatizo yanawafuata. vilevile wengi hudhani kuwa ni majribu. lakini ukweli ni kwamba yale huwa siyo majaribu. majaribu yapo lakini huwa sio kila upatwapo na tatizo ni jaribu. kwanza kabla hatujaendelea mbele tuone kwanza majaribu nini? majaribu ni vishawishi vya shetani ambavyo hukutega ili uiache imani. Lakini mada yangu hapa siyo majaribu, bali ni matatizo yanayowaandama watu waliookoka yana maana gani kwao.

Ukiangalia maandiko yanasema wamchao Bwana watalindwa usiku na mchana wala yule adui hatawagusa. pia maandiko yanasema wataishi kwa shangwe wala kilio na maombolezo havitasikika kwao! (Isaya 65:19….) lakini sasa mbona mambo yanakwenda vingine? watu wengi wakipatwa na shida hudhani kwamba wametenda dhambi, lakini kumbe hawajatenda dhambi!

Sasa hebu tuone; kwanini mambo haya huwapata sana watu wa Mungu, kiasi kwamba inafika hatua mtu wa Mungu umetamani kuwa na maisha kama ya yule jirani yako mwenye dhambi kwa kuwa yeye nyumba yake inavicheko kila kukicha.

Unajua Mungu hufanya kazi katika maisha yako kwa njia inayoitwa Agano (Mkataba) na ili Mungu akusaisie ni lazima afanye agano na wewe! ukiona Mungu anakusaidia bila kuweka agano naye basi ujue baba zak0 waliweka agano na Mungu juu ya kizazi chao!

Mungu alipokuwa akiwasaidia wana israel kule misiri alikuwa tayari kishafanya agano na baba zao Yakobo na Ibrahimu.

Nifuatilie vizuri nataka nikufundishe mambo ya msingi sana!na agano ni lazima liwe na vipengele ambavyo ni lazima vifuatwe bila kukiukwa! kwa mfano katika ajira mtu akifunga mkataba na mwajiri wake, hawezi kupandishwa mshahara au kushushwa kinyume na mkataba. kama mkataba unasema mshahara unaanza na sh.mil.1 unapanda na mshahara wa mwisho ni sh.mil.2. haitawezekana mshahara upande hadi mil.3 au ushuke hadi laki 9. vinginevyo mkataba huu utalazimika kuvunjwa ili uandikwe mwingine utakaoruhusu kiwango kupanda zaidi au kushuka zaidi.

Vivyo hivyo Mungu huweka agano na wewe; kwa mfano anaweza akaweka agano kwamba uchumi wako utakuwa kupata sh.5000 kwa siku. kwa hiyo haitawezekana kupata sh.10000 kwa siku hata kama ungekuwa mcha mungu kiasi kwamba ukitembea mawe hukuimbia hossana. kwa sababu hilo liko nje ya mkataba. sasa ili uweze kupata sh.10000 itabidi agano la kwanza la sh.5000 livunjwe kisha liletwe jingine la sh.10000.

Nifuatilie vizuri: Kama agano likishavunjwa ni lazima uchumi uharibike ghafla maana lile agano lililokuwa linasababisha kupatikana sh.5000 halipo tena! hivyo hata ile sh.5000 haitapatikana tena. utajaribu sana kuulejesha uchumi wako katika hali nzuri lakini haitawezekana. kila kitu utakachokuwa ukijaribu kukifanya ni lazima kishindikane, kama ni biashara ni lazima ishindikane; kama ni mimba ni lazima iharibike! na kama ni ndoa ni lazima ikose amani. na Mungu huwa haweki agano juu ya agano jingine bali huliondoa kwanza lile lililotangulia. maana biblia inasema hakuna ajengaye msingi juu ya msingi mwingine. inamaana kwamba ule wa kwanza lazima ubomolewe, ndipo ujengwe mpya.

Angalia pia Luka 5:37 ‘Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama akitia, ile divai mpya itavipasua vile viriba, divai yenyewe itamwagika, na viriba vitaharibika.’

Hapa Yesu aliongea kwa busara sana, anasema hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu, akaongeza kusema akitia   ile divai mpya itavipasua vile viriba, divai yenyewe itamwagika, na viriba vitaharibika.’ kwa hiyo kumbe ndiyo maana Mungu hulazimika kuliondoa kwanza agano la kwanza ili akiweka la pili lisiharibu (viriba) mafanikio yako yatakayotokana na agano jipya maana yananguvu kuliko lililopita.

Hivyo mtu wa Mungu ukiona mambo yako hayaendi, usianze kutafuta mchawi wako, tambua katika ulimwengu wa roho agano limeondolewa, sasa hapa kunamatokeo ya aina mbili, aidha mafanikio yako kupanda au mafanikio yako kushuka.

Kwa hiyo ukiona agano limeondolewa mtafute Mungu kwa bidii sana ili agano la pili liwe na nguvu kulio hilo liliondolewa!

Bwana akupe ufahamu zaidi katika Jina la Yesu.

Ev.Moses Mayila – Senior NHM

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

2 Responses to Umeokoka; lakini kwanini bado matatizo yanakuandama?

  1. trophaina wilson says:

    Asante saana kwa somo zuri limenipa kitu kipya ambacho nilikuwa nimekipoteza sasa nitafanya maagano mapya na Mungu wangu ili shida zangu zikome niendelee kwenye mafanikio.ubarikiwe

    Like

  2. sebaastian says:

    maombi yakufunja agano yanafanyajwe

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s