Mtu mmoja anafanya mauji kwa bunduki na kisu mjini taarime!

Aua watu saba, ajeruhi kadhaa! polisi waingia full armed kumtafuta!

Mauaji ya kutisha yametikisha wilaya ya
Tarime kiasi cha kumfanya Mkuu wa Jeshi la
Polisi (IGP), Ernest Mangu, kutuma timu
maalum kutoka makao makuu ya jeshi hilo
inayohusisha kamisheni ya Operesheni
kufanya uchunguzi.
Hatua ya kupelekwa kwa timu hiyo
inatokana na mauaji ya mfululizo katika mji
wa Tarime ambayo ipo kwenye himaya ya
Kanda Maalum ya Polisi ya Tarime na Rorya
ambayo yametokea kwa watu wanane katika
kipindi cha siku tatu.
Mauaji hayo yanadaiwa kufanywa na jambazi
mwenye silaha katika mji wa Tarime mkoani
Mara kwa siku tatu kuanzia Jumatatu hadi
jana.
Mmoja wa watu waliouawa ni askari mstaafu
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),
Koplo Zakaria Chacha Mwita ambaye ni mtoto
wa marehemu Meja Jenerali Mwita Marwa.
Pia wamo aliyekuwa Mhandisi Ujenzi Wilaya
ya Rorya, aliyetajwa kwa jina la David Mwasi
Misiwa.
Wengine ni mfanyabiashara, Samuel Richard
Mohenga na huku Jeshi la Polisi likisema
kuwa linaendesha msako.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya
Tarime/Royra, Justus Kamugisha, alithibitisha
kutokea kwa mauaji hayo na kusema kuwa
mtu anayesadikiwa kuwa jambazi akiwa na
bunduki kwa siku tatu kuanzia Januari 26,
mwaka huu usiku aliua watu saba kwa
kuwapiga risasi na kujeruhi kadhaa.
Aliwataja wengine kuwa ni mwendesha
bodaboda, mkazi wa kijiji cha Nkende, Juma
Marwa Nyaitara, Erick Lucas Makanya,
mfanyabiashara wa bucha mkazi wa kijiji
cha Rebu, Juma Mwita Mroni na mkazi wa
kijiji cha Kenyamanyori, Robert Chacha
Kisiri.
Jana asubuhi, wakazi wa mji wa Tarime na
vitongoji vyake walimfananisha mtu
aliyekuwa amevaa koti refu na mtuhumiwa
wa mauaji hayo na kutaka kumshushia
kipigo, lakini aliokolewa na polisi waliorusha
risasi hewani na kumpeleka katika kituo cha
polisi.
Kamanda Kamugisha aliwashauri wananchi
kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa
kutoa taarifa mara watakapomuona
mtuhumiwa.

Advertisements

About New Hope Ministry

Our ministry is based on Preaching the Gospel all over the world we preach the Gospel and we plant churches around the world. Contact us: Mobile: (255) 787589475 E-mail: newhopeministrytanzania@gmail.com
This entry was posted in HOME. Bookmark the permalink.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s